Watoto wako hutawaachia Barabara na Mabomba ya maji na Umeme kama urithi

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,472
8,692
Ukisoma Maendeleo ya nchi kama Korea Kusini ambao juzi kati wakati tunapata uhuru tulikuwa almost the same.

Ila Korea Kilichowafanya watupuge bao ni uwekezaji wao mkubwa sana kwenye elimu ambapo ndio leo hii wanatuundia simu bora kabisa Duniani.

Huku kwetu tumekuwa tunashangilia kuahidiwa Barabara, Majosho ya Mifugo, Maji huku vitu muhimu sana kama elimu ikiwa hoi.

Kwa Speed hii ya Sayansi ya Dunia na Elimu yetu ilivyo tutapata shida sana.

Watoto wako Urithi Bora kwa Dunia ya sasa ni Elimu na sio mabomba ya maji wala Barabara.

TUKATAE AHADI ZA KIJINGA TUTAKE AHADI ZENYE FEATURE KWA VIZAZI VILIVYOPO NA VIJAVYO
 
Ni kweli
Korea Kilicho wafanya watupuge bao ni uwekezaji wao mkubwa sana kwenye elimu ambapo ndo leo hii wanatuundoa simu bora kabisa Duniani.
 
Kwahyo unataka serikali ndio ikusomeshee watoto wako huku ww uwe unakula balimi mitaani na kubeti?? Somesha watoto wako eboo!
Uzuri JF tunavumiliana,kuna watu uelewa wenu ni wa kusuasua lakini mwisho wa siku mnaeleweshwa taratibu na mnaelewa hoja!!!
Mleta mada kakusudia kusema elimu inayopatikana sasa haina tija sana kwenye dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia!Kuna haja kubwa sana serikali kuwekeza zaidi kwenye elimu,maana yake kufumua mfumo wa elimu ili basi watu wakawe wavumbuzi au watatuzi wa changamoto zinazotukabili!
Mfumo wa elimu uliopo ni wa kupata ajira na kupata ugali wa kila siku!
 
Subiri serikali, ila ujue imekula kwako. Waache kukwapua kwa ajili ya njaa zao wampe mwanao elimu? Umeamua kuzaa, somesha mwanao popote kwenye elimu bora.
 
Mfumo wa elimu wa nchi hii unahitaji kufumuliwa kuanzia chini kabisa, yani tunasoma elimu ambayo haina tija inatengeneza magraduates ambao wana vyeti tu. Tuanahitaji watu wenye technical skills wengi zaidi, ndiyo maana nilishangaa vugu vugu la kila chuo kuanza kutoa degree.
Lakini pia barabara, maji, umeme ni muhimu sana katika maendeleo ya watu. Watu wanahitaji barabara kusafiri na kusafirisha mazao, watu wanahitaji maji safi kumbuka maji ni uhai, watu wanahitaji umeme katika uzalishaji.
Sisi tumebaki nyuma kwasasababu ya policies mbovu mbovu. Haiwezekani nchi masikini, shule nyinyine hazina hata madarasa, halafu eti inafanyika kampeni ya uchaguzi ya viongozi zaidi ya watutu wanazunguka nchi nzima wakiwa na misafari ya magari zaidi ya 150, tena V8, Yani hapo kuna posho, mafuta, n.k.
 
Subiri serikali, ila ujue imekula kwako. Waache kukwapua kwa ajili ya njaa zao wampe mwanao elimu? Umeamua kuzaa, somesha mwanao popote kwenye elimu bora.
Kila mtu ataweza kumpeleka mtoto wake ughaibuni kupata elimu iliyo bora?Ni wajibu wetu kusema ili serikali itakayoingia madarakani iangalie namna ya kuboresha elimu iendane na dunia ya sasa!
 
Mi nawazaga urithi bora kabisaa wa mtoto ni mali..elimu ni upuuzi tu....watu wana PhD, maprofesa bado wanasubiri mshahara kwa serikali...na ajira zenyewe itafikia mahali watu watakosa pamoja na elimu yao.

Mi natafuta mali niwaachie wanangu.
 
Na kwakuongezea wanaogundua vitu vyote wala si wasomi

Is just a talent.
talent does not automatically rise to the top, like bubbles in beer🍻. To be translated into outstanding accomplishment, talent must be nurtured in the home, developed by the right kind of teachers and honed by years of continuous training and practice.
 
Uzuri JF tunavumiliana,kuna watu uelewa wenu ni wa kusuasua lakini mwisho wa siku mnaeleweshwa taratibu na mnaelewa hoja!!!
Mleta mada kakusudia kusema elimu inayopatikana sasa haina tija sana kwenye dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia!Kuna haja kubwa sana serikali kuwekeza zaidi kwenye elimu,maana yake kufumua mfumo wa elimu ili basi watu wakawe wavumbuzi au watatuzi wa changamoto zinazotukabili!
Mfumo wa elimu uliopo ni wa kupata ajira na kupata ugali wa kila siku!
Point ni ya muhimu lakini kukataa maendeleo mengine ya vitu ni ujinga.

Kwani hatuwezi kuboresha maendeleo ya elimu huku mambo mengine ya kuboresha miundo mbinu yakisonga?

Nadhani kwa point ya elimu ingejadiliwa bila kubeza mambo mengine yanayofanywa na yaliyokwisha kufanywa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mfumo wa elimu ufumuliwe lakn Africa au Tanzania itabaki kuwa chini tu labda washuke jeshi la malaika toka mbinguni ndio waje waingoze Tanzania au Africa ndio itaendelea.

Kwa wasomi waliopo walitosha kabisa kuibadili Tanzania endapo tu wangekuwa wanatumia taaluma zao ipasavyo.

Angalia leo hii maprofesa, madaktari wamtupa taaluma zao kwenye makabati badala yake wanaenda kupiga magoti kwa mlala hoi ampe ulaji. Wakat maprofesa wa wenzetu wanajifungia maabara wakiibua mambo mazito.

Tatzo ni moja tu ubinafsi. Kila mtu anaangalia tumbo lake na watoto wake.
 
Point ni ya muhimu lakini kukataa maendeleo mengine ya vitu ni ujinga.

Kwani hatuwezi kuboresha maendeleo ya elimu huku mambo mengine ya kuboresha miundo mbinu yakisonga?

Nadhani kwa point ya elimu ingejadiliwa bila kubeza mambo mengine yanayofanywa na yaliyokwisha kufanywa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio elimu tu,mambo mengine yote ni kama yamesimama kupisha ujenzi na ununuzi wa ndege!Ukiona wizara ya ujenzi inapelekewa 228% ya bajeti iliyopangwa na bunge huku sekta kama kilimo na maji zikipelekewa chini ya 40% ya bajeti unaweza kuona nini kipaumbele cha serikali hii!
 
Ukisoma Maendeleo ya nchi kama Korea Kusini ambao juzi kati wakati tunapata uhuru tulikuwa almost the same.

Ila Korea Kilichowafanya watupuge bao ni uwekezaji wao mkubwa sana kwenye elimu ambapo ndio leo hii wanatuundia simu bora kabisa Duniani.

Huku kwetu tumekuwa tunashangilia kuahidiwa Barabara, Majosho ya Mifugo, Maji huku vitu muhimu sana kama elimu ikiwa hoi.

Kwa Speed hii ya Sayansi ya Dunia na Elimu yetu ilivyo tutapata shida sana.

Watoto wako Urithi Bora kwa Dunia ya sasa ni Elimu na sio mabomba ya maji wala Barabara.

TUKATAE AHADI ZA KIJINGA TUTAKE AHADI ZENYE FEATURE KWA VIZAZI VILIVYOPO NA VIJAVYO
Wazazi wetu hawakusoma, hawajui thamani ya elimu na serikali inalitumia hilo kujinufausha kisiasa. Serikali haijawekeza kwenye elimu na inafanya mengi kuwasadikisha wananchi kuwa hakuna haja ya elimu, eg hakuna kiwango cha elimu kwa wabunge au madiwani zaidi ya kujua kusoma na kuandika, kutoajiri wahitimu nk. Nchi jirani ziawekeza sana kwenye elimu, linganisha wahitimu vyuo vikuu Kenya na Tanzania utalia.
 
Wadau heshima zenu tafadhali naomba msaada anaejua benki inayotoa mkopo kwa wastaafu kwa riba nafuu.asanteni
Kwahyo unataka serikali ndio ikusomeshee watoto wako huku ww uwe unakula balimi mitaani na kubeti?? Somesha watoto wako eboo!
mpuuzi wewe ,
watoto wanasomeshwa na mawe. tunaomba nyongeza ya mshahara na punguzo la makato ya mkopo wa elimu ya juu ili tuweze kusomesha watoto
 
Ukisoma Maendeleo ya nchi kama Korea Kusini ambao juzi kati wakati tunapata uhuru tulikuwa almost the same.

Ila Korea Kilichowafanya watupuge bao ni uwekezaji wao mkubwa sana kwenye elimu ambapo ndio leo hii wanatuundia simu bora kabisa Duniani.

Huku kwetu tumekuwa tunashangilia kuahidiwa Barabara, Majosho ya Mifugo, Maji huku vitu muhimu sana kama elimu ikiwa hoi.

Kwa Speed hii ya Sayansi ya Dunia na Elimu yetu ilivyo tutapata shida sana.

Watoto wako Urithi Bora kwa Dunia ya sasa ni Elimu na sio mabomba ya maji wala Barabara.

TUKATAE AHADI ZA KIJINGA TUTAKE AHADI ZENYE FEATURE KWA VIZAZI VILIVYOPO NA VIJAVYO
Barabara, mabomba, umeme n.k ni miundombinu inayowekwa na serekali ili uitumie kujipatia maendeleo ambayo utawaachia wanao kama urithi. Hakuna nchi, inayotoa urithi kwa watu wake, hakuna taifa linalowapa pesa wananchi wake.
To be honest, Chadema hamuwezi wapa watu maendeleo.Mnachokitaka ni dola ili muuze nchi hii kwa beberu zenu. Wananchi wote wa taifa hili, hawatakubali ujinga mnaopanga kulitenda taifa hili linalojitahidi kuinuka. Maendeleo ya nchi, huletwa na wananchi wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii na sio mabeberu.
 
Mkuu, ama sijakuelewa au nikupe pole kwa uelewa duni wa masuala ya uchumi wa kimataifa.

Kwa msaada tu jitahidi kufahamu juu World System Theory. Fahamu maana ya Core; Semi-peripheral na Peripheral countries. Kwanini China; Russia; South Africa; India; Brasil wenye uwezo kutishiana misuli ya kiuchumi na Western Block wanaendelea kuwepo kundi la Semiperipheral wakati kuna wachovu kama Spain na nyingine hata Mabeberu wanaona aibu kuzitaja zikiendelea kuwepo kundi la Core countries.

Kuhusu Elimu, kwani hatuna Watanzania waliosoma huko kwa Mabeberu? Kwa mfumo huu wa uduni wa miundombinu ya huduma ya barabara, umeme, maji n.k. unatarajia Msomi anaweza ku-utilize elimu aliyonayo na kupambanisha bidhaa yake katika soko?

Kwa taarifa yako, JPM ni miongoni mwa Kizazi cha Tatu cha Viongozi Asili wa Afrika (baada ya Mkwawa; Rumanyika,...ambao walikuwa kizazi cha Kwanza waliokuwa na uwezo wa kutofautiana na Sera za Mabeberu; wakifuatiwana akina Nkurumah; Nyerere; Lumumba...). Wanaomwamini JPM kuwa anao uwezo wa kuboresha miundombinu ya elimu, afya, usafiri (anga, barabara na majini) watarithi uchumi uliobora na usalama wa mali (mali asili, madini) za nchi. VIVA MAGUFULI -The 3rd Generation of True/Natural African Leaders

Kwasasa tunawaona wanaojitokeza kuomba Ridhaa ya Uongozi wakati walituaminisha kuwa Tulipe madeni kwa Matapeli wa Kimataifa la sivyo Ndege ATC zitataifishwa na kupigwa mnada. Kuzuia madini (makinikia) Acacia watatufungulia mashtaka katika Mahakama za Kimataifa na kufilisiwa kwa kuwalipa fidia kubwa.
TZ ni nchi Maskini; Hatuwezi Kufanya Lolote la Maendeleo Bila Msaada wa Mabeberu. Mjiandae kisaikolojia, 28/10 mnakataliwa na WaTZ
 
mpuuzi wewe ,
watoto wanasomeshwa na mawe. tunaomba nyongeza ya mshahara na punguzo la makato ya mkopo wa elimu ya juu ili tuweze kusomesha watoto
Ww ndio mpuuzi umefanya kazi miaka 20 lakn bado unalalamikia nyongeza ya mshahara.

Umeshindwa hata kujiwekea kiingiza kipato cha ziada.
 
Uzuri JF tunavumiliana,kuna watu uelewa wenu ni wa kusuasua lakini mwisho wa siku mnaeleweshwa taratibu na mnaelewa hoja!!!
Mleta mada kakusudia kusema elimu inayopatikana sasa haina tija sana kwenye dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia!Kuna haja kubwa sana serikali kuwekeza zaidi kwenye elimu,maana yake kufumua mfumo wa elimu ili basi watu wakawe wavumbuzi au watatuzi wa changamoto zinazotukabili!
Mfumo wa elimu uliopo ni wa kupata ajira na kupata ugali wa kila siku!
Ameshakuelewa huyoo ukiona kimyaa jua kichwani kuna kitu kimemuingia kimeongeza ufahamu
 
Maji na umeme ni vya muhimu sana, kuvibeza hivi sikubaliana nawe kabisa. Hayo maendeleo hayatofikiwa bila hivi vitu kuwepo.
 
Back
Top Bottom