Watoto watatu familia moja wafa kwa moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto watatu familia moja wafa kwa moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 21, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Watoto watatu wa familia moja katika Kitongoji cha Ikanamalenge, Kijiji cha Muhanga, Tarafa ya Itigi, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, wamefariki dunia baada ya nyumba walimokuwa wakiishi kuteketea kwa moto.
  Marehemu hao ni Geste Masana (4), Madiwa Masana (3) na Degekali Masana, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Diwani wa Kata ya Ipande, Daniel Manyika na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Celina Kaluba, tukio hilo lilitokea Desemba 15, mwaka huu saa 11:00 jioni.
  Akisimulia mkasa huo wa kusikitisha, Diwani Manyika alisema siku ya tukio mama wa watoto hao aliondoka na kuwaacha nyumbani baada ya kuwaandalia chakula na kwenda kuchota maji huku baba yao, Masana Kidabiti (58), akiwa shambani.
  Alisema baba wa watoto aliporudi nyumbani saa 12:00 jioni, alipigwa butwaa baada ya kushuhudia nyumba yao ya nyasi waliyokuwa wakiishi ikiwa imeteketea yote kwa moto na watoto wake wote wakiwa majivu matupu.
  Diwani alisema muda mfupi baadaye, mkewe naye alirudi nyumbani na kushuhudia kilichotokea.
  Alisema wazazi wakishirikiana na majirani, walijaribu kuwatafuta watoto hao na kugundua majivu yao yakiwa chini ya uvungu wa kitanda.
  "Yawezekana wakati watoto hao wakihangaika kujiokoa na kubaini kuwa mlango umefungwa, waliamua kujificha chini ya uvungu," alisema diwani huyo.
  Alisema taarifa za tukio hilo zilitolewa kwa Mwenyekti wa Kitongoji hicho, Kimenda Matanga, ambaye naye aliwasiliana na Afisa Mtendaji wa Kijiji na kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Muhanga.
  Hata hivyo, baba wa watoto hao, alidai kuwa kabla ya tukio hilo la kusikitisha, aliwahi kutishiwa na mtu ambaye hakumtaja kwamba atamhamisha kijijini hapo.
  Kwa mujibu wa Diwani Manyika, chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
  Kamanda Kaluba alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba hakuna mtu au watu waliokamatwa.
  Katika tukio lingine, daktari mstaafu wa Hospitali ya Mkoa, Phillipo Daniel (68), mkazi wa Machinjioni mjini hapa, amekufa papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki.
  Kamanda Kaluba, alisema daktari huyo mstaafu aligongwa na pikipiki Desemba 15, mwaka huu saa 2:30 usiku eneo la Hospitali ya Mkoa wa Singida barabara ya mtaa wa Bomani, mjini hapa.
  Alisema dereva wa pikipiki ambaye hajafahamika jina wala usajili wa namba ya chombo chake hicho cha usafiri, alikimbia baada ya ajali hiyo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. L

  Lady JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Poleni familia!
   
Loading...