Watoto wengi wanaosoma shule zenye mtaala wa Kiiengereza wanaongea Kiingereza kibovu! Wazazi wabaneni Wamiliki wa shule

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,544
15,215
Mtaa mmoja Kila siku yamapita magari zaidi ya kumi kushusha watoto. Yaani vile watoto wanaongea 'broken' ni balaa.

Utasikia.....

'' Me is going hooome...''
'' Me is need to pass ''
'' me is my friend is to go homeeeee''

Hii inaniuma maana mtoto akienda english medium lengo kuu ngeli kwanza mengine mbwembwe.

Nasikitika sana kama hili lisipofanikiwa. Wazazi muwafanyie usahili watoto wenu kama wanaongea makorokocho mkawapige mikwara walimu hao au wakuu wa shule.
 
Mkuu kama mtoto ni mdogo std 3 au 4, basi hiyo ni broken, ila from std 5 to std 7 vinatumia slang wananesa ki America utakuta anasema "me going home" badala ya "i am going home" mara uulize ktu kaseme "IMO" instead of in my opinion basi vita tu.... Tunaoumia ni sisi wazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jirani yangu ni mke wa kibosile, watoto wanasoma English medium, kule shule wameambiwa wazazi pia waongee na watoto kizungu. Alikuja shost amevimba, sasa tunawapa mahela yote bado wanatusumbua sisi wazazi😂.
Hahahah ndio ilivyo hata huku kitaa kwetu,..wazazi ngeli haipandi basi watoto wakirudi utawasikia wanasema "eeeh washarudi wazungu,tutakoma mwee"😂
 
Nafikiri wengi ya wanaongea broken ni wa level ya chini yaani nursery, std 1,2 kwa maana ndio wanaanza kujifunza lugha ya kigeni yaani wanaupungufu wa maneno ya english vichwani mwao maana familia nyingi hatuongei na hatujui english.

Mtoto au hata mtu mzima anapoanza kujifunza kuongea lugha ya kiswahili haundi sentensi kama vile anavyounda anayejua kuongea vizuri kiswahili, kwa hiyo watoto nafikiri wanaweza kubadilika kutoka kwenye broken kadri muda unavyoenda.
 
Wazazi wenyewe(wengine) broken...😊
mkuu inabidi wajiongeze watafute hata wakina Prof Las Simba wawafanyie interview watoto wao ili waone kama matarajio na kinachoendelea vinaendana? Maana Jana nilikiwa kwenye shule moja English Medium Ni Boarding, Bwalo wanalolia ubwabwa chafu balaa, nikajiuliza kwa huu ucareless hawa watoto ngeli watakuwa wanaelewa kweli?
 
sasa si ndio vimeanza anza mkuu,subiri hata vifike std 5
mle huwa viko mchanganyiko huwezi kujua yupi ni yupi, ila ni vizuri wazazi kucheki performance za uwezo wao kuonhea kiingereza kwa viwango vya dunia sio kutoa pesa na kuishia tu.
 
Sasa kama mimi mwenyewe ki-inglish sijui. Ntamsaili mtoto vp
mtest kwa wanaojua ili wakuambie kama unaliwa pesa au dogo yuko kwenye raititraki.
Lengo kuu la English medium ni dogo kujua fasaha Lugha hii pendwa duniani, mengine ni mbwembwe tu
 
Mkuu kama mtoto ni mdogo std 3 au 4, basi hiyo ni broken, ila from std 5 to std 7 vinatumia slang wananesa ki America utakuta anasema "me going home" badala ya "i am going home" mara uulize ktu kaseme "IMO" instead of in my opinion basi vita tu.... Tunaoumia ni sisi wazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
hivyo navyo sumbufu balaa. sasa wewe hata Thelesa May haongei huo uuni wao wanataka tena kuongea viingereza vya mateja wa london. Hii tabu hii mkuu. Hapo napo wazazi watakuwa wanapoteza ngawila.
 
Wakiajiri waalimu wageni mnalalamika,wakaijiri wazawa mnalalamika aiseeee
wale wengi walikuwa wanafundisha english za kijaruo.
mfano
how arrrrrrrrre you. Watoto wanatakiwa kuongea english standard sio english za kilugha.
 
Back
Top Bottom