Watoto wafia kwenye gari kwa kukosa hewa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,847
Posted Date::11/29/2007
Watoto wafia kwenye gari kwa kukosa hewa
Jackson Odoyo na Prisca Mussa
Mwananchi

WATOTO wawili wa familia moja wamefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kujifungia ndani ya gari la familia yao. Watoto hao walifariki dunia Novemba 27, mwaka huu.

Watoto hao Polycarp Mrina (4) na Martin Mrina (3) waliingia ndani ya gari hilo muda mfupi baada ya mjomba wao kuliegesha nje ya nyumba yao kwaajili ya kumshusha mgeni wa mama wa watoto hao.

Baada ya kuegesha gari na kuingia ndani na mgeni huyo, huku nyuma watoto hao waliingia ndani ya gari hilo na kuanza kucheza, wakati huo mama yao alikuwa chumbani kwa mazungumzo na wageni wake.

Akizungumza na waandishi wa Mwananchi jana nyumbani kwake muda mfupi kabla ya miili ya marehemu hao kuagwa kwa ajili ya mazishi, mama mzazi wa watoto hao Happines Zamba alisema kuwa siku ya tukio akiwa amelala ndani akisumbuliwa na homa, ghafla akapigiwa simu iliyomweleza kwamba akampokee mgeni wake katika Kituo cha Kukuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo (UBT).

Alisema baada ya taarifa hizo alimpigia simu mdogo wake mwenye gari hilo ili akampokee na kuwapeleka nyumbani kwake.

Akisimulia mkasa huo huku akiwa na majonzi mama huyo alisema baada ya mgeni huyo kufika nyumbani alimlaki akiwa na watoto wake na baadaye watoto hao wakaondoka kwenda kucheza nje na baada ya muda mfupi mdogo wake akatoka nje kwenda kutoa mzigo ndipo alipowakuta watoto hao wakiwa hoi ndani ya gari hilo huku wakiwa wajifungia milango.

Zamba alisema kwamba baada ya hapo mdogo wake alirudi ndani haraka na kuwaita ndipo wakaamua kuwakimbiza hospitali ya Amana kwa kwa tiba zaidi lakini wakati madaktari wakijaribu kuokoa maisha yao mtoto mdogo akafariki dunia.

Mama huyo alieleza kwamba baada ya hapo madaktari wa Amana waliamua kumpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Afya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto mwingine, lakini wakiwa njiani mtoto huyo pia alifariki dunia.

“Siwezi kuzungumza mniache wala siwezi kusimulia mnisamehe”alisikika akilalamika mama wa watoto hao.

Baada ya waombolezaji kumfariji na kumuomba amkabidhi Mwenyezi Mungu kwa sababu kazi ya Mungu haina makosa, alitulia na kukubali kuzungumza.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk Willy Sangu alisema kwamba siku ya tukio hilo alipokea watoto wawili na mmoja akiwa ameshafariki dunia na mwingine akiwa na hali mbaya huku mama yao akiwa amezimia kisha wakampeleka mtoto mmoja kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi wakati huo wakipatia mama yao huduma ya kwanza.

Sangu alisema kwamba uamuzi wa kufanya uchunguzi wa kina kufahamu chanzo cha kifo cha marehemu hutolewa na Jeshi la Polisi sambamba na ndugu wa marehemu hao na si wao.

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mkoa wa Ilala Masindoki Masindoki alisema hajapata taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo Masindoki alimuuliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Buguruni kama kuna tukio hilo, naye alisema kwamba hajapata taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.

Naye Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow alisema hana taarifa hizo na kwamba alikuwa akifanya jitihada za kupata ripoti sahihi juu ya tukio hilo.
 
inasikitisha. May they rest in peace. Hili ni fundisho kwetu wazazi daima tujue whereabouts za watoto, mambo mengine huwa wanajifanyia tu bila kujua athari. Hivi juzi juzi tulisikia baba mmoja huko tabata alimkanyaga na kuua mtoto wake kwa gari kwa bahati mbaya akiwa anareverse gari kumbe mtoto yupo nyuma anatambaa.
with small children we ought to be extremely careful.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom