Watoto wawili wameokolewa kwenye kifusicha jengo la ghorofa saba lililotitia

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000
Watoto wawili wameokolewa kutoka katika kifusi cha jengo lililotitia la ghorofa saba, ikiwa ni takribani saa 24 baada ya tukio huko Nairobi, Kenya.

Taarifa rasmi ya waokoaji imesema waliokolewa ni mtoto wa kiume na kike ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu hospitali.

Mwanamke ambaye naye aliokolewa akiwa mzima kutoka kwenye mabaki ya jengo hilo huko kusini mwa mashariki Kware eneo la bomba la mafuta Ebakasi alifariki baadaye.

Shirika la Msalaba mwekundu la Kenya, limesema mtu mmoja pia alifariki dunia kufuatia kutitia kwa jengo hilo Jumatatu usiku. Watu kadhaa wameripotiwa kutoonekana katika ajali hiyo.

Operesheni ya kuwasaka na uokoaji wahanga inaendelea katika eneo hilo.

upload_2017-6-14_11-7-28.jpeg


Chanzo: Azam News
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom