Watoto Walindwe: Mtoto apigwa kama mnyama, ugomvi wangu ni huyu aliyechukua hii video anaroho mbaya sana

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,431
2,000
Wazazi na jamii kwa ujumla hatuna budi kuwapa ulinzi watoto mahali popote pale unapokutana na tukio ambalo si la kiungwana kwa watoto, mtoto hata kama si wako ni wajibu wako kumlinda.

Nimetafakari nikakosa majibu huyu aliyekuwa anachukua video hii alikuwa na roho gani? Badala ya kumuokoa mtoto anapiga Picha, inasikitisha sana.

Huyu mama anatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria, maana huu ni uhalifu.
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,903
2,000
Huyu mtoto sidhani kama atakuwa hai! Mama lina roho mbaya kama li meneja langu! Halafu huyo aliyechukua hiyo video anatakiwa awajibishwe! Tuanze na mleta mada amtaje aliyemtumia! Ila TCRA na Polisi kitengo cha cyber crime nao dhaifu sana!
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
23,316
2,000
Halafu huu ugonjwa wa kuchukua video matukio ya ajabu umeingia watu sana, kiasi mtu anaweza kuwa anaungua moto mtu yuko busy anarekodi.

Kuna moja wadada wanapigana, mmoja akakabwa, kashikwa kisawa sawa mpaka anaanza kurusha miguu, ishara ya kukata roho jitu linarekodi tu mpaka akatulia, kimyaaaa.

Sasa hapa lengo lilikiwa jema tu, kwamba "oneni anachofanya huyu mama" lakini mtoto ndio anateketea sasa.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
8,799
2,000
Wazazi na jamii kwa ujumla hatuna budi kuwapa ulinzi watoto mahali popote pale unapokutana na tukio ambalo si la kiungwana kwa watoto, mtoto hata kama si wako ni wajibu wako kumlinda.

Nimetafakari nikakosa majibu huyu aliyekuwa anachukua video hii alikuwa na roho gani? Badala ya kumuokoa mtoto anapiga Picha, inasikitisha sana.

Huyu mama anatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria, maana huu ni uhalifu.
View attachment 1793963
Asingerekodi ungejuaje kuwa kuna mtoto alipigwa somewhere?!
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
8,799
2,000
Huyu mtoto sidhani kama atakuwa hai! Mama lina roho mbaya kama li meneja langu! Halafu huyo aliyechukua hiyo video anatakiwa awajibishwe! Tuanze na mleta mada amtaje aliyemtumia! Ila TCRA na Polisi kitengo cha cyber crime nao dhaifu sana!
Kwa mfano asingerekodi na huyo mtoto anapigwa kila siku na huyo mnyanyasaji, je wewe ungejua kinachoendelea?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom