Watu 8 wahofiwa kufa baada ya boti kupotea baharini. Watatu wapatikana hai Kenya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Upepo mkali uliotoka jana Mcheweni Pemba umepeleka kupotea kwa boti mbili zikiwa na jumla ya watu 8

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohammed Shamim ameseama licha ya juhudi zilizochukuliwa na serikali pamoja na kamati ya uwokozi laki bado watu hao hawajaonekana wala kujuwa taarifa yoyote na hadi hii leo hawajafanikiwa .

Orodha wa watu hao amabao walikuwemo kwenye boti hiyo ni pamoja na Moh’d Makame, Omar Ali, Kombo Ali, Rashid Othman, Mwalim Bosi Faki, Kombo Faki, Omar Kombo na Said Ali Omar

===============

Wavuvi watatu kati ya wanane wa kijiji cha Shumba Wilaya ya Micheweni Pemba, waliokuwa wamepotea kwenye boti 2 wamepatikana wakiwa hai eneo la Watamu nchini Kenya huku mwenzao 1 akihofiwa kufariki

Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Haji Khatib Kai, alisema wavuvi waliopatikana ni Omar Ali Hassan (50), Kombo Ali Hassan (40) na Rashid Othman Ali (30) wote wakaazi wa kijiji cha Shumba Micheweni

Mbunge huyo alisema, ambao hawajaonekana na wala hakuna taarifa zao ni pamoja na Kombo Fakih Mwalimu (55), Mwalimu Bosi Faki (32), Said Ali Omar (50) na Omar Kombo Fakih (25) waliokuwa chombo kimoja.

Aidha, Mbunge huyo wa Jimbo la Micheweni alilalamikia kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa kutokuwa na ushirikiano wa hali ya juu kwenye shughuli ya uokozi
 
Hii
Watu 8 wahofiwa kufa  kutokana  na  boti kupotea baharini

Upepo mkali uliotoka jana Mcheweni Pemba umepeleka kupotea kwa boti mbili zikiwa na jumla ya watu 8

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohammed Shamim ameseama licha ya juhudi zilizochukuliwa na serikali pamoja na kamati ya uwokozi laki bado watu hao hawajaonekana wala kujuwa taarifa yoyote na hadi hii leo hawajafanikiwa .

Orodha wa watu hao amabao walikuwemo kwenye boti hiyo ni pamoja na Moh’d Makame, Omar Ali, Kombo Ali, Rashid Othman, Mwalim Bosi Faki, Kombo Faki, Omar Kombo na Said Ali Omar
Hii ni habari maya sana. Je hizo livejacket zilikuwa za hao waiopotea?
 
Back
Top Bottom