Watu 10 muhimu waliomuweka Magufuli Ikulu 2015

mtoa post aliekutuma mwambie hujatukuta.

usilete habari zilizopitwa na wakati.

JPM ndio Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu.

kama mnaumia roho bado MTAPATA TABU SANA,akimaliza 2025 tunamuongezea.
 
Huyu rais yuko ikulu kwa njia haramu kuanzia kwenye mchakato wa kuchagua mgombea urais ndani ya chama ulikuwa haramu, tume ya uchaguzi nayo ikamhalalisha kwa njia haramu, polisi nao walifanya kazi yao kubwa sana kuhakikisha haramu inakuwa halali
bora kuliko FISADI PAPA lilokuwa na uchu wa madaraka ambalo hadi Mungu mwenyewe ALIKATAA.
 
Acha fix wewe, aliyemweka JPM Ikulu ni Mzee Benja Mkapa..baada ya mgawanyiko mkubwa wa wajumbe wa Mkutano mkuu ambao walikuwa makundi mawili; Kundi la kwanza lenye nguvu ajabu lilikuwa na Mzee Lowassa na lile jingine la Membe!!

Suruhisho likawa wakatwe wote, kisha apatikane mwingine neutral = kura ikamwangukia JPM; yaani embe kwenye mnazi.
 
Mkuu una bonge la akili sana , umeongea ukweli mtupu jamaa alipata nafasi kibahati bahati tu na ugomvi wa tim membe na tim mamvi kugombana so mamvi alivyokatwa tim yake ikaona bora wote wakose kiti apewe jiwe, lakini target kubwa ilikuwa kwa membe, sasa wote wanajuta sasa hivi

Hahaha,,kina MEMBE hawawezi kujuta mkuu,kwani ngosha pia si CCM mwenzao,, ila
mkwere mwenzangu kimoyomoyo anajuta kwann alimbania swahiba wake mamvi,,, maana ngosha anatunyoosha aswaa,,, achagui mkwere wala mzaramo ye analalanao mbele ,, Miaka saba iliyobakia,,ni kama imebakia karne moja hakyamungu😀😀😀
 
Kwanza naanza kwa kusema rais magufuli unakosea sana kwa kusema kwamba ikulu umeitafta mwenyewe, sentensi hii inawaumiza sana watu waliopigana kufa na kupona,

Kuna watu muhimu ambao bila wao leo hii usingekuwa rais tuwe wakweli, wako katika rika mara mbili, kuna wazee na vijana,

WAZEE WALIOSABABISHA UWE IKULU:

1. Mzee Benjamin Mkapa,
Huyu alianza kukupigania tokea mwaka 2013, akawa anashinikiza baadhi ya mambo nadhani Mangula angekuwa anapita hapa angejua na kukumbuka.

2. Jakaya Kikwete, alihakikisha majina aliyopewa na Mkapa, Karume, Kinana na Mangula, Msuya, na Msekwa ndo hayo hayo anayapeleka Kamati Kuu.

3. Mzee Lubuva, huyu alikuwa mjanja sana, angeyumbishwa usingeupata urais, maana kuna muda vijana waliokuwa pale hoteli wanapika matokeo, walimchanganya ikabidi achukue hatua stahiki.

4. Dr. Wilibrod Slaa, Hotuba yake ya pale Serena Hotel ilikuwa ni credit kwako, ilisababisha watu wakate tamaa na Lowassa, usiibeze ile hotuba hata kidogo.

5. Frederick Sumaye, wengi watashangaa kumtaja huyu ila kazi yake aliifanya vema sana na habari na mipango mingi vya UKAWA ikijulikana mapema sana.

VIJANA:

6. Nape Nnauye, hata kama sasa hamko vema kimahusiano lakini mchango wake ni mkubwa mno sana sana, kuna mbinu nyingine zilitumika sana tunazijua.

7. January Makamba, huyu alihakikisha masuala ya Cyber anayamudu, tuwe wakweli - naye ana mchango mkubwa sana watu hawajui hili.

8. Mwigulu Nchemba, Wanamuita Madelu, huyu kijana amepigana kwa hali na mali mpaka nakumbuka baadhi ya vikao muhimu vya siri. Sitasahau!

9. Humphrey Polepole, huyu alileta maelezo juu ya tuhuma zako pale Channel Ten na kuwaaminisha watanzania juu ya asemalo, hasa kwenye MV Bagamoyo na utaratibu wa kuiongezea speed ndo maana ikapelekwa jeshini.

