Watu 29 wafa katika mkanyagano wa kusanyiko la Maombi, Liberia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Watu wapatao 29 wamekufa baada kukanyagana kwenye kusanyiko la maombi katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia hii leo. Polisi wamesema kuwa idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka. Kwa mujibu wa vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi maafa hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana.

Msemaji wa polisi Moses Carter ameliambia shirika la habari la AFP kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka kwa sababu baadhi ya watu waliojeruhiwa wamo katika hali mahtuti. Amesema watoto ni miongoni mwa waliofariki.

Dixon Seebo, mwakilishi wa kitongoji cha walala hoi cha New Kru ambako mtafaruku huo ulitokea, amesema watoto 11 wamepoteza maisha.

Vyombo vya habari vimesema kuwa bado kuna utatanishi kuhusiana na maelezo juu ya tukio hilo lililohudhuriwa na mkusanyiko mkubwa wa watu kwenye maombi ya Kikristo yaliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu katika kitongoji hicho cha New Kru.

Mchungaji Abraham Kromah, muhubiri maarufu nchini Liberia, aliandaa maombi ya siku mbili ambayo yaliuvutia umati mkubwa wa watu, kulingana na picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii.
 
Kafara ya damu ilikua inahitajika..naona mwamposa kaenda huko kutoa lecture.


#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu kafara sio kitu Fulani labda kinachoonekana kwa macho.....ni kile kitendo cha kumwaga/kuua kiumbe bila hatia Ili utimize haja/umridhishe kiumbe mwenzako..
Hivi huwa inatokea vipi mtu anaona kabisa hatari lakini bado anaisogelea hatari hiyo?

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
Sawa wakuu, natamani tungejadili lakini kichwa kinaniuma kidogo, mambo ni mengi.
 
Back
Top Bottom