#COVID19 Watu 29 wameshakufa kwa wimbi la 3 la Coronavirus. Wagonjwa wafikia 858 Tanzania nzima

Mbona wewe haujazikwa? Kwani kabla ya corona wazee walikuwa hawazikwi? Kwani kufa ni ajabu? Msisingizie corona kwa kila kifo!! Kwa nini leo kila mtu akifa ni corona!! Kwani kupumulia kwenye mashine kumeanza baada ya corona? Ina maana kabla ya corona mitungi ya oxygen ilikuwa haitumiwi kabisa na wagonjwa hospitalini? Kwa nini leo kila anayepumulia kwenye mashine wanasema ni corona?? Huu ni ujinga wa kiwango cha juu!!
Mkuu afya ulinayo usifikiri na mwingine anayo, uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi usifikiri na mwingine anao huo uwezo, japo haya magonjwa inaweza kuwa ni project za watu lakini jua upo.... kwa muda huu ongezeko la utumiaji wa mashine za oxygen umeongezeka....
 
Kweli shetani ni mbaya sana. Kaleta Corona kuleta taharuki nafsini mwa watu ili wamsahau Mungu muweza wa yote ili wakazanie kiponyacho Mwili yaan chanjo, kuliko kiponyacho roho. Duh shetani mbaya na kawanasa wengi.

Hiyo inayoitwa Corona inaanzia rohoni na nafsini mwa mtu ndipo matokeo yanakuja mwilini sasa na Bahat mbaya wengi wananitahidi kupambana na hali ya nje kuliko ya ndani.

Bila kujua adui unaepambana nae huwezi kujua namna ya kumshinda zaidi atakushinda. Mimi na nyumba yangu tutamtumainia Mungu kama ni kuishi, tutaishi kwa Kristo na kama ni kufa tutakufa kwa Kristo. Hatuna hofu
Yaani unakuja kabisa na kuandika kuwa ugonjwa hakuna kwa sababu unafuata Imani za kuletwa hukohuko Wanakosema ugonjwa upo. Hivi huoni albu kuacha kufuatilia na kuabudi dini za mababu zako. Ulokole ni moja ya ugonjwa wa akili
 
Back
Top Bottom