Watu 7 wenye funguo za kuzima na kuanzisha upya internet..

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,123
Je wajua kuna watu 7 pekee duniani wenye funguo za kuanzisha internet upya duniani iwapo kukitokea tukio lolote litakalo sababisha janga kubwa duniani ambalo linaweza zima mtandao.
Programme hii inaangaliwa na kampuni iitwayo ICANN (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers).
Watu hawa saba (7) wenye funguo hukutana mara moja kila mwaka, ambapo pia wana back up ya watu wengine saba(7) hawa backup wenyewe hawana haja ya kukutana ila kila mwaka wanatakiwa piga picha wakiwa wameshika gazeti la siku husika pamoja na kadi/smartcard zao kuonyesha uhalali wao.
Ili kuweza kushikilia funguo hizi, watu hawa wanatakiwa kuwa na historia ya kufanya kazi katika masuala ya ulinzi wa mitandao na kwenye taasisi mbalimbali. Walichaguliwa kwa kuangalia ujuzi wao na maeneo mbalimbali wanayotoka duniani , pia haitakiwi nchi moja kuwa na washika funguo wengi.
Ingawa wapo saba(7) lakini wanaotakiwa kuweza anzisha upya system ni atleast watu watano(5) na kila mmoja ana kipande tu cha system ina maana mpaka kuianzisha system ni atleast upate vipande vitano(5) toka kwa hawa watu saba (7).
Seven Internet Keymasters:-
- Paul Kane Great Britain
- Dan Kaminsky United States
- Jiankang Yao China
- Moussa Guebre Burkina Faso
- Bevil Wooding Trinidad and Tobago
- Ondrej Sury Czech Republic
- Norm Ritchie Canada

Meet the seven people who hold the keys to worldwide internet security
 
Back
Top Bottom