Watoto wetu kwanini hivi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wetu kwanini hivi??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sizinga, Jun 22, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Ni juzi tu tumesherehekea mtoto wa Afrika/fahari ya Afrika kwa generation ijayo, lakini mbona imekuwa hivi siku hizi za usoni??kwanini hasa??je ni kweli wa kulaumiwa ni wazazi??walimu??,walezi??au majirani??napata ugumu sana.
  Hakuna tena tunachojivunia kupitia kwa watoto wetu, ikiwa ratio yake ni 1:100..hii ni mbaya sana.


  Maadili ya watoto wengi wa siku hizi yameshuka mno,mitoto mingi ni mitukutu, wagomvi, wavivu,
  watundu, waoga, sio creative, wala sio constructive kabisa!! au ndio shule za kata, lakini mbona zimeanza karibuni tu??sidhani...hii dalili au tabia nyingi za watoto zimeanzia majumbani tunakoishi nao. Hembu nikupe homework kidogo!! Ikifika mida ya mchana watoto(wa shule za msingi au sekondari) wanapokuwa group kurudi nyumbani jaribu kukaa nyuma yao na sikiliza kwa makini wanayoyaongea, then njoo hapa jamvini na jibu.


  Ni upuuzi mtupu wanaooongea!! Tofauti kabisa na zamani, utakuta watoto wanadiscuss magazijuto, wanazungumzia kani mwendo, respiresheni, milinganyo na kadhalika. Leo hii utawasikia, mara kule mdundiko, huku kiduku, mara Kanumba kafanyaje sijui, mara hili mara lile..hovyohovyo!!


  Sasa ngoja nikupe kitu cha kusikitisha kabisa hapa mtaani kwangu Mabibo...kuna mtoto(wa kiume) anasoma darasa la pili, juzi maza angu mdogo katujuza kwamba anawabaka watoto wenzake!! can u imagine this???mpaka sasahivi keshawatenda watoto wenzake wawili. Wa kwanza anakaa nae nyumba moja na ni wakiume, wa pili ni wa kike wa nyumba jirani. Wazazi wote wako macho sasa hivi kuhusu huyu firauni mtoto. Pale Luanga anti yangu kawakuta watoto 2 wanabakana(hawa ni chini ya miaka 10), kawafungia mlango wako uchi kamsubiri mama yao alivyokuja kawaambia angalia kinachoendelea ndani/hakuamini, kanalamba fimbo sana wale watoto.


  Sasa ukiangalia hizi stori fupi unaweza jiuliza maadili yepi ya kujivunia toka kwa watoto wetu??
  Ukiwapa homework ni utumbo mtupu wanafanya, sasa sijui nani alaumiwe. Kinachoumiza zaidi ni kwamba hakuna mwelekeo wowote wa mabadiliko ya ghafla au ya muda mrefu kwa hawa watoto.
  Eeh Tanzania yetu nani katuloga lakini??mtoto anangalia muvi ya Kaumba au John Sina, nae anachukua kisu anamtishia mzazi au anaruka kwa ajabu sana..eeh??hivi mnajua kwanini muvi za kina Rambo na za vita zilikosa mvuto kipindi flani hadi leo??wazungu waliacha kupractice na kuonyesha in public coz ziliharibu sana watoto. Sameway kwenye games vivyohivyo.


  Jamani tujitahidi kuwarekebisha watoto wetu. Hali si shwari kabisa tukiendelea na mwendo huu. Baba yuko bize kuhangaikia mkate na huku nyuma mitoto iko bize na filamu na mambo ya ajabuajabu. Tutafika tu!!


  Siku njema!!
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  My dear
  Story za bibi na babu zimetupiliwa mbali
  Sasa ni TV, Video games, Xbox, PlayStation,
  NINTINDO , WII, sing star, etc

  Na mie sintokaa hapa ni mlaumu yeyote
  Bali ni jamii kwa ujumla.. kwani mtoto awezakuwa na maadili yote nyumbani kwa kuogopa wazazi lakini atokapo mlangoni ni story nyingine..

  Kipindi mi niko shule ya msingi mtu akituona
  Tunapigana barabarani baada ya shule anatukamata na kutufinya halafu tunakimbia
  Nyumbani ukifika husemi kitu ng'oooo..
  Sasa hivi we mguse mtoto wa mtu
  Utaeleza kama ulimsaidia kusukuma .

