Watu 36 Wajitolea Kufanyiwa Majaribio ya Kinga ya Ukimwi Afrika Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu 36 Wajitolea Kufanyiwa Majaribio ya Kinga ya Ukimwi Afrika Kusini

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Watu 36 Wajitolea Kufanyiwa Majaribio ya Kinga ya Ukimwi Afrika Kusini Tuesday, July 21, 2009 7:29 AM
  Afrika Kusini imezindua mwezi huu majaribio ya kinga ya ukimwi kwa binadamu na watu 36 wenye afya zao wamejitolea kufanyiwa majaribio kuthibitisha uhakiki na usalama wa kinga hiyo. Kwa mara ya kwanza kinga ya virusi vya Ukimwi iliyotengenezwa na wanasayansi wa barani Afrika inafanyiwa majaribio kwa binadamu.

  Kinga hiyo imezinduliwa jumatatu na imegunduliwa na wanasayansi wa Afrika Kusini katika chuo kikuu cha Cape Town.

  Watu 36 wenye afya ambao hawana maambukizi ya ukimwi wamejitolea kufanya majaribio ya kinga hiyo iliyotengenezwa na wanasayansi wa Afrika Kusini chini ya udhamini wa serikali ya Afrika Kusini alisema Anthony Mbewu, rais wa baraza la utafiti wa tiba la Afrika Kusini.

  Watu 12 nchini Marekani walijitolea kufanyiwa majaribio ya kinga hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.

  Mbewu alisema kuwa kinga hiyo iligunduliwa katika chuo kikuu cha Cape Town na walipewa msaada wa kiufundi na Taasisi ya afya ya Marekani ambayo ndio waliochukua jukumu la kuzitengeza dawa za kinga hiyo waliyoivumbua.

  Dr Anthony Fauci, mkurugenzi wa taasisi ya afya ya Marekani ya magonjwa ya kuambukiza na mmoja wa watafiti wakubwa wa ugonjwa wa ukimwi alikuwa nchini Afrika Kusini kwaajili ya uzinduzi wa kinga hiyo jumatatu.

  Baada ya miaka 10 ya kupuuzia suala la ugonjwa wa ukimwi, Afrika Kusini hadi mwaka jana ilikuwa na jumla ya watu milioni 5.2 wanaoishi na virusi vya ukimwi. Theluthi moja ya watu hao ni wanawake wenye umri mdogo kati ya miaka 20 na 34.

  Mwaka 1999 wizara ya afya ya afrika kusini ilizindua taasisi ya kufanya utafiti wa kutafuta kinga ya ukimwi na iliichangia jumla ya rand milioni 250 za Afrika Kusini katika kipindi cha miaka 10.

  Jumla ya wanasayansi na mafundi 250 wanashiriki katika mradi huo wa kutafuta kinga.

  "Serikali iliona kuna umuhimu wa kutafuta kinga ya ugonjwa wa ukimwi na kama ikigundulika walitaka iwafikie watu wengi kwa bei nafuu" alisema Mbewu.

  "Tuna janga kubwa kuliko yote duniani" alisema Mbewu na kuongeza "Nchi nyingi zinazoendelea kama vile Brazili na Korea zinajaribu kwa njia zao kugundua na kutengeneza kinga ya ukimwi"
  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2571954&&Cat=2
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mungu turehemu.
   
Loading...