Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Habari wana MMU, Leo naomba tujuzane na kujadili athari ya watoto katika mahusiano baina ya wanandoa. Jambo hili linaweza kudhaniwa kuwa dogo lakini ukweli ni kwamba mahusiano ya wanandoa wapatapo watoto hutetereka kiasi kwamba mahaba ya busu,vicheko,kupapasana, n.k hubakia kuwa historia na kuona runingani. NI KITU GANI KINATOKEA? 1.Mtoto/watoto huingia katika ushindani wa mapenzi na thamani; hapa ndipo Baba hujisikia kutengwa katika familia (Wengine hutafuta nyumba ndogo) kwani Mama huwa karibu sana na mtoto kuliko Mume (Psychological jealous). 2.Mgogoro juu ya namna ya kulea; hutokea pale ambapo mawazo ya wazazi hutofautiana kisha huharibu mahusiano yao. 3.Kelele na ugomvi wa watoto; nyumbani huwa siyo romantic kwa wazazi kufurahishana kimapenzi. Mambo mengine ni gharama za afya,muda na elimu hugeuka mwiba kwa wanandoa ambao hujikuta hawana muda wa kufurahi bali kusaka pesa. Mwana MMU umejipangaje kupambana na changamoto hizi?