Watu 2 wahukumiwa kwa hatia ya kusambaza Huduma ya Internet bila kibali na kuisababishia hasara TCRA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu Mhandisi Baraka Mtunga (43) na Rajabu Katunda (42) kulipa faina ya Sh. Milioni 1.5 kwa kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza Huduma ya Internet bila kibali na kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zaidi ya Sh. Milioni 200.

Pia washtakiwa hao, wametakiwa kulipa fidia ya Sh.Mil 267.656.794.30 baada ya kuingia makubaliano na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutokana na kukiri kwao makosa hayo.

Washitakiwa hao wamefanikiwa kulipa kiasi cha Sh.Milioni 200 kati ya fedha hizo.

Hukumu hiyo, imetolewa ba Hakimu Mkazi Mkuu, Kassian Matembele baada ya kupokea makubaliano baina ya washtakiwa na DPP na kukiri makosa mawili ya kutumia mitandao kilaghai na kuisababishia hasara TCRA.

Hakimu Matembele alisema Mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili, ambapo upande wa mashtaka uliomba adhabu kali itolewe na upande wa utetezi waliomba kupunguziwa adhabu kwa sababu washtakiwa wameonesha busara ya kukiri makosa yao.

Chanzo: Millard
 
Outdoor nadhani inahitajika leseni
Tcra wamekuja kuwa wasumbufu sana miaka hii hadi kuagiza simu saiv wanataka ulipie ukaguzi wa hiyo simu, sijui wana shida gani hawa watu.
Fafanua kidogo hapa yani mm ninunue simu then tcra waje waikague na nilipe pesa ya ukaguzi how!!?
ama ndio ukusanyaji wa mapato mpya!?
 
Back
Top Bottom