Watu 15 washikiliwa na Polisi kwa kosa la kukutwa na pembejeo feki

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu kumi na tano kwa tuhuma za kukutwa na tani themanini na nne nukta tatu za pembejeo ya unga aina ya Salfa, pamoja na dawa ya maji pisi miambili na tisini na mbili zikiwa zimeisha muda wake, ambapo kiwango kikubwa cha dawa hizo zinatumika kupambana na magonjwa yanayo sumbua mikorosho.

Dawa hizo zilikamatwa katika wilaya ya Tandaimba na Mtwara.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bregedia General Marco Gaguti, amesema pembejeo hizo zimekamatwa katika baadhi ya maduka yanayouza pembejeo.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Mark Njera amesema zoezi hilo limefanyika kwa muda wa siku mbili katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom