Watu 10 wauawa kwenye vita vya jogoo nchini Mexico

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
5,963
Points
2,000

kidadari

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
5,963 2,000
Takribani watu 10 wamepigwa risasi na kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu Jogoo yupi aliyeibuka mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico. Miongoni mwa wale waliouawa ni ni mvulana mwenye umri wa miaka 12 aliyepigwa risasi katika mji wa Cuajinicuilapa.Watu wengine 7 walijeruhiwa vibaya.

Uchunguzi wa awali uliashria kuwa mashabiki wa jogoo hizo mbili walitofautiana kuhusu ni yupi aliyeibuka mshindi.Hata hivyo duru zinasema kuwa huenda ukumbi huo wa mapigano ya majimbi ulivamiwa na watu walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Hadi kufikia sasa,haijulikani iwapo magenge yanayoshamiri mjini Guerrero ndiyo yaliyotekeleza mauaji hayo ya kinyama.Mwaka uliopita wanafunzi 43 walitoweka katika mji wa Iguala na kuweka tatizo la magenge katika majimbo ya Mexico katika rubaa za kimataifa.

Chanzo: BBC
 

Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
5,584
Points
2,000

Jackal

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2012
5,584 2,000
Hao majogoo watakuwa wanahusisha kwenye uchezaji WA kamari. Kwa hiyo mtu kalewa hapo ndio sababisho la hilo zogo!
 

Forum statistics

Threads 1,390,952
Members 528,319
Posts 34,067,773
Top