watoto wa wakulima,wafugaji na wafanyakazi tuungane kupinga usaliti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

watoto wa wakulima,wafugaji na wafanyakazi tuungane kupinga usaliti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meningitis, Oct 24, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  rushwa na undugunization ndani ya ccm iko wazi kwani tumeshuhudia na kusikia wenyewe kutoka katika chaguzi za ndani za ccm na jumuiya zake.
  Ccm kama ilivyo serikali yake imeshindwa kupambana na ufisadi au rushwa.
  Ccm ni chama cha wenye nazo!
  Nimesoma na marafiki zangu kadhaa ambao ni watoto wa maskini,watoto wa wakulima,wafugaji wadogo wadogo na wafanyakazi wote wa kipato cha chini au wastani,wote tuliamini kwamba ukiendelea kuwa mtiifu kwa ccm basi iko siku utapata nafasi ya uongozi ndani ya ccm na serikali.ndoto hii imekufa rasmi kwa yale yanayoendelea kutokea ndani ya chaguzi za ndani za chama hiki.
  Sasa ni dhahiri kuwa mtoto wa mkulima,mfugaji au mfanyakazi wa kipato cha chini au kati hana nafasi ndani ya chama hicho,hii inamaanisha ni ndoto kwa vijana wa kada tajwa kushika nafasi ndani ya chama au serikali ya ccm.

  Huu ni muda muafaka wa vijana wenye ndoto zao kuhamia chadema.
  Ndugu zangu na marafiki zangu vijana ni wakati wa kuachana na uroho wa fisi wa kusubiri mkono wa binadamu udondoke ,kamwe haitatokea.

  Mimi nilishtuka miaka kadhaa iliyopita na sasa najisikia faraja kuheshimika ndani ya upinzani.

  Ombi kwa chadema ni moja tu!tuwapokee vijana wenye vision ya kuonyesha vipaji vyao na kuishi ndoto zao za maisha hasa hasa wale watoto wa wakulima,wafugaji na wafanyakazi wa kipato cha kati na chini.

  Vijana wenzangu tuwaachie matajiri na mafisadi chama chao tuache kujidhalilisha na kujipendekeza kwa kina kikwete,malecela,lowassa,mahita,lucy nkya,mwinyi,mwandosya,ndejembi,sumaye,pinda,sumari n.k

  tuungane kuitokomeza ccm iliyowaacha waanzilishi wake na kukumbatia matajiri na mafisadi.

  Vijana njooni tuikomboe nchi.njooni tuungane na kina mnyika,nassari,wassira,zitto,mr 2,nyerere,lema,wenje n.k

  miaka 10 ijayo nchi itatawaliwa na vijana basi tusifanye dhambi ya kuiweka nchi mikononi mwa watoto wa matajiri na mafisadi kwani hawajui na kamwe hawatajali shida tunazopata.

  Wale tuliotoka ebuyu,tandahimba,kikonga,godigodi,nkuarua,unyanyembe,msanga n.k tuungane kupigania maslahi yetu kama vile matajiri na mafisadi walivyoungana kutuhujumu.

  Ewe mtoto wa maskini nisikie usije kujuta.tusaidiane na tuache ubinafsi.

  Usisubiri kuzawadiwa haki bali simama kutetea haki yako.
  Lets fight for our destiny!

  CCm imesaliti watanzania,tusione aibu kupiga chini.hutakosea kuiacha ccm kwani ni ccm iliyoanzisha ubaguzi.

  Upuuzi ni kuendelea kutegemea ccm ikuletee maendeleo na maisha bora kitu ambacho wameshindwa kukifanya kwa miaka 50.

  Uvumilivu una mwisho,naamini sasa wale wote waliovumulia ndani ya ccm wamekata tamaa.

  Mafisadi na matajiri ni wachache mno kama tukiungana!

  Tuipe dola chadema ili tujenge heshima ya wanasiasa kwa wananchi,ninamaanisha chadema ikishindwa tunaiyondoa kama tutakavyoiondoa ccm.
  Tukijenga heshima hii maendeleo yatakuja kwani kila mwanasiasa atajua kuwa ukitaka kukaa madarakani basi unahitaji kuleta maendeleo na si vinginevyo.wananchi hawaheshimiki kwa kuwa tunarudia yale yale wakati wa uchaguzi.


