'Watoto wa wakubwa' wajazwa Idara ya Afya; Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K’ndoni

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Jumatano, Oktoba 31, 2012 07:07
*Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
*Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K'ndoni

Siku chache baada ya kuibuka mjadala wa kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hali kama hiyo imejitokeza tena kwenye Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, JAMHURI imebaini.

Baadhi ya wafanyakazi wa Idara hiyo, wametoa waraka wakihoji namna watoto hao wa vigogo walivyoweza kushika nyadhifa kubwa katika manispaa hizo, ilhali watumishi wengine wenye sifa, ama wakiachwa au wakipelekwa mbali na Jiji la Dar es Salaam.Katika waraka huo, ambao JAMHURI imepata nakala yake, wanatajwa baadhi ya watoto wa vigogo na nyadhifa zao kuwa ni Janeth George Kahama, ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji. Huyu anatoka katika familia ya Mzee George Kahama, mmoja wa mawaziri wawili walio hai wa kwanza katika Baraza la Kwanza la Mawaziri la Tanganyika huru. Mwingine aliye hai ni Job Lusinde.

Waraka huo pia unasema nafasi ya Mganga Mkuu Msaidizi wa Jiji la Dar es Salaam inashikwa na Dk. Hawa Rashidi Kawawa. Huyu ni mtoto wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Tanganyika, Waziri Mkuu wa Tanzania, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Hivi ni kweli watoto hawa wa wakubwa ndiyo wenye sifa tu za kushika nyadhifa hizi? Kweli, wanaweza kuwa na sifa, lakini iweje wasipelekwe Tandahimba, Kibondo au Karagwe? Kwanini Dar es Salaam tu?" Wamehoji waandishi wa waraka huo.

Wameendelea kusema kuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ni Dk. Gunini Kate Kamba. Huyu ni mtoto wa Kamba aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na ndani ya CCM. Wadhifa wa karibuni kabisa aliokuwa nao ni wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Manispaa ya Ilala, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo ni Dk. Asha Omar Mahita. Dk. Asha ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omar Mahita.

Mtoto mwingine wa kigogo ni Dk. Amani Kighoma Malima ambaye ni Mganga Mfadhiwi wa Hospitali ya Temeke. Huyu ni ndugu yake na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Dk. Amani ni mtoto wa marehemu Kighoma Malima, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini. Mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti alikuwa Waziri wa Fedha.
Aidha, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Sylvia Mamkwe, ingawa si mmoja wa watoto wa vigogo, lakini alikuwa na uhusiano wa karibu mno wa kikazi na aliyekuwa Mganga Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K'ndoni
Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa; aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo mwaka huu kutokana na shinikizo la madaktari waliogoma.

"Haya ni majina ya baadhi tu ya watoto wa vigogo katika Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na Manispaa zake. Tunauliza, iweje watoto wa wakubwa tu ndiyo washike nyadhifa hizi kwa Dar es Salaam na si mikoani?" Umehoji waraka huo.

Wiki iliyopita, JAMHURI iliandika taarifa ya kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya BoT. Hadi sasa, majina yanayovuma ya watoto hao ni ya Pamela Edward Lowassa, Filbert Tluway Sumaye, Zaria Rashidi Kawawa, Harriet Matern Lumbanga, Salama Ali Hassan Mwinyi, Rachel Muganda, Salma Omar Mahita, Justina Joseph Mungai, Kenneth Nchimbi, Blasia William Mkapa, Violet Philemon Luhanjo, Liku Kate Kamba, Thomas Mongella na Jabir Abdallah Kigoda.

Kuwapo kwa watoto wa wakubwa katika sehemu nyeti na nzuri kumeanza kuzua minong'ono ya upendeleo miongoni mwa wananchi.

Mmoja wa wananchi amehoji hali hiyo kwa kusema, "Ninachojiuliza na sipati majibu mpaka sasa ni hiki, kama imetokea coincidence (bila kutarajia) BoT ikaajiri watoto 14 wa vigogo; je, coincidence hiyo hiyo inaweza kutokea kwenye Wizara ya Elimu watoto wenye majina kama hayo hayo wakapangwa kwenda kufundisha shule za kata vijijini, ambako hakuna maji wala umeme na wakaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo bila kujali kuwa mishahara imechelewa na hawajapandishwa vyeo; na wakati huo huo wakiidai serikali sikivu malikimbizo?

"Hivi kweli binadamu wote ni sawa kwa maana ya fursa za ajira bila kuangaliana usoni, hasa BoT?"

Source Gazeti la JAMHURI
Kuhusu Mtoto wa Kawawa ameajiriwa Kama Daktari wa Jiji toka jiji ni Manispaa na amewahi kuwa Daktari wa wilaya ya Kinondoni tangu miaka ya tisini nafikiri kwa hapo alipo sasa anastahili kwani ameanza chini na anazaidi ya miaka Ishirini ya service Labda awe ni mwengine.
 
Waenga walisema mwenye nacho hatazidishiwa

Na ng'ombe wa maskini hazai akizaa basi dume, wote mnaolalamika hata kama ni wewe ungekua mtoto wa hao mnao waita vigogo kama sifa unayo utakataa hiyo nafasi kisa mzee wako ni KIGOGO
 
Watanzania bado tuna safari ndefu, uelewa bado ni mdogo sana, yaani mtu ameeleza kwa ufasaha juu ya watoto wa vigogo kupewa nafasi za upendeleo mijini, halafu vilaza wengine wasioelewa wanakurupuka kujibu na kutetea uovu. Rudini shule kwanza sio mnan'gan'gania tu kuandika pumba kwenye jamii forum
 
Watoto wa MZEE KAWAWA Wamesoma kweli, Wako kila Mahali kwenye sekta ya UCHUMI na SIASA nchini
Hadi nje ya nchi, kweli alihakikisha WANAE Wamesoma, ndicho alichowaachia....

Hata kama hakusoma sana aliiweka ELIMU MBELE; alivyokuwa anasema ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA

Wewe elimu yako mbona nayo ni ndogo,au unataka niseme?tatizo lenu ninyi Bwana mnajifanya mnajua kuwafuatilia sana wenzenu kuhusu maisha yao wakati hata ninyi maisha yenu ni machafu,halafu we kaka jiangalie utapewa za uso kumbuka tunakufahamu vizuri.

Lakini la pili,hivi kwa akili yako hiyo ndogo uliyoa nayo ulikuwa unataka baada ya hao watoto wa vigogo kusoma wakafanye kazi wapi???!!!,au ulikuwa unataka ukae nao n kuwanyanyasa kama ambavyo unawanyanyasa wale wenzako???
 
LOL... Unanifahamuje VIZURI USO WANGU? Wangapi Wamepewa za USO wakiwa Wachangiaji wa JAMII FORUMS?
HII INAONYESHA imekugonga NDANI ya KIWILIWILI chako kisicho na ROHO ila USO usiofahamika!
 
Mhhhh kwa hiyo interview zinavyoitishwa ni kutakatisha majina haya? Nakumbuka miaka ya 2000 BOT bodi iliweka pingamizi kwa watoto hawa wa vigongo walioajiriwa bila kufuata taratibu za weledi mana wengi wao hata vyeti vyao ni hitilafu na ukimwambia aandike report umeua kabisa!! Rubbish!!! Kiflichofuata ni Governor Bilal kuitisha interview ili kuwatakatisha!!! Yaani Bilal aliua kabisa ule utaratibu wa kuajiri kwa SIFA BOT na matokeo yake Seniors wanapata tabu sana kufanya kazi na hawa watoto wa vigogo!!! Ni wachache kati yao wana angalao minimum qualifications!!
 
Wewe elimu yako mbona nayo ni ndogo,au unataka niseme?tatizo lenu ninyi Bwana mnajifanya mnajua kuwafuatilia sana wenzenu kuhusu maisha yao wakati hata ninyi maisha yenu ni machafu,halafu we kaka jiangalie utapewa za uso kumbuka tunakufahamu vizuri.

Lakini la pili,hivi kwa akili yako hiyo ndogo uliyoa nayo ulikuwa unataka baada ya hao watoto wa vigogo kusoma wakafanye kazi wapi???!!!,au ulikuwa unataka ukae nao n kuwanyanyasa kama ambavyo unawanyanyasa wale wenzako???

FINALLY NIMEIPATA CISCO Trans.Matrix Nimepata IP ADDRESS yako; Sasa JIBU MASWALI kama KIONGOZI SIO USHABIKI... I do constructive criticism OF YOU
 
Ah mbona watu wanasema waislamu wanayimwa nafasi,mbona hiyo list wapo waislamu,nimesema hivyo kuwa jamani mambo ya dini hayabagui katika ajira muhimu uwe na sifa baaasi,ndugu zangununi tujitahidi kwa kula hali tuwasomeshe watoto wetu,waacha tuvae hata suruari za viraka lakini hakikisha unasomesha wanao,huo ndio utakuwa ukombozi kwa watoto wa kimasikini kulalama kila siku,maandamano hakutatufanya watoto wetu wapate ajira nzuri,huo ndio ukweli na asiyeukubali ameze wembe!
 
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Jumatano, Oktoba 31, 2012 07:07
*Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
*Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K’ndoni

Siku chache baada ya kuibuka mjadala wa kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hali kama hiyo imejitokeza tena kwenye Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, JAMHURI imebaini.

Baadhi ya wafanyakazi wa Idara hiyo, wametoa waraka wakihoji namna watoto hao wa vigogo walivyoweza kushika nyadhifa kubwa katika manispaa hizo, ilhali watumishi wengine wenye sifa, ama wakiachwa au wakipelekwa mbali na Jiji la Dar es Salaam.Katika waraka huo, ambao JAMHURI imepata nakala yake, wanatajwa baadhi ya watoto wa vigogo na nyadhifa zao kuwa ni Janeth George Kahama, ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji. Huyu anatoka katika familia ya Mzee George Kahama, mmoja wa mawaziri wawili walio hai wa kwanza katika Baraza la Kwanza la Mawaziri la Tanganyika huru. Mwingine aliye hai ni Job Lusinde.

Waraka huo pia unasema nafasi ya Mganga Mkuu Msaidizi wa Jiji la Dar es Salaam inashikwa na Dk. Hawa Rashidi Kawawa. Huyu ni mtoto wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Tanganyika, Waziri Mkuu wa Tanzania, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Hivi ni kweli watoto hawa wa wakubwa ndiyo wenye sifa tu za kushika nyadhifa hizi? Kweli, wanaweza kuwa na sifa, lakini iweje wasipelekwe Tandahimba, Kibondo au Karagwe? Kwanini Dar es Salaam tu?” Wamehoji waandishi wa waraka huo.

Wameendelea kusema kuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ni Dk. Gunini Kate Kamba. Huyu ni mtoto wa Kamba aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na ndani ya CCM. Wadhifa wa karibuni kabisa aliokuwa nao ni wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Manispaa ya Ilala, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo ni Dk. Asha Omar Mahita. Dk. Asha ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omar Mahita.

Mtoto mwingine wa kigogo ni Dk. Amani Kighoma Malima ambaye ni Mganga Mfadhiwi wa Hospitali ya Temeke. Huyu ni ndugu yake na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Dk. Amani ni mtoto wa marehemu Kighoma Malima, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini. Mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti alikuwa Waziri wa Fedha.
Aidha, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Sylvia Mamkwe, ingawa si mmoja wa watoto wa vigogo, lakini alikuwa na uhusiano wa karibu mno wa kikazi na aliyekuwa Mganga Watoto wengine wa vigogo wajazwa Idara ya Afya
Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K’ndoni
Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa; aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo mwaka huu kutokana na shinikizo la madaktari waliogoma.

“Haya ni majina ya baadhi tu ya watoto wa vigogo katika Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na Manispaa zake. Tunauliza, iweje watoto wa wakubwa tu ndiyo washike nyadhifa hizi kwa Dar es Salaam na si mikoani?” Umehoji waraka huo.

Wiki iliyopita, JAMHURI iliandika taarifa ya kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya BoT. Hadi sasa, majina yanayovuma ya watoto hao ni ya Pamela Edward Lowassa, Filbert Tluway Sumaye, Zaria Rashidi Kawawa, Harriet Matern Lumbanga, Salama Ali Hassan Mwinyi, Rachel Muganda, Salma Omar Mahita, Justina Joseph Mungai, Kenneth Nchimbi, Blasia William Mkapa, Violet Philemon Luhanjo, Liku Kate Kamba, Thomas Mongella na Jabir Abdallah Kigoda.

Kuwapo kwa watoto wa wakubwa katika sehemu nyeti na nzuri kumeanza kuzua minong’ono ya upendeleo miongoni mwa wananchi.

Mmoja wa wananchi amehoji hali hiyo kwa kusema, “Ninachojiuliza na sipati majibu mpaka sasa ni hiki, kama imetokea coincidence (bila kutarajia) BoT ikaajiri watoto 14 wa vigogo; je, coincidence hiyo hiyo inaweza kutokea kwenye Wizara ya Elimu watoto wenye majina kama hayo hayo wakapangwa kwenda kufundisha shule za kata vijijini, ambako hakuna maji wala umeme na wakaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo bila kujali kuwa mishahara imechelewa na hawajapandishwa vyeo; na wakati huo huo wakiidai serikali sikivu malikimbizo?

“Hivi kweli binadamu wote ni sawa kwa maana ya fursa za ajira bila kuangaliana usoni, hasa BoT?”

Source Gazeti la JAMHURI

jamani nauliza tuu..hivi huyu mtoto wa malima ana misimamo ya babake?Babake ai alishashaungwa mkono ni vijana mamia waliokuwa tayari kuanzisha jihad ya kupindua nchi..Asijemchoma mtu sindano ya sumu ili asiwe mpinzani wa ndungu yake akikgombea Upresidaa.Si swali tuu si lazima kujibiwa.
 
nanyie msomeshe wa kwenu afu muingie kwenye system mfanye mambo.:shut-mouth::majani7:
 
Mbona JIBU ni rahisi sana;
Ili kupunguza urasimu wa kutoa recommendation, advise na referrals za viongozi (Ambao ni baba, mama zao na ndugu zao) kwenda kutibiwa nje ya nchi
 
Kuhusu Mtoto wa Kawawa ameajiriwa Kama Daktari wa Jiji toka jiji ni Manispaa na amewahi kuwa Daktari wa wilaya ya Kinondoni tangu miaka ya tisini nafikiri kwa hapo alipo sasa anastahili kwani ameanza chini na anazaidi ya miaka Ishirini ya service Labda awe ni mwengine.
Kinachoulizwa hapa ni kwa nini wao ni mijini tu na hawaendi huko mikoani na vjijini ili kutoa huduma kwa watanzania wenzao? na hao wenye elimu kama wao waliopo mikoani na vijijini kuja kutoa huduma huku mijini?
 
Ah mbona watu wanasema waislamu wanayimwa nafasi,mbona hiyo list wapo waislamu,nimesema hivyo kuwa jamani mambo ya dini hayabagui katika ajira muhimu uwe na sifa baaasi,ndugu zangununi tujitahidi kwa kula hali tuwasomeshe watoto wetu,waacha tuvae hata suruari za viraka lakini hakikisha unasomesha wanao,huo ndio utakuwa ukombozi kwa watoto wa kimasikini kulalama kila siku,maandamano hakutatufanya watoto wetu wapate ajira nzuri,huo ndio ukweli na asiyeukubali ameze wembe!

Andika kama mtu unaefualitia kwa ukaribu mwenendo wa utoaji wa elimu unavyokwenda katia nchi hii, hao unaosema wamesoma ni watoto wa vigogo na mikopo yao University ni 100% wa masikini hata mkopo apati na wengi wanashindwa. kuna shule za kata walimu 2 au 1 shule nzima na ndiyo shule za watoto wa masikini kwa hali hiyo usitarajie miujiza kwa mtoto wa masikini kupata elimu bora, kwani elimu ya nchi hii ni KANDAMIZI kama huduma zingine.
 
nikikumbuka hata SENSA NILIKOSA najionea huruma na kuichukia nch yangu
 
soma na wewe usilete wivu wa kijinga hapa wenzio wamesoma ulitaka wafanye nini??? jaji mkuu wa znz
aliwahi kusema watu wanaomsema kumpendelea mwanawe kuwa jaji wanamwonea kijicho cauz wao hawakusomesha wakwao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom