Watu 25 mbaroni kwa kuteka gari la maiti - SUA

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,667
Polisi mkoani Singida. limefanikiwa kuwakamata watu 25 wanatuhumiwa kuteka gari la Chuo Kikuu cha Sokoine, na kisha kuwapora fedha watu waliokuwa wanasindikiza maiti iliyokuwa inapelekwa Mkoani Mara. Katika utekaji huo, jeneze lililokuwa mwili wa Muchari Lyoba, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chou cha SUA, lilifumuliwa na mwili wa marehemu ukapekuliwa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Singida' alisema katika msako mkali unaendelea, mbali na kukamatwa watuhumiwa, pia baadhi ya mali zilizoporwa zikiwemo nguo, kamera, kompyuta pakato (Laptop), na simu zimekamatwa.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na vitambulisho vya kazi, charger mbili za simu, kadi za Benki aina ya Tembo card, na shilingi 20,500 ziliokotwa katika eneo la tukio. Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi.
Alisema baadhi ya watuhumiwa baada ya kugawana sh 19.8 milioni walizopora walianza kunywa pombe hovyo, huku wakijitapa kuwa wakijitapa kuwa wana uwezo mzuri wa kiuchumi.
 
Maisha bora kwa kila mtanzania yameota mbawa, ndio maana watu wamefikia hatua ya kuteka maiti.
 
Siku si nyingi wataanza kufukua na makaburi kabisa kuchukua nguo na viatu vya marehemu
 
Polisi wa tz wakishasikia kuna mavumba(midako) lzm wafanye msako mkali,cha kusikitisha hizo 19.8mil sijui kama zitarudi hata sumni.....si umeona mil6 ya sharo hawajairudisha..
 
Siku si nyingi wataanza kufukua na makaburi kabisa kuchukua nguo na viatu vya marehemu

Maiti zilishafukuliwa siku nyingi hasa za Wajerumani ati wanatafuta rupia na vito vya thamani! Maendeleo ya miaka 51 ya baada uhuru ni bora kuliko ya miaka 51 kabla ya uhuru.
 
Hao washenzi walipaswa kutumbukizwa ndani ya pipa la Pombe linalochemka ili waendelee kunywa vizuri.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Malipo ni humuhumu unajisifia na rambirambi za marehemu du! aibu kubwa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom