Watoto watatu wafa maji baharini Zanzibar

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,396
Watoto watatu wamefariki dunia baada ya kuzama baharini eneo la Muungoni mkoani Kusini Unguja.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kheri Mussa Haji aliwataja watoto hao kuwa ni Issa Kombo Hassan (11), Abrahman Zahran Ali (7) na Omar Aboud (10) wote wakazi wa Muungoni.

Kamanda Haji alisema jana kuwa uchunguzi uliofanywa umebaini vifo vya watoto hao vimetokana na kunywa maji mengi.

Akizungumza kwa niaba ya familia za watoto hao, Sheha wa Muungoni, Shafii Hassan alisema watoto hao walikuwa wakicheza ufukweni mwa Bahari ya Hindi na kuingie kwenye dau (jahazi dogo) lililokuwa limetia nanga eneo.

Shafii alisema baada ya muda kupita ndipo watu walianza kuulizana ni wapi walipokwenda watoto hao na hawakupata jibu.

Alisema msako wa watoto hao ulianza juzi saa 11:00 jioni hadi saa mbili usiku walipoiona miili hiyo baharini.

Sheha alisema miili ya watoto hao imeshakabidhiwa kwa jamaa zao kwa ajili ya maziko.

- Mwananchi
 
Poleni, ila kinachoua ni maji kujaa mapafuni siyo tumboni. Kwa hiyo msemo wa "kafa kwa kunywa maji" si sahihi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom