Elections 2010 Watu 19.6 mil kupiga kura mwezi huu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082


TUME ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza idadi ya wapiga kura Tanzania bara watakaopiga kura kuwa ni 19,694,416.

Tume hiyo pia imetangaza mabadiliko katika karatasi ya kupigia kura na sasa wananchi watakaopiga kura, watapaswa kuweka alama ya vyema kulia kwa mgombea wa chama anachokusudia kukichagua,badala ya kuweka alama chini ya picha ya mgombea kama ilivyozoeleka.

Wakizungumza katika mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya Mkoa wa Mwanza, Ofisa wa tume, Anna Ruganyoisa, alisema jumla ya wagombea walioteuliwa katika nafasi zote ni 8,980.

Alisenma wagombea saba miongoni mwa hao ni wanaowania urais na 1,041 wengine ni wanaogombea ubunge katika majimbo mbalimbali.

Ofisa huyo alisema walioteuliwa kugombea udiwani katika uchaguzi unaotrajiwa mwishoni mwa mwezi huu ni 7,932.

Mapema, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Omari Makungu, alisema kwamba kuanzia Oktoba 12 mwaka huu, karatasi za kupigia kura zilianza kusambazwa katika majimbo.

Alisema karatasi hizo zilisambazwa pamoja na vifaa vingine, lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa vinafika mapema majimboni.

Alisema katika hatua ya mwisho, vyama vinapaswa kuzingatia umuhimu wa kuchagua makala na kwamba ni vyema mawakala hao wakapangwa kulingana na maeneo wanayotoka, ili nao wapige kura.

"Mawakala hawa watapaswa kula kiapo siku tatu kabla ya uchaguzi, kwa hiyo tume inawaomba viongozi wa vyama vya siasa, kushirikiana nayo, ili kufanikisha uchaguzi," alisema.



Jaji Makungu alisema mawakala hao, wana wajibu mkubwa wa kulinda maslahi ya vyama wanavyowakilisha.
Hata hivyo alisema kuna haja kwa mawakala kuzingatia kanuni za uchaguzi, ili kuwezesha uchaguzi kuwa wa haki na huru.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom