Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Asante sana Esther Wasira 0655 048797 kwa ufafanuzi

3.jpg
..

Mhhhhhh!!!!
 
Hawa Ma binti wapewe nafasi ya kugombea UBUNGE kwenye jimbo la Baba yao mdogo kwa kweli itakuwa safi sana sana
Big upu watotot wa WASIRA NI BABA YENU TU HATA KAMA ASEME SIO WAKUWA ZAA NI BABA MDOGO WAO NA NI WATOTO WAKE TU
 
Binafsi namfahamu vizuri ESTHER WASSIRA nilimuacha mwaka mmoja UDSM kitivo cha sheria kwa kweli CDM tumepata KAMANDA wa uhakika na naamini na DADA yake naye ni KAMANDA wa ukweli baba yao mdogo anaweweseka hakutegemea kama mashambulizi yataanza kwenye familia yake kama si ukoo wake WAZIRI WASSIRA anatakiwa ajue MPAMBANO ndo kwanza umeanza wakati anaweweseka na magamba wenzie kina BULAYA, CDM ndo kwanza imeanza safari ya kulichukua JIMBO LA BUNDA.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU


Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira
mmeshakua mastar overnigh.shikilieni hapohapo maana hamtakosa hata ubunge wa kuteuliwa.
Maisha yamekua magumu na bila ubunifu lazima ile kwako.
 
Ahhh ok kumbee ni waandishi ndio walio likoroga
Laiti wange fafanua kusingekuwa na ulakini.Upande shilingi ni wanae
 
Je watoto hawa wana umaharufu gani kisiasa au kijamii huko Tanzania mpaka wachukue nafasi kubwa katika vombo vya habari huko Tanzania?

Mimi ninavyofahamu Tanzania SIO nchi inayotawaliwa kifalme kuwa mtoto wa mfalme laazima aishi kifalme. Huko inawezekana kabisa mtoto wa rais kuwa tarishi. Si jambo la ajabu. Tumeona kwa watoto wa Nyerere ambao mpaka leo hakuna rais, mkurugenzi wala waziri ndani ya JMTz.

Au ndo wanataka kusafiria nyote ya Steven WASIRA?
 
Sasa anayefata ni mtoto wa kumzaa wassira na siku hiyo lazima alie.

Siasa tamu sana hasa ukijua jinsi ya kucheza, cheki wassira ana teswa na jina lake mwenyewe.

Chezea cdm weyeeeeeee!

Daaaaah hadi raha
watoto wa wassira wajiunga na chadema..................... Gazeti

Sio watoto wangu wa kuzaa ni watoto wa kaka yangu:::::::::wassira

Steven wassira ni baba yetu mdogo yani walinyang'anyana ziwa na baba yetu- watoto

Daaaah siasa tamu sana kumbe hawa watoto ni wa wassira bana!

Hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
Shida yetu waafrika tunachanganya sana utamaduni wa kizungu na wa kiafrika kiasi kwamba tunafika mahali fulani tunakuwa hatuelewani dhana tunayotumia ni ipi. Na mara nyingi tunakimbilia kutumia dhana ya kizungu badala ya kiafrika au kitanzania.

Ona suala la "ubaba" linavyotuhangaisha. Wengine wanakubali wasira kuwakataa watoto wake (kwa kutumia dhana ya kizungu). Wengine wanasema kakosea kwani wale ni watoto wake kwa vile ni watoto wa mkubwa wake (kwa kutumia dhana ya kiafrika).

Kwa kweli nadhani kwenye masuala haya ya undugu ni bora tukatumia dhana yatu ya kitanzania: kwamba wale watoto hata kama si wake wa kuzaa kimwili lakini ni watoto wake kwa vile ni wa ndugu yake. Wasira alikosea sana kwa kusisitiza kwamba watoto wale si wake eti kwa vile hakuwazaa yeye kimwili.

Alitakiwa atumie busara. Anasahau mila na desturi za makabila yetu. Ona sasa watoto walivyomkosoa kichini-chini ktk maelezo yao hasa hapo mwishoni wanamwita "baba". kwa lugha nyingine wanamsahihisha namna yake ya kifikiri.

Na ajue kwamba kwa namna moja au nyingine atakuwa amewajeruhi sana wale mabinti kwa majibu yake ya juzi. Ilitosha aseme: "ni wanangu ndiyo, wana uhuru wa kujiunga na chama chochote." Hili lisingeharibu kitu kabisa; tena lingeonesha ni kiasi gani ana hekima. Sasa yeye akakurupuka kuwasimanga wale mabinti. Alikosea sana. Waafrika tujali utamaduni wetu na concepts zetu hasa kwenye masuala haya ya undugu.
 
3.jpg


ahsante kwa kwenda beyond the margin.
Ngoja wadau wamchangamkie kumpa compan.
Mtoto mzuri na atakuwa turufu ya chadema.
 
Back
Top Bottom