  Amani,amani,amani
  Tunaoweka amani ni sisi na tukiamua kuivunja amani ni sisi pia.juzi juzi tumeshuhudia matukio yanayoweza kuvunja amani,yameletwa na kutulizwa na sisi watoto wa wakulima,wafanyakazi au wafugaji.tukipenda amani iwepo itakkuwepo tu.wagomvi na wapiganaji ni sisi hivyo tunaweza kuamua amani iwepo au itoweke,sio chama chochote!

  Kwa sasa niishie hapa.
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  meningitis Nimependa hoja yako mkuu lakini lazima tuseme kuwa kuiacha ccm na kuingia chadema si kwaajili ya kuwa viongozi labda kwa wale wenye kujaaliwa,tujoin CDM kwa kuwa itatupa nafasi ya kutengeneza fursa za ajira,elimu ya uhakika,madini na rasilimali zote zilizopo zitatunufaisha sote,haki itatendeka kila panapostahili,Kuingia CDM kwa kila mmoja kuamini kuwa alichikikosa CCM atakipata CDM i mean madaraka kunaweza kuwa na hatari mbeleni aana kila mmoja atatumia kila njia ili apate atakacho kitu ambacho sio kizuri,tujenge nchi yenye uwajibikaji kupitia tumaini hili na CDM kama taasisi will do for you whatever good you wish.

  Ili tuweze kufikia malengo haya basi sote tunatakiwa tujue tunahitaji nini na na nani atatusaidia kufikia malengo haya.Kila jema wanamabadiliko wote na Mwenyezi Mungu awabariki sana!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mkuu nashukuru kwa tahadhari yako.
  Kwa sasa chama chenye muelekeo wa kukomboa nchi hii ni chadema.lakini lazima tuwaelewe wanasiasa,kwani ni wale wale.sasa ili kuleta discipline ni lazima kama vijana na wananchi tujenge heshima kwa wanasiasa.heshima itakuja pindi wanasiasa watakaporealize kuwa wananchi tuna uwezo wa kuleta mabadiliko pale mwanasiasa anaposhindwa.for now chadema tunawategemea kuleta mabadiliko,wakishindwa tutawaondoa!hapo ndipo tutakapoweza kuheshimika mbele ya wanasiasa.

  Tuiondoe ccm,ikifa sawa...ikijipanga ni safi.lengo letu ni maendeleo anayeshindwa aondoke ndivyo wenzetu walioendelea wanavyifanya.
  Tujenge Democrats na Republican/conservative na labour yetu!
  This is the time.
   
 4. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,437
  Likes Received: 10,646
  Trophy Points: 280
  inasikitisha kuona kanuni za uongozi bora zikikiukwa huku viongozi wenye dhamana wakibaki kulalamika!

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  2015 hakuna jema la kuiokoa ccm.
   
 6. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Wise words! mkuu nimependa maelezo yako na kwa kweli hili ndilo tunahitaji kufanya na hatuhitaji kusubiri kesho isipokuwa sasa.Its me and you we can make it.Well understood mkuu!
   
 7. l

  lufungulo k JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 1,267
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Mwanzo ulianza vzr saana nikadhani unataka uanzishwe umoja wa kujikomboa kumbe unafanya kampeni kwa chama CDM kufanya kampeni ni haki yako. lkn hao CDM nao hawako mbali saana na uswahiba kuna tuhuma zilizoelekezwa kwao za chama cha mkwe, chama cha kifamilia, chama cha kidini na nikichunguza kwa juu juu tu baadhi kama zinaukweli iweje mtu na kaka yake wawe wabunge, mmoja wa kuteuliwa na mwingine kwa kura. iweje nasaba nasaba ziwe kibao aaaah wanaitana enzi za Mrema alipoona anaandamwa na udini na ukabila akazima kwa kumleta sheikh Mtopea.iko wazi toeni nafasi za ubunge wa kuteuliwa kwa kina mama wasio na nasaba vinginevyo siasa ni ajira.
   
Loading...