Watu 28 wajinyonga Geita ndani ya miezi 6

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,006
9,872
Watu 28 wamefariki dunia kwa kwa kujinyonga mkoani Geita ndani ya miezi sita iliyopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya mkazi wa Nyang’wale aliyejinyonga kwa sababu za kuolewa na kuachika mara tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe ameyasema hayo leo Februari 17, 2022 wakati akizungumza na viongozi wa kamati ya amani ya mkoa huo.

Mwaibambe amesema watu hao 28 ni miongoni mwa vifo 49 vilivyotokea kwenye mkoa huo ndani ya miezi sita kuanzia mwezi Agosti mwaka 2021 hadi Januari 2022 ambapo vifo vingine vya watu 21 vimetokana na mauaji.

Amesema kuwa kati ya mauaji ya watu 21, mauaji ya watu 10 yalitokana na wivu wa mapenzi 10, ushirikina mawili, uhalifu matatu huku mauaji ya ugomvi wa kawaida yakiwa nane.

Amesema mkoa wa Geita awali uliripotiwa kwa mauaji ya wazee na ushirikina lakini sasa hali imebadilika na kuwa mauaji ya kujinyonga ndio yanayoongoza.

Kamanda amewaomba viongozi wa dini kutoa elimu ya kiroho kwenye makanisa na misikiti ili kuwafikia watu walio wengi.

Wakizungumza kwenye kikao hicho viongozi wa kamati ya amani wamesema sababu kubwa ya mauaji ni mmononyoko wa maadili kwenye jamii.

Shehe wa Mkoa wa Geita, Alhaji Yusuph Kabaju amesema mbali na mmomonyoko wa maadili lakini kitendo cha wanaume kuwaacha wake zao na kudai mahari imekua manyanyaso kwa wanawake na hivyo kukata tama ya maisha.
 
Back
Top Bottom