Watu 7 wakamatwa kuhusiana na mauaji ya Mabina

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Serikali bado inazidi kuonyesha unfair justice kwa umma wa Tanzania mara baada ya kamata kamata ya watu wanahusika na kumuuwa Bwana Clemet Mabina alipokuwa anapora shamba la wanakijiji.

Huu alikuwa anafanya wizi kama wezi mwingine ila kwa kuwa yupo kwenye chama cha serikali tungojee mengi kutokana na hili.

Ni watu na raia wangapi wanakufa na hakuna kamatakamata wala uchunguzi unaofanyika???

Bomu la Kanisani, bomu la soweto na mengine mengi kwanini iwe kwa wanachama wa CCM na vibaraka wake tu???
 
Naona kuna special people huku tz but tutafika tu tunakoelekea wa Tanganyika,
 
Usiongozwe na ushabiki mtoa mada.

Sheria za nchi zipo ni lazima zifuatwe na sio kujichulia sheria mkononi. Kwa sasa imekuwa ni tatizo mkigombana na mtu tu mtaani anakuitia mwizi. Halii hii ni hatari wapo watu waliuawa na wananchi ambao sio wezi.

Lazima tuelimike watanzania kutojichukulia sheria.
 
Serikali bado inazidi kuonyesha unfair justice kwa umma wa Tanzania mara baada ya kamata kamata ya watu wanahusika na kumuuwa Bwana Clemet Mabina alipokuwa anapora shamba la wanakijiji.

Huu alikuwa anafanya wizi kama wezi mwingine ila kwa kuwa yupo kwenye chama cha serikali tungojee mengi kutokana na hili.

Ni watu na raia wangapi wanakufa na hakuna kamatakamata wala uchunguzi unaofanyika???

Bomu la Kanisani, bomu la soweto na mengine mengi kwanini iwe kwa wanachama wa CCM na vibaraka wake tu???.

Sasa wakazi wanakimbaia nyumba zao kisa mporaji aliyepewa hukumu inayomstahili
 
Mtoa mada anataka iwe sheria isiyoangalia nani ameuawa!

Sijui wewe unaishi wapi lakini DSM wezi wanachomwa moto mbele ya Polisi au wanakuta watu wamemchoma moto mwizi wao wanabeba maiti na kuondoka nayo hakuna anayekamatwa.

Umeshawahi kusikia mtu amefishwa mahakamani kwa mob justice? Kwani Mabina ana tofauti gani na watu wanaouawa na wananchi kwa kutuhumiwa wizi?
 
Sasa bandungu.....si'mlimchagua wenyewe mkampa uprezdaa wa jamhuri ya muungano ati kisa tu anasura nzuri!!!!!asa mnalalamika nini!!!!ndo'mpaka 2015 hiyo......kumaaaaaaa-nisha!
 
wananchi wamemuuwa diwani wao, maswali bado ni mengi sana katika hili tukio, ukoo wa panya hawashindwi kitu
 
Wao wakamate tu lakini ujumbe umewafikia kuwa wananchi wamechoshwa na dhuluma ya serikali ya CCM
 
Mtoa mada anataka iwe sheria isiyoangalia nani ameuawa!

Sijui wewe unaishi wapi lakini DSM wezi wanachomwa moto mbele ya Polisi au wanakuta watu wamemchoma moto mwizi wao wanabeba maiti na kuondoka nayo hakuna anayekamatwa.

Umeshawahi kusikia mtu amefishwa mahakamani kwa mob justice? Kwani Mabina ana tofauti gani na watu wanaouawa na wananchi kwa kutuhumiwa wizi?
Usiongee kitu uschikijua ww na akil zako hzo za usku,wale waliowauwa wala mabaunsa tegeta mbona walihukumiwa? Au ni Dsm gani hiyo unayoisemea ww kwamba wezi wanachomwa moto mbele ya askar?

Qcha story za kwenye kahawa; iongeleee hiyo kwako ww au kwa baba yako mzaz ndo ujue how sweet it is.

Shabikieni upuuzi huu kesho atapigwa Mbowe tuone kama mtatetea upumbavu kama huu humu jamvini.

Nalaaani wote waliohuska na kumuuua huyo kiongozi,
 
Mtoa mada anataka iwe sheria isiyoangalia nani ameuawa!sijui wewe unaishi wapi lakini DSM wezi wanachomwa moto mbele ya Polisi au wanakuta watu wamemchoma moto mwizi wao wanabeba maiti na kuondoka nayo hakuna anayekamatwa.

Umeshawahi kusikia mtu amefishwa mahakamani kwa mob justice?Kwani Mabina ana tofauti gani na watu wanaouawa na wananchi kwa kutuhumiwa wizi?

Sheria inatoa muongozo gani juu ya tukio kama hili!!!!?????
 
Very true! Tatizo kubwa sana hapa nchini kwetu hususani kwa viongozi wetu ni kufikiri kwa kutumia vichwa vya wengine. Watu hawataki kuwa creative. Eti kwa kuwa ni CCM basi atatetewa hata kama amebaka au kutishia kuua.

Hebu imagine angekuwa ni kiongozi wa Chadema yamemkuta hayo nini ingekuwa suluhisho kama siyo kimya cha hivyo vinavyoitwa vyombo vya dola.

Tukubali au tukatae, haya ni matokeo ya kupuuuza mambo kwa kufikiri kwamba unmkomoa adui yako. Unapokuwa kiongozi wa Taifa lenye watu zaidi ya Milioni 45 halafu wewe ukafikiri kwamba wewe ni kiongozi wa kikundi cha watu wachache, haya ndiyo matokeo yake. Na huu ni mwanzo tu, bado wananchi wanaendelea kutoka gizani!

Time will tell........
Mtoa mada anataka iwe sheria isiyoangalia nani ameuawa!sijui wewe unaishi wapi lakini DSM wezi wanachomwa moto mbele ya Polisi au wanakuta watu wamemchoma moto mwizi wao wanabeba maiti na kuondoka nayo hakuna anayekamatwa.

Umeshawahi kusikia mtu amefishwa mahakamani kwa mob justice?Kwani Mabina ana tofauti gani na watu wanaouawa na wananchi kwa kutuhumiwa wizi?
 
Usiongozwe na ushabiki mtoa mada.

Sheria za nchi zipo ni lazima zifuatwe na sio kujichulia sheria mkononi. Kwa sasa imekuwa ni tatizo mkigombana na mtu tu mtaani anakuitia mwizi. Halii hii ni hatari wapo watu waliuawa na wananchi ambao sio wezi.

Lazima tuelimike watanzania kutojichukulia sheria.

bado kapuya, akikatiza kwenye sehemu ya watu wenye hasira kali watampinga tu!
 
Alishinda udiwani kwa kishindo. Je wapiga kura wake walikua wapi wasimtetee ? Au alishinda kwa kura za wizi ?
 
Serikali bado inazidi kuonyesha unfair justice kwa umma wa Tanzania mara baada ya kamata kamata ya watu wanahusika na kumuuwa Bwana Clemet Mabina alipokuwa anapora shamba la wanakijiji.

Huu alikuwa anafanya wizi kama wezi mwingine ila kwa kuwa yupo kwenye chama cha serikali tungojee mengi kutokana na hili.

Ni watu na raia wangapi wanakufa na hakuna kamatakamata wala uchunguzi unaofanyika???

Bomu la Kanisani, bomu la soweto na mengine mengi kwanini iwe kwa wanachama wa CCM na vibaraka wake tu???

Hivi wewe ulieleta hii post uwezo wa akili upo sawa sawa kweli! Mbona watanzania tunafika sehemu tunakuwa na ujinga uliopitiliza? Hivi kwa uelewa wako hafifu unadhani kuna Sheria inayomruhusu mtu kunyofoa uhau wa mtu hatakama unahisi mtu huyo amekukosea! Kwahiyo ulitaka Serikali ikae kimya hata baada ya mauaji hayo kutokea! Kwanini ushabiki wa kisiasa na itikadi za kijinga tunaziruhusu zififishe uwezo wetu wa kufikiri. Hii ni aibu kwakweli.
 
Hata kama ni mwizi sheria za Tanzania haziruhusu mwizi kuuwawa, bali anatakiwa kupelekwa kwenye vyombo husika, Hao Wananchi wamevunja sheria.
 
Mauwaji ya Clement Mabina sio mob justice kama mnavyodai wengi! Watanzania tumefikia hatua mbaya ya kuangalia kila jambo kwa mwanga wa vyama. Kilichotokea Kisesa ni uhalifu kama uhalifu mwingine tena uliopangwa na kuratibiwa kwa ustadi mkubwa. Ila kwa vile Watanzania tumejizoeza kubwabwaja na kuacha kanuni muhimu ya Mao " ...no research no right to speak.." RIP Clement Mabina na wengine wote waliouawa kwa Uonevu kw kile kinachoitwa mob justice!
 
Mnakumbuka ya Mzee Ditopile pale njia-panda ya Kawe? Alishuka ktk gari, akachomoa bastola, akampiga risasi ya kichwa na kumuua dereva wa daladala, akashitakiwa na DPP kwa kosa la kuua bila kukusudia!
Lakini, Mungu si athumani, Mungu mwenyewe akaamua kumpa kumwondosha duniani!
Tanzania kwa sasa unapata haki lazima uwe na cheo, unafahamika na uwe na pesa, la sivyo usahau!
Pia linganisha wa kauli inayodhaniwa kuwa ya Kapuya sisi ndiyo wenye nchi, serikali, we utashindana nasi? Vionghozi wamejisahau na kulewa madaraka. Ndiyo maana kuna kila sababu ya kuadilisha utawala.
Ewe Mwenyezi Mungu, iangalie dhuluma hii dhidi ya watu wako, wanyonge uwatetee dhidi unyanyasaji unaozidi kuongerzeka.
 
Back
Top Bottom