  Enzi za bibi na babu zimeondoka
  Za.mama na baba zimepita, zetu
  Zimeisha za wenetu zinatisha za wajukuu
  Na vitukuu naogopa kuvifikiria ...

  Technology na media vinachangia
  kuwakiza wenetu haraka kupita kiasi
  ..
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  mtoto anawabaka wenzake; kosa la wazazi, je wanalala na mtoto? kuna jirani zangu walipata aibu baada ya kitoto cha kiume kidogo kuwambia kitoto kidogo cha kike wafanye kama baba yake na mama yake, then akiwa na majirani anawasimulia na kuwaonyesha wazazi wake wanavyofanya!!!

  pili wazazi wa siku hizi ukimkanya mwanae atakuja kukusema na ugomvi juu, wakati enzi zetu tunakua hata jirani akikuona barabarani unafanya ujinga la atakuburuza mpaka kwenu kukusemea , kisha upate stiki za nguvu, kosa likiwa kubwa hadi shule mzazi atakuja upigwe mstarini, hapo mtoto utanyooka tu, sasa siku hizi gusa mtoto wa mtu ukome, utajuuuuuuuuuuta kumfahamu!!!!!!!!!!

  tatu siku hizi hakuna malezi bora wala ukaribu kati ya mzazi na mtoto, watoto wanapelekwa boarding toka wadogo hapo unategemea nini? Au maendeleo ya mtoto shuleni housegirl ndo anafatilia kama mtoto kaenda shule au la, kufuata ripoti na kadhalika, malezi ya watoto wetu tumeyakabidhi kwa housegirl, mbaya zaidi ukute housegirl ni mtoto, hapo inakua mtoto anamlea mtoto mwenzake

  na mengineyo meeeeeeeeeeengi ambayo wazazi tumeyachangia. mzazi unamuacha mwanao full time kwenye tv na internet hujui anaangalia nini anajifunza nini, mzazi humkanyi mwanao au hauwi karibu na mtoto mpaka unakuja kushtukia tayari too late...
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kuna thread kama hii tuliwahi kuijadili nani alaumiwe pale mtoto anapokosa maadili. Nafikiri ni jamii kiujumla, mtoto anaweza kuwa na muda mdogo sana wa kuwa karibu na wazazi wake ukilinganisha na jamii inayomzunguka, maisha anayoishi akiwa ndani yanaweza kuwa tofauti na maisha anayoishi nje. Inaweza kuwa ngumu kwa mzazi kupata matukio maovu ya mwanae. Kama ambavyo mtoa mada umesema huyo mtoto amebaka watoto wawili, wewe na aunt yako mnajua ila mlifanya nini kumsaidia yule mtoto?
  Inabidi tuache kasumba ya kumuona mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio au kumuona kama vile hakuhusu.
   
 5. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Njia pekee ya kuwanusuru watoto wetu ni kuwaonyesha milango ya Madhabahu ilipo. Malezi ya watoto imekuwa ihu ngumu kwa sababu ya hali halisi ya kimaisha.
  Ukimkataza wa kwako kufanya jambo fulani, wa mwenzio anafanya kwa kiwango kisichovumilika, matokeo yake hata wa kwako hataiga. Lakini watoto tukiwajengea mazingira ya kumjua Mungu ndo itakuwa suluhisho kwao. AMINA
   
 6. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kiukweli maadil ya mtoto yamepotea kabisa, na hili linatokana na jamii inayomzunguka na maendeleo ya sayansi na technolojia,
  kama ukifuatilia vipind vinavyoangaliwa na kusikilizwa na watoto siku iz vinawakomaza watoto, wazazi wako bize watoto wanajiendeshea maisha
  kivyao mzazi hajui maendeleo ya mtoto.
   
 7. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mtoto hazaliwi na tabia ..kama sio wewe umefundisha ni ndugu yako..kama sio ndugu yako ni jirani yako..kama sio jirani yako ni jamii yako.. Tusilaumu mabadiliko ya teknolojia tujilaumu sisi wenyewe..Toka asubuhi unambwaga mtoto shule..unaonana nae kesho..baba anaenda kazini akitoka anapitia kuangalia Manchester united na Liverpool... Mama anaenda kazini wakati anarudi ana-appointment kibao za vyama na vi-kitchen party.. watoto wanabaki na kina dada - house girls ambao kutokana na elimu ndogo wanashinda kuangalia kina Komedi.. na mzunguko huu wa maisha ni mwaka mzima..halafu tunalamu mambo mengine..tatizo ni sisi wenyewe..
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Siongezei kitu, kesho nikitoka job naacha gari, nachukua daladala naenda kuwavizia wale watoto wa shule moja hivi . . .
  Naahidi kuleta uvumbuzi mwingine kama utakuwa tofauti na huu
  Shukrani Sizinga Master
  Umekamilisha My day
   
 9. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Zamani mtoto/watoto walikuwa wa jamii nzima,
  lakin siku hizi watoto/mtoto ni wa wazazi wake tu,

  pia na sisi wazazi wenyewe tumepungukiwa sana na tabia njema,
  tunasahau kuwa mwalimu wa kwanza wa mtoto/watoto ni wazazi wake,
  na wengine wanafuata, pia wazazi wa siku hizi tupo busy kupita kiasi,
  kiasi ambacho hatuna muda wa kuzungumza/kuwafundisha,kuwaeleza,kuwatahadharisha,
  watoto wetu kilichopo,kinachoendelea katika maisha yetu ya kila siku.
  Mtoto anapokosa mwongozo toka kwa wazazi wake, basi kila akionacho anacopy na kupaste,
  katika mazingira yoyote ayapendayo yeye.

  Kuharibikiwa kwa watoto ni tatizo la wazazi pamoja na jamii nzima.
  Pamoja na hayo hatupaswi kukata tamaa ya kuwalea wanetu, ni lazima,
  tujitahidi kadri ya uwezo wetu kuwafundisha,kuwaelimisha,kuwaonya,kuwasikiliza,
  bila kusahau kumshirikisha mungu wetu kwa kila jambo katika maisha yetu ya kila siku.
   
 10. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa ufuatiliaji mdogo tu nilioufanya,
  watoto wengi wa siku hizi wakike kwa wakiume wakitoka shule wanaongelea,
  yafuatayo

  big brother, mpira hasa time za nje, tamthiliya za kwenye tv, movie,
  mambo ya kuchat kwenye internet, facebook,twitter. Mambo ya vijana na burudani vinavyoendelea,
  kwenye tv. Mambo ya b/g friend. Fiesta.............
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mkuu hivi unaongelea tanzania ya leo ama??hembu jaribu kumkaripia au kumuonya mtoto wa jirai yako uone utakavyorushiwa maneno ya kejeli na matusi...acha bana!! siku moja baba mmoja kamuonya mtoto akiyechezea pikipiki i;iyokaa vibaya coz ingeweza kumwangukia na kumvunja miguu...toto limeenda home linalia, yule mama kaja kwa jazba na mitusi juujuu...hahaaa!!
   
 12. CPU

  CPU JF Gold Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Am back now . . . .
   
 13. CPU

  CPU JF Gold Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Deleted . . . .
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa kwanini hukuweka muongozo kwenye thread husika?!

  Hahhahah baada ya kuangalia video nakwambia acha uzushi.Hii video nineonyeshwa kwenye net nadhani ilikua wikiiliyopita nikataka kuiweka JF but i never got to it.

  Nwy maoni yangu kwenye hiyo video ‘japo sio wewe uliyeirecord‘ ni kwamba watu wazima wanachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa wanavyokua.Hapo kwenye video watu wazima kibao wanashangilia na kufurahia kinachoendelea. Hata kama sio wazazi/na walezi wa wahusika bado watoto wanakua influenced na attitude ya hiyo audiance...sasa watoto kama hao wataachaje kufanya vitu ambavyo wanaobyeshwa vina ‘mshiko‘?!Sio rahisi....
   
 15. CPU

  CPU JF Gold Member

  #15
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Noted and thanked
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...la kujilaumu ni sie wazazi tunavyochangia kwa kiwango kikubwa kuwaharibu watoto.
  Kama sisi tulilelewa kwenye maadili mema, kwanini sisi tumeshindwa kupandikiza vichwani mwa
  hao watoto yale yaliyo mema?

  Kwa tahadhari, na wasaa wako soma link hii; MCHUMBA WA MTU AVUA NGUO HADHARANI! - Global Publishers ....Tujilaumu wenyewe kwa mmomonyoko huu wa maadili, Period.
   
 17. charger

  charger JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  CPU procesor nzima kweli?
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Hakuna kuku anaetaga yai viza!!
   
Loading...