Watu 600,000 wanaolitegemea ziwa Nyasa ni wepi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu 600,000 wanaolitegemea ziwa Nyasa ni wepi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tindikalikali, Aug 8, 2012.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Toka umeibuka mtafaruku huu umeanza, wanasiasa wetu wametoa kauli mbali mbali hasa zinazoashiria shari huku wakitumia kigezo cha kuwalinda watu laki 6...

  Mi bado najiuliza hao watu laki 6 wanatoka wapi? Je ni hawa watu wanaokaa ukanda wa Matema Beach na kutengeneza vyungu, au hawa wavuvi jirani na Itungi port ambao bado wanatumia mitumbwi ya kupalasa kwa mikono kufanya uvuvi?
  Nani asiyejua kwamba tumeshindwa kufanya uvuvi endelevu na bei za samaki hazikamatiki tena ukanda ule?
  Nani asiyejua kuwa usafiri wa meli unasua sua kama siyo kufa kabisa?

  Wanasiasa wetu lazima wajue kwamba tumeshindwa kulitumia ziwa ili kwa tija, kama inawezekana wawaachie hao wanaoweza kulitumia, hizi gharama za vita wanayoihubiri ikafanye mambo mengine ya msingi...

  Sisemi raia hata kama ni wachache wasilindwe, kinachotakiwa ni kusimama katika ukweli na kusimamia nguvu ya hoja, hawa wamalawi siyo wendawazimu, hilo lazima tulijue

  NB; nina taharifa zisizo rasmi kwamba, ndege za Tanzania zilianza utafiti wa mafuta na gas toka mwezi June mwaka huu.
   
Loading...