Watu 420,000 hufariki kila mwaka kwa kula chakula kisicho salama

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,840
2,000
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema watu wa wanaokadiriwa milioni 600 huugua kutokana na kula chakula kisichosalama na kati yao takribani watu 420,000 hupoteza maisha kila mwaka

Takwimu zinaonyesh kuwa wahanga wengi wa chakula kisichosalama ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huku pia madhara mbali mbali yanayohusiana na ulaji wa chakula kisicho salama yakiripotiwa katika matukio mbali mbali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS leo Juni 7, 2021, Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani, Kaimu Mkurugenzi wa Uthibiti wa Ubora, wa shirika la viwango Tanzania (TBS), Gervas Kaisi amesema magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama yanazuilika iwapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake katika mnyororo wa chakula.

Amesema usalama wa chakula ni nyenzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa na kuepuka kupoteza mapato na kukataliwa kwa chakula kingiapo sokoni kwa kutokidhi viwango vya ubora kwani ni hitaji muhimu kwa afya na ustawi wa Jamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Maadhimisho hayo ya siku ya chakula duniani mwaka huu yenye kauli mbiu 'Chakula salama sasa kwa afya njema kesho' yanalenga kukumbusha, kuelimisha na kuongeza uelewa wa jamii juu ya usalama wa chakula kutoka shambani, majini hadi kufika kwa mlaji kuonesha namna ya kujikinga na maradhi kupitia chakula salama.

"Sote tunatambua kwamba chakula salama ni hitaji muhimu kwa afya na ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla kitu ambacho kinasababisha usalama wa chakula katika kulinda afya ya jamii na uchumi wa nchi...., pia chakula salama ni nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu hasa, kuondoa nm umaskini, kutokomeza njaa pamoja na kulinda afya ya jamii na ustawi wake. Amesema Kaisi.

Ameongeza kuwa, wananchi wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa chakula wanachonunua ni salama kabla ya kula au kukitayarisha na pia ni muhimu kwa walaji kukagua chakula ili kuhakikisha kuwa hakijaharibika, kuisha muda wake wa matumizi au kuchafuliwa kwa namna yoyote.

"Walaji wanayo haki ya kupata taarifa kuhusu chakula kwa kupitia maelezo yaliyoandikwa katika lebo za chakula husika na ni muhimu kuhakikisha kuwa taarifa hizo zimewekwa kwa kuzingatia viwango, kanuni na miongozo, amesema Kaisi.

Naye, Rose Shija muwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), amesema, kwa mujibu wa benki ya dunia kila mwaka chakula kisicho salama kinagharimu nchi za kipato cha chini na cha kati pekee kiasi cha USD bilioni 95 katika uzalishaji uliopotea.

Amesema uzalishaji na matumizi ya chakula salama una faida za haraka na za muda mrefu kwa watu, mazingira ya Dunia na uchumi. "Upatikanaji wa chakula salama na cha afya kwa wote unaweza kuendelezwa kwa siku zijazo kwa siku zijazo kwa kuukubali uvumbuzi wa kidigitali, kuendeleza ufumbuzi wa kisayansi pamoja na kuheshimu maarifa ya jadi ambayoyamedumu na kuleta tija katika nyakati mbalimbali". Amesema Rose.

Amesema, WHO imedhamiria kuingiza na kuendeleza masuala ya usalama wa chakula katika ajenda ya Umma na kupunguza mzigo wa magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama.

Michuzi Blog
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom