Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Kwani wangekuwa wa steven wangesaidia nini? Kwanza mzee mwenyewe (steven) chenga tupu. halafu anafikiri nani amfagilie????
 
hawa mabint wapo smart sana na wanajua wanachokifanya Chadema majimbo mawili hayo yameingia wapewe nafasi ktk majimbo, Regia Mtema (RIP) wengine hao Wameibuka ndani ya chama makini.
 
Steven Wassira tumbo joto!

Anajua kwamba comes 2015 kama Steven Wassira (CCM) atapambana na Lillian George Wassira itakula kwake.

Ushauri wa bure kwa Steven Wassira bora jimbo hilo amuanchie Esther Bulaya (CCM) anaweza kufurukuta kwa Lillian Wassira. Count my words.
 
Mimi niliposoma kichwa cha habari basi akili yangu alinijia kuwa ni Kambarage au wale ndugu zake watoto wa Rose.

Haya kazi kwenu. kwani kuna wengi watasafiria nyota za wenzao
 
Joseph Selasini na Masumbuko Lamwai ni ndugu lakini mbona siyo Ishu!!
 
Post deleted
Paw
Haya maneno muwe mnayatamka taratibu. Ina maana huyu binti hana uasili (Gene) wa kina Wasira? Kutokufanana na Steven kuna maanisha nini. Au unamaanisha George ali... aende TBS kutafuta uhalali??
 
WANABODI MNAIKUMBUKA HII
MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.

Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.

Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.

Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.

Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.

Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.

"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.

Pia alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amekuwa akimtumia Leticia kama mtaji wa kisiasa katika kuomba kura.

Katika hotuba yake, Makongoro pia alisema Dk Slaa naye anapoteza muda mwingi kuzungumzia ufisadi, wakati jambo hilo limeshashughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.

Alisema serikali imeshughulikia jambo hilo, kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa.

"Ufisadi ni sawa na kibaka, fisadi anaweza kuwa upande wowote, mbona hata kwao wana mafisadi kibao,ufisadi ni tabia ya mtu,CCM iko safi na ndio maana tumekuwa tukiendesha kampeni zetu kwa ustaarabu bila kutumia matusi. Wnanchi msidanganywe na hoja ya ufisadi mwacheni Dk Slaa aendelee kupiga kelele kuhusu ufisadi,",alisema.

Kwa upande wake, Mansoor alisema akichaguliwa kuwa mbunge, atamaliza matatizo ya maji, huduma za afya na upungufu wa walimu katika shule za jimbo hilo.
 
Mzee Wasira hayuko sawa sawa...soemthing is missing somewhere.

Labda kuna "network error" kichwani kwa waziri wasira. Haiwezekani waziri mzima unaanza kutoa mipasho kwenye vyombo vya habari wakati mipasho yenyewe inagusa familia yako.
 
Back
Top Bottom