Watoto wetu wa Siku hizi 'mnapotupiga' Wazazi wenu Pesa kwa 'Kutudanganya' msidhani huwa hatujui ila tunakausha kwakuwa nasi 'tuliwapiga' Babu zenu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,528
Na kama tukiamua 'Kuwakazia' tutaishia Kuwachapeni sana 'Bakora' na huenda hata hizi Pesa zenyewe tusiwe tunawapeni vile vile na hakuna cha Kutufanya.

Haiingii Akilini Mtoto umeenda Kumtembelea Wiki Mbili tu zimepita Leo hii anakupigia Simu na Kukuambia sijui kaishiwa Vitabu mara sijui kaibiwa Begi na Viatu na hapo hapo tena anakuunganishia kuwa wana Ziara ya nje ya Mkoa halafu ukimuomba namba ya Simu ya Mhusika hapo Shuleni anakuambia kuwa kwa sasa hana Simu aliibiwa na Vibaka.

Kwahiyo Watoto wa Siku hizi mnavyotudanganya Wazazi wenu na 'Kutupiga' kwa Kutudanganya katika Mahitaji yenu ya Pesa huwa mnatuona bonge la Washamba na Malofa fulani na kwamba huwa hatuwashtukieni?

Tunajua kila Kitu, ila tunawakausha tu.
 
Mkiwa mmebeba mimba muwe mnakemea na hizo roho ZA udanganyifu kutoka Kwa viumbe mlio wabeba tumboni.

Ona Sasa Mtoto umembeba mwenyewe tumboni Kwa miezi Tisa halafu leo anakuona we mshamba ... Pole Sana mkuu..ukibeba ujauzito mwingine mkuu kumbuka kusali Sana.
 
Kweli mkuu mzee yule nikimkumbuka naishia kucheka tu, ila kibomu hadi cha kupoteza fyekeo aisee mimi nilizidi😂
Mkuu nisamehe unazitesa mbavu zangu kwa Kucheka. Una Vituko sana.

Toto langu limenidanganya Mchana huu huu halafu nimekagua Simu yake kumbe Hela yote niliyompa kamtumia Demu wake.

Hasira zilinipanda ila nikaishia tu Kupoa na kuanza Kucheka kwani Kudadadeki zake 'Junior' wangu anapita mule mule kwa Mimi Baba yake hivyo nikitaka Kumchapa / Kumpiga nafsi inanisuta na nakubaliana tu na hali.
 
Halafu Wenyewe wanavyotudanganyaga hujiona 'Geniuses' kweli kweli wakati Sisi Wazazi / Walezi wao ndiyo tuliwa 'Wapigaji' na 'Masela' zaidi yao kwa Babu zao.
Umeambiwa ukibeba mimba nyingine, uwe unaifanyia maombi ili kiumbe atakayezaliwa hasiwe tapeli kama wewe mzaziwe.
 
Nasubiri vibomu vya watoto wangu.m😂😂ila hawataniongopea ..nikikumbuka nilikuwa namuombaga Baba pesa ya project na field dah
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom