watoto wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

watoto wake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Penny, Feb 6, 2009.

 1. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani za leo, mimi niko kwenye ndoa ya karibia mwaka sasa, huyu mwanamme alidivorce ndoa ya kwanza na anawatoto. Cha ajabu huyu bwana hana hata mawasiliano na wanae hata kuwajulia hali hamna. Kwa kweli nimekuwa nikimkazania sana kwenda kuwaona wanae akaanza vizuri kulingana na sheria ya hizi nchi za wenzetu (one weekend watoto kwa baba then the other kwa mama)ila kutokana na mambo yao walivyoafikiana ambayo siyajui hawezi kuchukua watoto na kukaa nao zaidi ya kwenda kuwachukua na kuwatoa out tuu then kuwarudisha kwa mama yao. Katika mda huu toka niolewe wote kwa kweli sijawaona hao watoto machoni mwangu. Toka mwaka huu umeanza baba hajaona watoto kwa madai yake yuko buzzy! kwa kweli sielewi nini cha kufanya, kumsharuri...!
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wewe shida yako hasa nini? ni just upendo kwa hao watoto wa mwenzio au kuna lingine au sijakusoma vizuri?
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuna msemo kwenye kabila moja la hapa Bongo usemao kuwa upendo wa baba kwa watoto umeshikiliwa na mama!! Ikiwa na maana kuwa kama mambo kati ya baba na mama hayaendi (hasa hasa chakula cha usiku) basi mzee hana shida na watoto. Kwa ufupi, hataki kusikia hizo story za watoto. Kwa upande wako, ama ujue kuwa huyo baba hana deal na interest na mama wa watoto; kwa hiyo inampa taabu kwenda kuwaona watoto au ndo tabia yake. Kwamba yeye na mama tu. Mambo yakiisha kila kitu ni historia! Hebu endelea kuchunguza ndugu yangu, mwenzio akinyolewa........!!
   
 4. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  labda anaogopa/hapendi bughudha za mama watoto anazozijua/mjua,anajua labda akiwachukua ndio mwanzo wa malumbano baina yenu, kwa nijuavyo mimi kweli angestahili kuwaona angalau mara moja/mbili kwa mwezi coz ni wanae jamani, mimi nilimkuta mume wangu na mtoto but tulikubaliana kabla ya kufunga ndoa kwamba baba atahitaji tuishi pamoja na mtoto, na ndivyo tulivyo na huwa anaenda kumsalimia mamake wkend,akitaka analala huko asipotaka atasema aje achukuliwe, maisha yanasonga.
   
 5. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Langu ni kwamba nakuwa na wasiwasi, je kama ndo anavyowatendea watoto waliotoka kwenye kiuno chake hivi kweli na mimi ntakuwa katika upande gani kwake!
   
 6. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni kweli dada, maana hapa ndo maneno hunza mara ooh mke wake kamshikilia mara kawekewa limbwata...kumbe ni akili zake tuu. Mwee, baada ya mimi kuwa mkali sana ndo akaanza kwenda kuwaona kama mara tatu hivi, baada ya hapo jiii toka mwaka umeanza.
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  wewe ni mke, wao ni watoto. Kuna tofauti hapo ya Mapenzi, ningekuelewa wasiwasi wako iwapo ungetaka linganisha mapenzi yake kwa wanao/mwanao.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mi naona unajishitukia tu, kuna mambo mengi sana yanaweza kuchangia hali hiyo ikiwa ni pamoja na mambo ya mshiko, au amefall in love sana na wewe au wale watoto hawamheshimu au mama yao hamjali kama mzazi mwenzie etc.

  Kama hana fedha za kutosha au kama kipato chake si cha uhakika, then usitegemee awatembelee vijana wake mara kwa mara, kwa sababu hawezi kuwatembelea mikono mitupu lazima awabebee zawadi kidogo au hela na akifika huko yule mama kama hana busara, atawapandikiza watoto wamwambie baba yao mimatatizo kibao kisa atolewe fedha za kutosha! au kama amekufia sana wewe nayo inaweza kusababisha kupunguza upendo the other side au pia inawezekena akienda kuwaona vijana wake mama anamwona kama choo imeingia nyumbani pale, so akifika tu watoto wanapewa ratiba kabambe za kazi, mara kelete kile, au nenda sehemu fulani au kuwapigapiga mikwara ya hapa na pale, ili mradi tu kumkosesha raha huyo bwana!

  Cha msingi wewe ndo mwenye nyumba now, mpende tu mmeo hope naye atakupenda! Usimlazimishe akawaone watoto wake every time, cause binafsi na dought huo upendo unatoka wapi, kawaida wanawake walio wengi huwa hawawapendi watoto waliowakuta au wa nje ya ndoa, labda wewe ni exceptional sijui! Lakini ni vizuri ukawa realistic sio kupretend!

  Cheers
   
 9. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante sana kwa uchambuaji wako ndugu, nikweli alishawahi kulala mika anapewa ma bill yasiokuwa na mpangilio!ok now i have got you very clearly. Swala la kupretend naomba nikupe pole maana mimi mwenyewe nimelelewa kama mtoto wa kambo na ninajua maswala yote. Siwezi kupretend maana in the long run time will tell!
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Good penny!

  Usinipe pole mimi, bali mimi ndo wakukupa pole na kukuonea huruma kwaajili moyo wako unaotaka kupondeka!

  Infact mi sijasema unapretend, ila nilikuwa nakutahadharisha kama una pretend, kama si hivyo from your bottom part of your heart...mibaraka itakushukia kama mvua! Amen
   
 11. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante sana kwa kunitakia heri njema, nami pia na imani hiyo Mungu atanimiminia hiyo mibaraka one day. Ubarikiwe sana ndungu.
   
 12. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Exactly mbuu, nikweli kabisa maana kibinadamu lazima utafikiri mengi. Maana kama hana hela ya zawadi basi hata awe anawazumzia (that he miss them...) kha!
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwanini ali ku divorce? lilikuwa ni kosa lako?ndio maana unaona aibu kwenda mahakamani kudai matunzo ya watoto? tuambie kiundani zaidi kulitokea nina ili tukusaidie. kuna wanasheria wengi sana humu ndani wanaweza wakakupa ushauri ukatatua tatizo lako mara moja.
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nenda kwenye marriage revival party kule kwa lwakatare, anaongelea madhara ya divorce na mambo yanayofanana na hayo kwa wanawake na wanaume kama unataka kusolve kiroho.
   
 15. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  soma maelezo vizuri ndugu, nadhani utakuwa hujaelewa mada. asante kwa ushirikiano wako.
   
 16. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa maelekezo, natumaini siku nikija DAR inabidi nifanye naye appointment ili nipate chakula cha roho.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Penny,

  Your concern is justifiable! Just read again my post #3.

  May be that is how he behaves. He can only deal with one thing at a time! You are now the queen and everything else is not a priority including his own kids. Just explore deep, because you might be the next victim after all he wanted/admired is gone!
   
 18. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kama utakuwa na pesa, unaweza kumwona mwanasheria ukafungua fail incase unataka kusolve kibinadamu yaani kimwili. hapo unakuwa umeingia vitani ama zako ama zake. jino kwa jino yaani. na kwa hali unayoongelea, hauna kosa hata kama uliachwa kwa kosa lako wewe, mwanamme wako analazimishwa na sheria kumtunza huyo mtoto wako.kwani mlipopewa amri ya talaka watoto waliambiwa watatunzwaje? kwasababu mahakama inapotoa talaka(talaka zote lazima zitolewe mahakamani, sio nyumbani au sehemu za dini), mahakama iliarrange vipi watoto wataishi, na mali mtagawana vipi, ndio maana nilisema mwone mwanasheria. ila, kuna uwezekano mkubwa sasa kwako kushinda hiyo kesi, na utampiga faini na watoto wako watapata matunzo ya lazima, jamaa atalazimishwa auze hadi nguo zake lakini atoe matunzo kwa watoto wenu.

  kama wewe ni mkristo, kwa sheria za kikristo, nakushauri mwombe Mungu ili mrudiane na huyo mumeo wa zamani. msameheane na mrudiane. talaka katika ukristo haipo, mkishaoana tu hakuna talaka hadi kufa. hivyo huyo bado ni mume wako, mwombe Mungu alainishe mioyo yenu ili mrudiane kama kwanza.mtu anayetoa talaka na kuoa au kuolewa na mtu mwingine, anazini. hivyo kama mliachana na mumeo wewe ukaolewa na yeye akaoa, bado mnazini kila siku, mbele za Mungu mnazini. mtapata raha lakini jehanum inawasubiria hadi hapo mtakaporudiana. huo ndio ukweli wa Bible.mwombe Mungu akusaidie upate njia ya kutokea.alichokiunganisha Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha.mtu atamwacha babaye na mamaye ataunganishwa na mumewe, na hao watakuwa mwili mmoja. hivyo, ndani ya mwili uliommoja(ndoa)mmoja ama ambaye ni kiungo kimoja kikiondoshwa mtu anakuwa kilema hata kama atajiona anafaidi maisha kwa magongo. Yesu alisema hakuna kuachana mkishaoana. na ndoa hata kama hamjaenda kanisani, wazazi wenu wakishawakubalia mkakaa pamoja kama mume na mke, tayari Mungu anaihesabu. katika kitabu cha Malaki Mungu anasema"nachukia kuachana", pia anasema anachukia mtu anayetoka nje ya ndoa/anayezini. Mungu huwa anachukua na anaadhibu watu kama hao.

  naomba kuuliza swali, ni kweli mlioana? na je mlipewa talaka kweli? au mliachana tu. watu wengine kama mwanamme ameamua kumwacha bila hata talaka huwa wanasema wamepewa talaka kwakumaanisha kuachwa. talaka lazima itolewe na mahakama.hivyo ili wachangiaji humu ndani wakupe ushauri mzuri zaidi, wewe eleza vizuri kama ni talaka kisheria au ni kuachwa kwa kawaida. hata kama mtakuwa mlikubaliana wawili kwamba "bwana kila mtu achukue hamsini zake wewe ukakubali na yeye akakubali" hiyo sio talaka kama haijatokana na amri ya mahakama. lakini ni vizuri mkarudiana mtunze watoto wenu, ni kitu kibaya sana watoto kukua wakijua wazazi walishatalikiana, na mara nyingi watoto wanaokua na baba au mama wa kambo huwa si sawa kiakili na kimaendeleo na watoto wanaokuwa wakiuona upendo wa wazazi wote wawili. God bless you.
   
 19. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  THANKS FOR THE COMMENTS NAOMBA UREJEE KUSOMA VIZURI MADA HAPO CHINI!
  Jamani za leo, mimi niko kwenye ndoa ya karibia mwaka sasa, huyu mwanamme alidivorce ndoa ya kwanza na anawatoto. Cha ajabu huyu bwana hana hata mawasiliano na wanae hata kuwajulia hali hamna. Kwa kweli nimekuwa nikimkazania sana kwenda kuwaona wanae akaanza vizuri kulingana na sheria ya hizi nchi za wenzetu (one weekend watoto kwa baba then the other kwa mama)ila kutokana na mambo yao walivyoafikiana ambayo siyajui hawezi kuchukua watoto na kukaa nao zaidi ya kwenda kuwachukua na kuwatoa out tuu then kuwarudisha kwa mama yao. Katika mda huu toka niolewe wote kwa kweli sijawaona hao watoto machoni mwangu. Toka mwaka huu umeanza baba hajaona watoto kwa madai yake yuko buzzy! kwa kweli sielewi nini cha kufanya, kumsharuri...!
   
 20. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mhhh kazi kweli kweli achana na hao watoto kwa vile ni wake na mwanamke ameshamuacha sasa wewe fatilia watoto wako wapo vipi!! Kama wanakulala na kulala na baba yao anawapa huduma basi sio mbaya.Pia angalia mapendo anayowaonyesha watoto wako na wale watoto wengine yapo vipi???Hapo nadhani unaweza kupata jibu zuri!!
   
Loading...