10. Dr. Hamis Kigwangala, namkumbuka sana kule Kigamboni kwenye mipango yetu maalumu hasa kwenye suala la kudhibiti mambo fulani fulani.
umesahau MAMA JENI
 
Siku alipotangazwa Magufuli kuwa ndiye mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM ndiyo siku niliyojua kura yangu tarehe October 25 2015 itaenda kwa nani! Ama hakika sikuitaji kusikia kampeni wala nyimbo za mtu nilikuwa nisha muona nani wakumpa tiki.
 
Siku alipotangazwa Magufuli kuwa ndiye mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM ndiyo siku niliyojua kura yangu tarehe October 25 2015 itaenda kwa nani! Ama hakika sikuitaji kusikia kampeni wala nyimbo za mtu nilikuwa nisha muona nani wakumpa tiki.
Ulimpa nani
 
Kwa Nape na January Makamba upo sawa kwenye kampeni na wakati wa tukio lenyewe la uchaguzi nikwei walifaiti,ila ndani ya chama sio wao waliokuwa sababu ya NGOSHA kuteuliwa na chama,,

Magufuli alipata nafasi ya kusimamishwa na chama kugombea nafasi ya urais kwa nguvu za Mungu kaka, hakuna hata mmoja aliempigania ndani ya chama, wala hakuna ambaye alitegemea wala kuwa na muda wa kujipendekeza kwa Ngosha kwa kujua labda chama kitamsimamisha. Wengi waliwekeza nguvu zao za fedha na kila namna ya kampeni kwa Lowassa na Membe,,,

Kwa Lowassa waliwekeza nguvu sababu ndani ya CCM alikubalika hakuna mfano,, kwahiyo walijua kwa 100% ni Rais ajaye kwa maana atawakumbuka katika teuzi na kuwalinda kama ilivyo desturi kwa Africa wengi hujipendekeza kwa mtu mwenye muelekeo wa kushika madaraka kwa masilai ya biashara zao au kukumbukwa katika teuzi.

Na kwa Membe watu wengi walitegemea lazima chama kitamsimamisha kwa kuwa Rais aliekuwa anamaliza muda wake ndio ilikuwa chaguo lake Membe kwa 100%,,

Sasa bwana kwa nguvu za mwenyekiti aliekuwa anamaliza muda wake,,Lowasa akakatwa ili Membe iwe simple kupitishwa,, kwaiyo ndani ya ccm asilimia tisini walikuwa wanampenda na kumuitaji Lowasa,, sasa wakasema ngojea tumkomeshe Mkwere, wakamchagua mtu ambae wala hakuwa kwenye hesabu zao ili wakose wote, wakampa kura magufuri, wakamtupilia mbali Membe. Kwahiyo aliemnyima urais Lowasa ni swahiba wake Mkwere,,,kama kikwete angehamua kumpigania Rafiki yake Lowasa, na kwa namna alivyokuwa anapendwa ndani ya chama,, saizi angekuwa Rais,,

Kwahiyo siku zote ugomvi wa panzi furaha ya kunguru,, mtifuano wa kambi ya kikwete kumtaka Membe, na wanachama ndani ya ccm kumtaka Lowassa,, mtani wangu Ngosha akaokota embe dodo chini ya mti wa muharobaini kiulaini,,

Kwahiyo mzee baba Magufuri hakuna wakujivuna kuwa yeye ndio chanzo cha Ngosha kuwa Rais,, si kwa pesa za matajiri wala ndani ya chama,,, ni Mungi tu umpa madaraka amtakae,, na huyu Ngosha ni Mungu ndio alishampangia awe Rais,, kwa wasiompenda Magufuri,, me kwa upeo wangu wa kingumbaru nadhani wakulaumiwa labda Mkwere ndio chanzo,
Uchambuzi wako umeufanya kwa kuangalia cover la kitabu jinsi linavyoonekana kwa nje, na kila mtu asiyejua ndani ya kitabu kuna nini atafikiri kama unavyofikiri wewe..

Unajua kwa nini alirudishwa wizara ya ujenzi kutoka wizara na maji aliyokuwepo, na baada ya kurudi akaanza kuzindua madaraja na Barabara.

Unajua kuwa baada ya kurudishwa wizara ya ujenzi alianza kupewa ulinzi.

Hamnaga kitu cha bahati mkuu hasa linapokua suala la kiongozi wa nchi.
 
IMG-20181022-WA0001.jpg
 
Ulimpa nani
Kama una kumbukumbu mzuri CCM ndiyo walikuwa wa kwanza kumtangaza mgombea wao hivyo sitarajii kuwa unahisi nilimpa mtu asiye fahamika! maana nmesema baada ya kutangazwa JPM tu tayari nilikuwa na maamuzi ya kura yangu. hivyi ni JPM na 2020 ni yeye tena sihiitaji ngonjera ata mashairi ya mtu.
 
Back
Top Bottom