Watu 10 wauawa kwenye vita vya jogoo nchini Mexico

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Takribani watu 10 wamepigwa risasi na kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu Jogoo yupi aliyeibuka mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico. Miongoni mwa wale waliouawa ni ni mvulana mwenye umri wa miaka 12 aliyepigwa risasi katika mji wa Cuajinicuilapa.Watu wengine 7 walijeruhiwa vibaya.

Uchunguzi wa awali uliashria kuwa mashabiki wa jogoo hizo mbili walitofautiana kuhusu ni yupi aliyeibuka mshindi.Hata hivyo duru zinasema kuwa huenda ukumbi huo wa mapigano ya majimbi ulivamiwa na watu walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Hadi kufikia sasa,haijulikani iwapo magenge yanayoshamiri mjini Guerrero ndiyo yaliyotekeleza mauaji hayo ya kinyama.Mwaka uliopita wanafunzi 43 walitoweka katika mji wa Iguala na kuweka tatizo la magenge katika majimbo ya Mexico katika rubaa za kimataifa.

Chanzo: BBC
 
Hao majogoo watakuwa wanahusisha kwenye uchezaji WA kamari. Kwa hiyo mtu kalewa hapo ndio sababisho la hilo zogo!
 
Hao itabidi tuwapelekee Majogoo yetu wa uswahilini sababu hawa huwa hawacheleweshi kupata ushindi ulio clear kabisa,jogoo lao litapigwa mpaka litoe damu kudadeki.
Unaenda kupiganisha na jogoo amepigishwa cocaine na kitu cha arusha
5989359-Cock_Fight-0.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom