Watu 66 na pikipiki 34 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvamia mgodi wa North Mara

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
2,870
2,000
Watu 66 na pikipiki 34 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvamia mgodi wa North Mara, unaomilikiwa na Acacia, DC Glorious Luoga anaongea na waandishi wa habari.
Screenshot from 2017-06-23 18-36-43.png


figganigga Said; DC Luoga anasema "Yalipotokea mambo haya, Watu walipotosha sana waliongea sana kwenye mitandao, na kadharika sisi tukasema hatuongei ila tunafanyia kazi swala hili. Sasa Waandishi leo mpo hapa, mtapima wenyewe ninayoongea na yaliyofanyika". Amesema Glorious Luoga mkuu wa Wilaya ya Tarime.

" Wavamizi mumesikia wenyewe hapa, wengine wametoka Serengeti, Wengine wanatoka Rorya. Hoja kubwa watu waliosimama nayo ni Walivamia wanadai fidia. Si kweli. Hiyo ni hoja watu walitengeneza Baadae. Na hata aliye hamasisha hakusema kwa kuwa mnadai fidia twendeni, alisema kwakuwa hawa ni wezi twende. Wala hoja haikuwa kudai fidia". Amesema Luoga.

Amesema atakaa na watu wa mgodi na pamoja na kudai fidia atawaeleza pamoja na haya vilevile atatengeneza meza ya mazungumzo ndani ya Wilaya kuona manufaa makubwa ambayo wananchi wanaweza wakayapata, hivyo amewaomba wananchi watulie.

"Tumekutuma bungeni ukafanye kazi kwaajili ya watanzania, ukalinde masirahi ya Watanzania ukalinde sheria za nchi ukafuate taratibu, huwezi kutetea masirahi ya wananchi kwa kuua mtu. Kwahiyo walivyotajwa Rugemalira nani nani ni wezi kwahiyo tukawaue majumbani kwao? Sheria inashughulika. Diwani akitokea binti yako mwizi waje wamuue?. Mule ndani kuna mali za watu kwanza kuna mali Muwekezaji. Kwanza dhahabu ni mali ya watanzania wote isipokuwa pale ambapo ipo watanufaika zaidi kuliko mtu wa songea kuliko mtu wa mbeya". Amesema Luoga.
screenshot-from-2017-06-23-19-35-04-png.529502

Glorious Luoga Mkuu wa Wilaya Tarime

Hivi tukimruhusu leo intruder akavamie kule akachukue dhahabu, kwa kitendo hicho tutaongeza mshahara wa Mwalimu? Na yule hatuibii sisi tutapata madawa hospitali? Nlishangaa kuna sehemu nliona wamemquote sijui Tundu Lissu Sasa mbona hawa rais alishasema ni wezi, sasa kwanini Polisi wanawapiga mabomu? [Lissu: Kama ACACIA ni wezi, kwanini Polisi wamewapiga Mabomu wananchi wa Tarime?] Kuna wezi wengine tena wamekuja, ile dhahabu pale ni mali ya watanzania. Unapoiba inatuibia sisi Watanzania. kasema Luoga.


Polisi ni chobmo cha kulinda raia na Mali, na ile dhahabu ni mali yetu. Aliyekuja kuvamia ni juma, lakini Abdallah yupo Dar es Salaam hajaja hapa na anapaswa na yeye kunufaika na ile dhahabu iliyopo nyamong'o ndo maana tunaitetea. amesema Luoga.

Tumekamata watu zaidi ya 60 na msako bado unaendelea, mbona yeye hakufika aingie kule. Mara kule alisema yeye kidume ngangari, si angefika hapa?

screenshot-from-2017-06-23-19-32-43-png.529501

Mourice Okinda

Naye OCD wa Nyamwaga Mourice Okinda amesema, "Serikali inaogopa sana kuua wananchi wake na kutumia vyombo vya dola, lakini kwa hali iliyokuwepo juzi ilikuwa ni hali ngumu sana kwasababu vijana walihamasika walikuwa na mapanga nafikiri mapanga yaliuzwa mjini yakaisha, Lakini kilichonisononesha kupita kiasi Hawa waliokuwa wakihamasisha watu, tutawatafuta na tutawakamata, taarifa zao tunazo. Kwasabau walifanya makosa makubwa sana, kuhamasasha wanawake wajawazito na wazee. Tulishindwa hata baadhi ya maeneo kutumia vihusika vilivyokuwa vinatakiwa. Kuwezi kupeleka bomu la machozi unamuona mama amebeba mtoto, zaidi ya mama 20 wamebeba watoto mgongoni. anahangaika kutafuta, amedanganywa huyu". kasema Okinda.

Wanawake mjamzito ameebeba mtoto yupo kwenye kinu cha dhahabu. Tulipowahoji wakasema wameambiwa waende kuchukua dhahabu.
 

SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,638
2,000
Dc wakat anashadadia hayo anapaswa kuhakikisha wananchi walioupisha mgodi WAMESHALIPWA FIDIA YA KUUPISHA MGODI
 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Habari ambazo muda huu,

Watu 66 na pikipiki 34 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvamia mgodi wa North Mara, unaomilikiwa na ACACIA, DC Glorious Luoga asema.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,196
2,000
Watulie wafate sheria kwa lolote wanalodai, wanaona Mkuku yupo bizi kueeka mambo sawa eao wanataka kurudisha mengi nyuma ili basi tu.

Lazima ambao hawapendi anayofanya Magufuli wanawasukuma ili wapate vyao... hata kama kuna tatizo tunalolisikia why noe, wakivunja mali au kuharibu wanataka serikali isemeje.. ilipe au watalipa?
 

Igurumuki Masanja

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
480
1,000
Watu 66 na pikipiki 34 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvamia mgodi wa North Mara, unaomilikiwa na Acacia, DC Glorious Luoga anaongea na waandishi wa habari
HECHE kama nawe ni member hebu funguka tusikie maoni ako

leo jimbo zima limevamia au ndo desituri yao ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom