Watoto wetu wanavyopambana na kifo wakienda/kutoka shule | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wetu wanavyopambana na kifo wakienda/kutoka shule

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by JohnShao, Apr 15, 2011.

 1. J

  JohnShao Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Picture From: "Tanzania Daima" April 15, 2011, Page 1

  View attachment Wanafunzi wakivuka barabara.pdf

  Jamani, watoto wetu wana-risk kifo kila siku wakivuka barabara hadi wanashikana mikono ili kupambana na kifo au kama ni kufa wafe pamoja. Inasikitisha mno!

  Walio na wajibu wa kuhakikishia watoto wetu usalama ni Serikali, Wazazi na Walimu, na ni wazi kuwa tumeshindwa hili jukumu la msingi na kwaachia watoto wetu wajihami wenyewe. Aibu kubwa!

  Changia maoni yako please...
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Innocent Kids!
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...huyo aliyeziba masikio, atawezaje kuisikia honi?
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,864
  Trophy Points: 280
  pale karume hakuna tuta? au zebra
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Pamoja na kuwa sisi kama wazazi tunalo jukumu la kuhakikisha usalama wa watoto pia wazazi majukumu mengine. Ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba watoto hawa wanapata chakula, mavazi na malazi. Katika majukumu haya serikali inachukua kodi kubwa sana huku ikitudanganya kwamba itaajiri polisi watakaosaidia ulinzi wa watoto, itajenga barabara nzuri zitakazowezesha watoto wetu kupita kwa usalama, pia kwa fedha za kodi hizo watajenga shule nyingi na hivyo watoto wetu hawatukuwa na haja ya kutembea umbali mrefu kwenda shule. Ni kwa sababu ya kodi kubwa tunashindwa kuhakikisha usalama wa watoto wetu kwani kufanya hivyo tutakosa vibaru vyetu au kwa kufukuzwa kazi au kukosa wateja. Zaidi sana mishahara tunayolipwa haitoshelezi hivyo inatupasa kufanya kazi kwa mda mrefu sana ili kuweza kuwapatia waototo wetu mahitaji yao.
  Kwa sababu hizi na nyingine nyingi serikali inajiweka katika nafasi ya kutatua matatizo ya wananchi, lakini ndo kwanza ufisadi kila mahali. Kila kona ubadhirifu unafanyika. Hii ndiyo sababu mtoto akigongwa na gari leo tunaomboleza na baada ya siku mbili tunaendelea kuchachariki kwani kutokufanya hivyo kutatufanye tufe kwa afa jingine la njaa.
  Hivyo ni wakati mwafaka sasa serikali itumie fedha za kodi zetu kwa mipango kusudiwa na si kuachia fedha zetu ziishie mikononi mwa mafaisa na wabadhirifu. Kwani ipo siku kwa hakika tutachoshwa na hali hii. Akifa mtoto barabarani serikali isidhani baada ya kumzika basi mambo ndo yamekwisha. Familia inaingia katika simanzi kubwa sana, na hii inatengeneza uhasama mkubwa sana kati ya watu an serikali.
   
 6. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Inauma sana kuona watoto wanapata shida namna hii.
   
Loading...