Watu 5 mbaroni kwa kukutwa na nyaraka za serikali za kugushi.

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000


Idara ya uhamiaji nchini inawashikilia watu watano wakiwemo Afisa polisi mstaafu na mtumishi wa halmashauri ya jiji mstaafu wakiwa na nyaraka mbalimbali za serikali za kugushi na mihuri 50 tofauti tofauti ya ofisi za serikali na mawakili.

Kamishina wa Usimamizi na udhibiti wa mipaka bw Samuel Magweiga amesema watuhumiwa hao wamekamatwa jijini Dar es Salaam wakiwa katika ofisi alizodai kuwa wanafanyia utapeli huo wakiwa na nyaraka hizo na kuongeza kuwa upelelezi umekamilika na watafikishwa mahakamani.


Kati ya nyaraka ambazo watuhumiwa hao wamekutwa nazo ni pamoja na vyeti vya kughushi vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam na katika hali isiyokuwa ya kawaida watuhumiwa hao wakati wanahojiwa na waandishi wa habari wakiwa katika ofisi za makao makuu ya idara hiyo wamekana kutokuhusika na ofisi hiyo huku kila mmoja akidai kuwa alipitia ofisini hapo kusalimia.

Chanzo: ITV
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,861
2,000
Hao kumbe ndio wazalisha vyeti feki ee?? Serikali ichukue hatua kali dhidi yao
 

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Feb 1, 2015
1,671
2,000
Hao jamaa nimewaona nikajiuliza hivi wameshaingiza kiasi gani kwa hawa walimu wa kikenya,kizimbabwe na hawa wanaijeria na wakongo waliojaa mitaani. Wanafoji mpaka permit jamaa ni kiboko hao.
Kulionekana nyaraka za kupata leseni za maduka, leseni za vileo zinazotolewa na halmashauri.

Kweli hao jamaa wako vizuri
 

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,312
2,000
Hawa jamaa hawajaanza leo.Na tatizo letu watanzania tunapenda kuletewa chakula mezani lakini kujua kinapatikanaje hatutaki kujua.

Waandishi wa habari mpaka leo sijasikia kuhusu wale jamaa walikamatwa Dar na Kigoma wakiwa na mitambo yote ya kutengeneza vyeti mpaka masters.

Ni kimya kabisa kama vile hawakukamatwa watu wa vile ambayo tungejua hata kilochoendelea na ukweli kuhusu walichofanya maana may be ndiyo waliowaponza Hata wale 9932 waliofukuzwa na vyeti fake Serikali
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom