Watu 35 wanashikiliwa na polisi Mwanza kwa kuchoma moto gari

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
msangi.jpg


Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 35 kwa tuhuma za kuchoma moto gari lililowagonga watoto wawili wa familia moja na kusababisha kifo cha mmoja wao katika barabara ya Igombe eneo la Kayenze ndogo wilayani Ilemela majira ya asubuhi juni 7 mwaka huu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa polisi Ahmed Msangi amemtaja mwanafunzi aliyefariki papo hapo kuwa ni Naomi Opio mwenye umri wa miaka 12 mwanafuzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kisundi, huku mdogo wake aitwaye Baton Opio mwenye umri wa miaka 9 anayesoma darasa la tatu katika shule hiyo akijeruhiwa kichwani na kuvunjika mkono wa kulia na amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou toure kwa matibabu zaidi.

kamanda Msangi ameongeza kuwa katika tukio hilo wananchi hao pia wanadaiwa kumvamia na kumjeruhi dereva wa magari ya kwenda Igombe aliyefahamika kwa jina la Azizi Mohamed kwa kumpiga mawe na kumchoma na vitu vyenye ncha kali sehemu za mgongoni baada ya kuwasihi kuacha kujichukulia sheria mkononi kitendo ambacho ni kinyume cha sharia.

Kutokana na tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani humo Ahmed Msangi ameitaka jamii kujiepusha na matukio ya uvunjifu wa amani na kujichukulia sheria mkononi huku akiwasihi madereva kuwa waangalifu wawapo barabarani.
 
Ndiyo wakome walivyo wajinga wanafikiri kuna dereva huwa anatoka nyumbani kwa ajili ya kwenda kusababisha ajali
 
Ndiyo wakome walivyo wajinga wanafikiri kuna dereva huwa anatoka nyumbani kwa ajili ya kwenda kusababisha ajali
Madereva wengi hii nchi shule ndogo na akili ndogo. Ukosefu wa umakini, busara na kufuata sheria za barabarani husababisha vifo na majeruhi wasio na hatia.

Kosa moja barabarani hugharimu maisha ya watu wengine.

Dereva anashindwaje kutumia akili sehemu zenye shule na sehemu za miji kutembea taratibu?

Huyo dereva hao jamaa wamemuonea huruma, wangemtanguliza mbele ya haki.
 
Msangi ameongeza kuwa katika tukio hilo wananchi hao pia wanadaiwa kumvamia na kumjeruhi dereva wa magari ya kwenda Igombe aliyefahamika kwa jina la Azizi Mohamed


Yawezekana wingi wa magari anayoendesha ndiyo chanzo cha ajali
 
Halafu wakimtanguliza mbele za haki nini kinafuata huoni kwamba mtashitakiwa kwa kosa la mauaji?
 
Back
Top Bottom