Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU


Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa.

Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga
CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema.

Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA.

Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira.

CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu.

Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1).

Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Lilian Wasira 0719 604156
Esther Wasira 0655 048797

 
Haya ndio matatizo ya gutter politics... Katika haya mambo ya kisiasa msingi wa familia yoyote ni mshikamano hasa wakati wa kashfa mbali mbali ziwe za kweli ama uongo. Sielewi uhusiano wa hao mabinti na Waziri Wassira, ila ukweli utabaki lazima kutakuwa na kidoa kimeingia sababu tu ya baadhi ya waandishi waliandika habiri katika misingi ya ushabiki!

Imekuwa ni sifa kutaja watoto wa mkubwa fulani kajiunga CDM nadhani in a way kama kuonesha kuwa watoto hawawakubali wazazi wao na vyama vyao (mara nyingi kutoka CCM). Ile habari ya juzi kuhusu hao mabinti ilielezwa in the lines ya kuonesha Waziri Wassira kana kamba ni baba yao mzazi, kumbe NDIO ni ndugu lakini sio baba yao Mzazi.

Nam support Wassira kuliweka wazi kuwa wale sio wanawe na kwamba wa ndugu yake... ingawa kauli yake inaonesha wazi ni namna gani amekereka; na nawapongeza pia akina binti Wassira kuliweka hili wazi na kulipa ufafanuzi na kutowa upande wao wa shillingi. Haya mambo hayatakoma, yataendelea tu ili mradi ushabiki wa majina makubwa katika siasa yakiendelea kushobokewa... Mambo ya aibu basi tu.
 
Asante sana Esther Wasira 0655 048797 kwa ufafanuzi

3.jpg
 
Biashara ya kuuza habari (magazeti ) nayo imechangia kupotosha hii habari..
 
safi sana.........ila inauma sana watoto wanapokua upande wa pili!!..ila inawezekana pia wamekuja CHADEMA baada ya kukosa nafasi stahiki ndani ya CCM..ingawa mtapinga dada zangu lakini mnatumia kofia ya baba yenu mdogo kujipatia umaarufu hasa ikizingatiwa kwamba wanabif kali sana na CHADEMA..na CDM itawatumia kama silaha ya kumuangamiza.
 
Kudadeki watu mna hasira, itakuweje siku so and so Kikwete akijiunga CDM?
 
Back
Top Bottom