Watoto wamtuhumu baba yao kutaka kupora ardhi aliyowagawia, Baba adai wamekua wakatafute ya kwao

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Mgogoro wa kugombea Mali ikiwemo ardhi na majengo umeibuka katika familia ya Mzee Kamakia mara baada ya watoto wa mzee Huyo kumtuhumu baba yao kutaka kuwapora ardhi ambayo waliachiwa urithi baada ya marehemu mama yao, kufariki dunia.

Mgogoro huo ambao umevuta hisia za wakazi wa eneo la Kijenge na ndani ya jiji la Arusha umepelekea kuvuruga amani ndani ya familia hiyo.

Baadhi ya watoto wa Mzee Kamakia akiwemo Nusin Kamakia walidai kwamba hatua ya baba yao kutaka kupora maeneo yao ilifuatia baada ya mama kufariki dunia miaka mitano iliyopita ambapo baada ya mazishi baba yao alianza mipango hiyo kwa kuleta watu mbalimbali katika maeneo yao kwa kulenga kuwauzia ardhi yao.


Mtoto mwingine wa Mzee huyo aliyetambulika kwa jina la Bella Kamakia alidai kwamba kabla ya mama yao kufariki dunia baba yao alikuwa akiishi wilayani Loliondo na mwanamke mwingine na pindi baada ya mazishi ya mama yao ndipo matatizo yalipoanza.

Alieleza kwamba Mara walipomzika mama yao baba yao alianza kuleta watu mbalimbali wakiwemo wanajeshi kwa lengo la kununua ardhi waliyoachiwa kama sehemu ya urithi wa mama yao.

"Marehemu mama yetu alipofariki baba alikuja kuhudhuria mazishi kutoka Loliondo na pindi tulipomaliza kumzika ndipo baba yetu akaanza kuleta watu wa kutaka kununua ardhi yetu ambayo tuliachiwa kama sehemu ya urithi wa mama yetu" alisema Bella

Hatahivyo,Henry Kamakia alidai kwamba wanaiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwa kuwa limesababisha usumbufu wa Mara kwa Mara ndani ya familia yao.

Akijibu malalamiko hayo Mzee Kamakia alisema kwamba ardhi inayolalamikiwa na wanawe ni Mali yake kwa kuwa alitafuta kwa nguvu zake na hajawahi kutoa urithi kwa mtu yoyote.

Mzee huyo alifafanua kwamba jambo lililomchukiza mpaka kutofautiana na wanawe ni kitendo cha wao kushindwa kuhudhuria harusi ya mke wake mwingine baada ya mke wake wa awali kufariki.

"Wale watoto hakika wamenivua nguo kabisa kitendo cha wao kukataa kuja kwenye harusi yangu walinichukiza kabisa na wamenivua nguo" alisema Mzee huyo

Mzee Kamakia alisema kwamba suala la yeye kutuhumiwa kuuza maeneo na wanawe si kweli kwa kuwa yeye anauza ardhi ambayo ni Mali yake kihalali na endapo watoto hawafurahishwi na uamuzi wake wana haki ya kwenda kutafuta ardhi yao kwa kuwa wameshakuwa watu wazima.


Mwisho.
IMG-20200422-WA0070.jpeg
IMG_20200422_142342_512.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyamadoke75, Huyu mzee hata busara hana eti wamemvua nguo anajua maana kuvua nguo huyu nilifikiri aliumwa wakashindwa hata kumhudumia kumbe harusi apimwe akili huyu mzee
 
Babu anazingua anatumika hapo watoto wapambane la sivyo mshua akikata kamba watabako empty..

Najua humu mnaongea tuu yani wewe unakua unamuona mama yako anapambana na baba kusaka mali afu mama anakufa mali baba hauzi afu ghafla anatokea demu mpya wa baba tena mnalingana nae afu mali zinaanza kuuzwa mtakubali sio easy hivo..

Watoto wa Mengi wenyewe wametia ngunu kwa K lyn haya mambo magumu sana kama mzee age imesonga afu anachukua dogo dogo yani mzee anaoa demu mdogo kuliko wanae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Ameharibu kwenye kuingiza chombo kipya la sivyo kijana kung'ang'ania ardhi ya urithi wakati mapori hayana watu ni kukwama kama kichwa cha familia kijacho.
 
Mwali anavizia urithi na vijana wa mzee wamestuka. Sasa na wao malalamiko yao yawe mzee anatapeliwa Mali zake na huyo mwali,hivyo mzee hasiuze Mali kwa sababu kwa umri wake hawezi kujisimamia.
 
Back
Top Bottom