Watoto wadogo (2-10 years old) ombaomba Dar es salaam: Wizara ya Watoto inafanya nini???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wadogo (2-10 years old) ombaomba Dar es salaam: Wizara ya Watoto inafanya nini????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mabadilikosasa, May 29, 2011.

 1. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani. Inasikitisha. Hawa watoto wadogo kiasi hiki kati ya miaka 2 had 10 katika maeneo ya mnazi mmoja, magomeni, kinondoni, barabara ya ali mwinyi, watakuja kuwa watu wazima wa aina gani??. Unasimamisha gari wanazunguka gari nzima wanaomba msaada!. Je tukiwapa hata hiyo hela watajua kweli matumizi yake? hakuna namna ya kuwapeleka hawa watoto mashuleni wakasoma huko huko na wakala huko?? Hii wazara ya watoto inafanya kazi zipi? au hii wizara haina budget?? Je ccm ina sera zipi za kusaidia hawa watoto. CCM, hizi gharama zote wanazotumia kusafiri mikoani kuelezea kuhusu kujivua gamba (kumbe ni utapeli), na ma V8 yao, sii wangeweza kusaidia hawa watoto ....jamani tuwe na huruma.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  huo ni mtaji wa kisiasa wa ccm.

  wanasubiri mchakato wa katiba ukianza ndiyo wawe wanajaza kumbi
   
 3. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Bahati mbaya watoto hawapigi kura, na wakifikia umri huo tayari ni wajinga wa kutosha kutojua haki zao. Mtaji wa ccm
   
 4. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jamani jamani inasikitisha. Mungu Yupo. Vilio vya hawa malaika maskini vitaiondoa ccm madaraka na viongozi wao watakufa vifo vibaya. rais wa Tunisia aliondolewa madaraka na just a street boy ambaye alikua hana ajira. kabla hawa jamaa wa ccm hawajaenda kwenye ma tv na kutueleza kuhusu mambo ya gamba lao, hebu watusaidie hawa watoto wa mitaani wadogo sana kwenye miji yetu. Jamani matatizo ni rangi yetu, mioyo yetu, au nini kabsa???....wakati mwingine napita barabara nalia mwenyewe!!!
   
 5. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  mabadilikosasa umeleta hoja nzito sana! kwa kweli hili ni bomu ambalo litalipuka muda si mrefu.,watoto hawa wanakulia katika mazingira magumu, hatarishi na yasiyo na malezo bora,. mwisho wake ni kuwa na kundi kubwa la vibaka, majambazi na vijana waliothirika kisaikologia.
  ilani ya CCM inasema hivi au inaahidi yafuatayo:

  1. Kufanya utambuzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi katika wilaya 48 ambazo hazijafanya utambuzi.
  2. Kuanzisha mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Watoto yatima Mazizini Unguja
  3. kupinga ajira kwa watoto
  Kwa kweli sijaona mikakati au ilani kuhusu watoto wa mitaani. labda wenye ujuzi zaidi watusaidie.

  aidha ukisoma The National Costed Plan of Action for Most Vulnerable Children ya 2007-2010 (naona imeshapitwa na wakati na hakuna mpya), definition ya most vulnerable children inataja makundi yafuatayo:
  Using data from the population census, a standard classification of most vulnerable
  children has been developed that incorporates demographic characteristics and indicators
  of poor living conditions. It includes the following children

  • those living in child-headed households
  • those living in elderly-headed households with no adult from 20–59 years-old present
  • those with one or both parents deceased
  • those with disabilities
  • those in rural areas: children with one surviving parent living in a house with poor quality roofing (grass and/or mud) and those with a disability living in similar poor conditions
  • those in urban areas: children with one surviving parent living in a house with poor quality roofing (grass and/or mud) or with poor wall materials or without toilet facilities and those with a disability living in similar poor conditions (source http://www.pacttz.org/pdfs/Tanz_NCPA_web.pdf)
  katika makundi haya sioni ambapo wametajwa watoto wanaoishi mitaani na kwa msingi huo hakuna mkakati wowote wa kuwaokoa (again, mwenye maelezo tofauti anijuze).

  Sera ya maendeleo ya mtoto ya 1996 (Children Development Policy 1996) inaipa majukumu Wizara inayohusika na Ustawi wa Jamii (in this case Ministry of Health and Social Welfare) kuhakikisha watoto walio katika mazingira magumu wanapata haki na huduma muhimu. Aidha wizara zinazohusika na Maendeleo ya jamii na Elimu zinatakiwa kuhakikisha watoto wanapata elimu. nimependa sentensi hii kutoka kwenye SEra tajwa: It should develop a system whereby children of parents or guardians who are unable to pay will still get education (section 69 page26)". Aidha kifungu Na. 92 kinaeleza jukumu la serikali kuhakikisha inatenga rasilimali kwa ajili ya watoto walio katika mazingira magumu. sasa swali linalobaki Je utekelezaji unafanyika? kama unafanyika Je hawa watoto wa mitaani wametushinda nini?
  nawasilisha tujadili mada hii muhimu sana!!
   
 6. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  watoto wamesahaulika, watoto wanateseka saana. Niwaombe basi vyama vya siasa mfano chadema. kwa kuwa mna vijana wing, wanawake wing, naomba pia muwe na watoto wing. watoto hawapigi kura lakini mkiwatetea watoto mtajenga mazingira mazuri ya kupendwa na wana jamii wote, pamoja na wapiga kura wengi. Kuweni na idara ya watoto, na muwe na viongozi maalumu kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya watoto...........vijana wanatokana na watoto....tutafute watetezi wa watoto katika ngazi ya siasa. wamesahaulika sana
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Siamini hata kidogo kwamba watoto wote walioko barabarani ni Yatima. Na hata matumizi ya haya maneno 'wanaoishi kwenye mazingira magumu' yameibuka siku hizi za karibuni. Ndio wapo watoto yatima lakini walio wengi ni biashara za watu wazima. Cha kushangaza hawa watoto wako mtaani saa za masomo which means tayari wameshaondelewa kwenye mfumo wa elimu.

  Kwa nchi yeyote kuongelea maendeleo bila kuwekeza kwa wananchi wake na niseme kwenye elimu ni 'false strategy'. Karibu miji yote mikubwa hapa Tanzania wapo watoto wanaoombaomba au wanasafisha vioo vya magari. What future awaits for these little ones?

  Sophia Simba sijamskia akisema chochote kuhusu hili. Na hata kama ataulizwa leo nahisi atasema yafuatayo: "Serikali inalijua hili na tuna mpango wa kuangilia jinsi ya kulitatuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimabali, lakini tunatoa wito kwa jamii ili itoe ushirikiano maana hili ni tatizo la jamii nzima na sio serikali peke yake" . Hii ndiyo inaitwa RHETORIC.

  Sasa, CHADEMA wanaweza kabisa kumdhoofisha Sophia Simba na kwa maana hiyo wakaidhoofisha serikali iliyoko madarakani kwa kuonesha ni jinsi gani (serikali) wamezembea au hawajali au hawana mkakati wa kuondoa hili tatizo. Scrutinize govt plans, strategy about this problem, na onesha gaps zilizopo, na mtagundua Si Sophia Simba, wala Dr Asha Rose Migiro (aliwahi kushika hii nafasi) amefanya lolote kuhusu watoto wa mitaani. Onesha (walau kwa statistics) idadi inavyoongezeka , na muhimu zaidi onesha direct link between national development na lack of education kwa hawa wototo, plus social unrest. Wizi/pick-pocket ni kosa lakini wakati mwingine mwizi hana namna yoyote ya kuishi. Hawa watoto kama wanakaa barabarini leo wakiwa 5yrs old, je wakifiaa umri wa 25yrs watafanya nini? Nini umuhimu wa Wizara ya Sophia Simba? Can she categorially say in lay man's language kaondoa watoto wangapi mtaani? CHADEMA take this opportunity and show Tanzania you can.
   
Loading...