Watoto Wawili Mapacha wamefariki Dunia wakati Mama yao akiwa busy live Facebook

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,603
20,064
Mapacha.JPG

Watoto wawili mapacha wamefariki dunia baada ya kuporomoka kutoka ghorofa ya kumi wakati mama yao akijivinjari LIVE katika mtandao wa facebook.

Mapacha hao Moise Petrice wa kiume na Beatrice Petrice pacha wa kike wamekumbwa na umauti huo baada ya kudandia katika dirisha lililokuwa wazi. Tukio hilo limetokea katika jiji la Ploiesti nchini Romania.

Polisi wanasema mama wa watoto hao hakugundua kama wanae wameporomoka na kufariki dunia hadi hapo aliposikia milio ya magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) huku kukiwa na mtu akibisha hodi mlangoni kwake.

Muda wote huo alikuwa LIVE facebook akiongea na wafuasi wanaomfuatilia katika ukurasa wake wa mtandao huo.

Imeelezwa kuwa wakati mama huyo Andreea Violeta Petrice alisahau kufunga dirisha ambalo watoto hao walilitumia kucheza kwa kujaribu kutoka na ndipo walipododondoka na kupoteza maisha.

Baada ya kumfungulia mlango mtu ailyekuwa anabisha hodi alimtaarifu kuwa kulikuwa na watoto mapacha wamedondoka na kufariki.

Mama huyo kwa haraka alikwenda chumbani kwa watoto wake ili kujua kama ni wake na ndipo alipogundua kuwa hawakuwa ndani na dirisha lilikuwa wazi.
 
Kuna mmoja alikua anaandaa maji ya mtoto ya kuoga kwenye bath tab. Ameanza na maji ya moto ili apozee na ya baridi. Wakati maji ya moto yanatoka shost alipiga simu wakaanza kupeana up-to-dates za gossip za mjini.

Mtoto alipokosa attention ya mama muda mrefu alikwenda bafuni, tab karibia ijae maji ya moto, mtoto aka ingia. Mama amestushwa na kelele za maumivu. Amefika mtoto ameungua mwili mzima.
 
Back
Top Bottom