Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Watu saba wa familia moja katika kijiji cha Kibuhi wilaya ya Rorya mkoani Mara,wamefikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma, kwa ajili ya matibabu,baada ya kula mbona za majani aina ya Mgagani zinazodaiwa kuwa na sumu na kusababisha kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kupoteza fahamu huku baadhi yao warukwa na akili na hivyo kuwafanya kukimbia ovyo.
Baadhi ya ndugu wa wagonjwa hao,wameiambia ITV katika hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Mara mjini Musoma kuwa,jioni ya aprili nane mwaka huu,mama mmoja wa familia hiyo,anadaiwa kuchuma mboga hizo katika moja ya shamba kijijini hapo,kisha kuzipika na kula yeye na familia yake kama chakula cha jioni,na kwamba baada ya muda mfupi walianza kujisikia kizunguzungu kabla ya kupatwa na magonjwa hayo.
Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Mara Bi. Edinnes Makoba,amethibitisha kupokea wagonjwa hao ambao wanadaiwa kula mboga hiyo ya majani aina ya Mgagani.
Chanzo: ITV