Watoto wanaharibu mahusiano ya kimapenzi katika ndoa, umejipanga?

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Habari wana MMU, Leo naomba tujuzane na kujadili athari ya watoto katika mahusiano baina ya wanandoa. Jambo hili linaweza kudhaniwa kuwa dogo lakini ukweli ni kwamba mahusiano ya wanandoa wapatapo watoto hutetereka kiasi kwamba mahaba ya busu,vicheko,kupapasana, n.k hubakia kuwa historia na kuona runingani. NI KITU GANI KINATOKEA? 1.Mtoto/watoto huingia katika ushindani wa mapenzi na thamani; hapa ndipo Baba hujisikia kutengwa katika familia (Wengine hutafuta nyumba ndogo) kwani Mama huwa karibu sana na mtoto kuliko Mume (Psychological jealous). 2.Mgogoro juu ya namna ya kulea; hutokea pale ambapo mawazo ya wazazi hutofautiana kisha huharibu mahusiano yao. 3.Kelele na ugomvi wa watoto; nyumbani huwa siyo romantic kwa wazazi kufurahishana kimapenzi. Mambo mengine ni gharama za afya,muda na elimu hugeuka mwiba kwa wanandoa ambao hujikuta hawana muda wa kufurahi bali kusaka pesa. Mwana MMU umejipangaje kupambana na changamoto hizi?
 
hiyo kweli changamoto, nafikiri watu wasizae mapema kama vipato vyao havipo stable. pia wanandoa kuwa na nafasi ya kujadili mienendo yao inaweza saidia. badala ya kulalamika kwa watu unamuita muhusika na kumueleza ukweli. ubaya ni kwamba wengi hawaambiani ukweli wanaishia kuumia tu moyoni na mwisho wa siku huona solution ni kuwa na mpango wa kando.
 
Husninyo; Ni kweli kabisa, kabla sijafanya uchunguzi nilidhani wasomi na wenye pesa wanaepuka tatizo hili kwa kuwa na uelewa mkubwa sambamba na kipato kumbe ndivyo sivyo. Matukio mengi ya wanaume kutuhumiwa kutoka nje ya ndoa kwa utafiti wangu mdogo hutokea baada ya wahusika kupata mtoto.Hapo ndipo utakuta mume huanza kuchelewa kurudi nyumbani kwani harufu za nepi na maziwa ya Mama hugeuka kero kwa wanaume wengi japokuwa hawasemi. Pia mtoto anapoanza kujitambua (2yrs old) mara nyingi wazazi hupata wakati mgumu haswa kufanya tendo la ndoa huku mtoto akiwa pembeni kwani wakimshitua tu inakuwa half time hadi alale. Changamoto hii hugeuka mzigo zaidi kwa vijana wakiwa katika nyumba za kupanga kwani chumba 1 hakitoshi kwa wanandoa na watoto hivyo vijana tujitahidi kuweka akiba na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuandaa mazingira bora ya familia kuishi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom