#COVID19 Watu 29 wameshakufa kwa wimbi la 3 la Coronavirus. Wagonjwa wafikia 858 Tanzania nzima

Chapu shule za Kilimanjaro na Arusha zifungwe sio mpaka hali iwe mbaya zaidi. Na makanisani tahadhari iwekubwa
 
Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi sasa jumla ya watu 29 wamefariki kutokana na wimbi la tatu la Covid-19 huku jana pekee kukiwa na wagonjwa wapya 176.

Idadi hiyo inafikisha Tanzania kuwa na jumla ya wagonjwa 858 wa Covid-19.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dk Dorothy amesema takwimu hizo ni alizopata jana hivyo upo uwezekano vifo zaidi vikawa vimetokea.

Waziri ameeleza kuwa licha ya Serikali kuendelea kusisitiza watu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo bado wapo wanaozembea.

“Itoshe kuwaambia kuwa ugonjwa upo na watu wanakufa, tusingependa kupeana hizi taarifa za vifo tuchukue tahadhari, kila mmoja wetu ajiulize unapofanya mambo kinyume na kuchukuta tahadhari unalenga kumtesa nani,” amesema Dk Gwajima.

Waziri huyo pia alitupa lawama kwa viongozi wa Serikali ambao hawashiriki kwenye vita vya kupambana na ugonjwa huo.

“Nawakumbusha watu hawa wasiotaka kwenda mstari wa mbele wasichukulie mzaha Uviko 19, ugonjwa huu upo tusijiachie kwa sababu wimbi la kwanza na la pili lilipita,”.

Mwananchi
Ni zaidi ya hao, mara 100
 
Hizi takwimu mbona hazipelekwi WHO wala AfrIca CDC ?

Kuna mahali kitu hakipo sawa....zamani enzi za dada Ummy zilikuwa zikitangazwa zinareflect kote, ila mpaka sasa huko kwenye hizo taasisi za kimataifa hatutambuliki !
 
Hatujasahau ndugu zetu waliofariki kwa wingi January na February wimbi la pili lilipotokea huku huyu kibibi na wajinga wengine wakisema ugonjwa haupo ni changamoto tu za upumuaji...she will pay for it! We shall revisit
 
Hii Corona naona inachukuliwa kwa mzaha na wengi, sijui tatizo ni nini, nionavyo wabongo bila kuugua hawaamini kama huu ugonjwa upo, na huko hospitalini oxygen hakuna yakutosha.

Itachukua muda sana Corona kuondoka Tanzania, hizi kauli za Waziri wengi wanaziona kama matamko tu ya kisiasa, naamini ipo siku watu watazitafuta chanjo wenyewe, only a matter of time.
Tena watanzania walivyowaoga. Sasa hivi utaona mikusanyiko kwenye vituo vya afya kama usajili wa nida.
 
Hii Corona naona inachukuliwa kwa mzaha na wengi, sijui tatizo ni nini, nionavyo wabongo bila kuugua hawaamini kama huu ugonjwa upo, na huko hospitalini oxygen hakuna yakutosha.

Itachukua muda sana Corona kuondoka Tanzania, hizi kauli za Waziri wengi wanaziona kama matamko tu ya kisiasa, naamini ipo siku watu watazitafuta chanjo wenyewe, only a matter of time.
Mbona unateseka sana?
 
Watumishi wa afya wengi wameshachomwa chanjo..ndo mana wengi wao sikuhz hawavai barakoa
 
Nimekutana na watu zaidi ya 15 wanasema wanaumwa na vichwa ,istoshe kuna msiba jirani wanazikwa watu wawili Siku moja yaani mume na make kesho
 
Barakoa, lockdown, na chanjo won't help,,mnaoona hvo vtu kama first hand sanctuary, ni kufa tu hatuna jinsi,, in times like this ambazo hata chanjo hatuna uhakika nayo, watu inabdi muishi na kanuni bora za afya kwa ajili ya miili yenu,, upatie mwili chakula cha kujenga kinga kwa hali ya juu,, fanya exercise,, pata enough rest,,,

Watu wanaishi maisha ya bora twende,,, wakiganda kama ruba kwenye barakoa na sanitizer wakati maisha yao kiafya ni sawa na mraibu wa dawa za kulevya,,
 
Mkuu huu ugonjwa upo, mtaani kwangu nimezika wazee kama wa 3...
Ugonjwa una walakini huu! mkuu ukae ukijua kuzikana hatukuanza leo.Mfano huku kitaa watu wakifa utasikia eeh corona! hata ndugu tu wanashangaa.wanadandia vifo tu ili kuhalalisha ugonjwa wao
 
Mkuu huu ugonjwa upo, mtaani kwangu nimezika wazee kama wa 3...
Ugonjwa una walakini huu! mkuu ukae ukijua kuzikana hatukuanza leo.Mfano huku kitaa watu wakifa utasikia eeh corona! hata ndugu tu wanashangaa.wanadandia vifo tu ili kuhalalisha ugonjwa wao
 
Wamekopa maela ya wazungu bado wanatukamua tozo hawajamaa akili zao zimefika mwisho
 
Data za uongo hizo. Kijijini kwa mke wangu huko Moshi ambao wameshazikwa ni wengi. Mfano:
1. Mke na mume
2. Baba na mwanaye
3. Jirani 2
4. Kaka zake wa ukoo 2
5. Jana amezikwa ndugu Kwa shangazi yake
6. Kesho anazikwa mkwe alikoolewa mdogo wake
Hao ni 10 wa karibu. Vijiji vingine nako wanakufa na wengine kutoka mijini kuja kuzikwa.
Hivi maiti za say KCMC zilizokufa na Korona hizo mnaziweka wapi? Bado say Mount Meru.
Tuseme ukweli ili watu wajikinge hasa mikoa ambayo imeathirika Sana.
 
Back
Top Bottom