Haya ndio matatizo ya gutter politics... Katika haya mambo ya kisiasa msingi wa familia yoyote ni mshikamano hasa wakati wa kashfa mbali mbali ziwe za kweli ama uongo. Sielewi uhusiano wa hao mabinti na Waziri Wassira, ila ukweli utabaki lazima kutakuwa na kidoa kimeingia sababu tu ya baadhi ya waandishi waliandika habiri katika misingi ya ushabiki!
Imekuwa ni sifa kutaja watoto wa mkubwa fulani kajiunga CDM nadhani in a way kama kuonesha kuwa watoto hawawakubali wazazi wao na vyama vyao (mara nyingi kutoka CCM). Ile habari ya juzi kuhusu hao mabinti ilielezwa in the lines ya kuonesha Waziri Wassira kana kamba ni baba yao mzazi, kumbe NDIO ni ndugu lakini sio baba yao Mzazi.
Nam support Wassira kuliweka wazi kuwa wale sio wanawe na kwamba wa ndugu yake... ingawa kauli yake inaonesha wazi ni namna gani amekereka; na nawapongeza pia akina binti Wassira kuliweka hili wazi na kulipa ufafanuzi na kutowa upande wao wa shillingi. Haya mambo hayatakoma, yataendelea tu ili mradi ushabiki wa majina makubwa katika siasa yakiendelea kushobokewa... Mambo ya aibu basi tu.
Kwani Stephen Wasira ndiye muasisi wa hilo jina (WASIRA)? Yeye kalikuta na ataliacha kama walivyoliacha mababu zake. Kuonesha hasira kuwa habari imepotoshwa ni ujinga kwani mtoto wa kaka yake kwake ni nani? Cha ajabu kabisa ni kwamba ukimuuliza Wasira habari za maendeleo atakasirika na kuanza kukutajia takwimu za Uarabuni pipa la mafuta limepanda bei, mara Iran na Iraq kuna vita hivyo uzalishaji wa mafuta umepungua hivyo watanzania tusitarajie maendeleo yoyote kwani hata nchi zilizoendelea zimeathirika. Siku zote yeye huwa ni mwenye hasira tu kama jina lake linavyoonesha (Wahasira). Hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.