Watoto wa wagombea urais kwa tiketi ya CCM 2005 ni wapinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa wagombea urais kwa tiketi ya CCM 2005 ni wapinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hasara, Oct 6, 2007.

 1. H

  Hasara Senior Member

  #1
  Oct 6, 2007
  Joined: Dec 29, 2006
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baada ya sereikali ya Tanzania kuwa na kiongozi mpya wa nchi familia za wangombea urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM wamejikuta kama wakimbizi na wapinzani kwenye nchi yao na wale walioko nchi za nje nitabu sana kwenda kumsalimia rais wao,

  wanamtandao wanawabagua kwa kiwango kikubwa sana na kukosa raha kwa wale tunao wafahamu,

  Mimi nina omba kuuliza hii ni haki?
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwani lazima wakamsalimie? Mbona wengine hatuenda kumsalimia, je tumekosa nini?

  Ubabaishaji tu na usanii, kwenda kuongea na rais na kupata picha za kutamba nazo kwa washikaji.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Siyo haki hata kidogo...

  Lakini waambie wasikonde bure, matatizo kama hayo yanawakuta Watanzania asilimia kubwa tu hapa nchini, wengine hata kuwaona wabunge wao tu ni vigumu kwani katika familia zao kuna watu walio jitokeza kuwania ukada chini ya vya upinzani wakashindwa na wenye bahati kushinda... hivyo familia zao zinakuwa doomed regardless, so to boot!

  Hasara, pia waambie wajiunge na JamboForums kwani naamini upweke wa kubaguliwa utapungua! Pia waambie familia zao zizidi na mlengo huo huo badala ya kusalim amri, zikaze uzi ili wazazi wao au ndugu zao wajiandae kugombea tena urais kwenye chaguzi zijazo.
  Sina mengi zaidi ya haya. Ahsante.


  SteveD.
   
 4. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Haina haja ya kuonana nao...........kinacho matter ni wajibu wao wa kazi!!kama ni mzuri basi, kuwaona wa nini kwani wao wamekuwa vimungu mtu...? hao jamaaz wanalilia "photo op" na prez ili wazitume kwa michuzi,sijui hata maana yake ni nini? aaaaaaaaaaagh yuk!!!!!!!!.
   
 5. H

  Hasara Senior Member

  #5
  Oct 6, 2007
  Joined: Dec 29, 2006
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima mkuu baada ya uchanguzi kwisha zimeanza chuki binafsi nyingi kati ya wagombe na familia zao zikiwemo za Wabunge, Madiwani, Urais, na nafasi nyingine za kiserekali basi waliyoko madarakani kwa sasa inakuwa vingimu kuwasikiliza watoto hao zaidi wanamtandao,

  MKUU HANA SHIDA-ruksa kumuona- NI WASAIDIZI WAKE KUMPELEKA MTOTO WA ALIYE KUWA MGOMBEA HAWATAKI, wasaidizi wakimuona mtoto wa haina hiyo basi wanaanza kuulizana ametumwa au nini, majibu atakayo pata siyo mazuri lakini yanarithisha ili uondoke,
  Sisi tuwasaidieje hawa watoto ili sauti zao zisikike?

  imekuwa vingu hata kupata mialiko ya kichama na serekali wanajiuliza hili jina mkuu akiliona itakuwa basi wanaacha, kumualika mtu kutoka katika hizo familia .
  jamani hebu tulijadili hili kwa kina kwasababu ni watanzania na wana haki na nchi yao na viongozi wao aliyeshinda ni kiongozi wa wote waliyo mchangua na wale ambao hawakumpa kura zao.

  kama unamjua mtoto au familia kama hii tufahamishe mara moja hapa ili tuweza kuwasaidia.

  asante
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nimekusikia pia Ndg. Hasara,
  Ndiyo maana nikasema kama wapo ni bora wajiunge na forum hii, nina imani wote wanajua kusoma na kuandika wote, hivyo kama unayoyasema yamewakuta basi hawana budi wajiunge hapa walau kwa majina ya 'ki-forum', maana majina halisia yanaweza kuleta matatizo ya aina yake tena.

  Ahsante kwa kuuliza kama wapo ninaowafahamu; jibu lake kwa kweli ni kuwa wapo wengi tu, lakini uzuri wote ninaowafahamu hawana matatizo ya kuelemea au kunyanyasika na vimbwega vya wakubwa, ni watu mahili tu wanaofanya mambo yao kutokana na merits zao.

  Hata hivyo nawaonea pole hao wanaojisikia wanyonge na wenye kunyanyasika kwa kukosa haya na yale kutokana tu na majina yao. Ni usia wangu tu tena nitakao urudia, WASIFEDHEHEKE BURE, WAJIDHATITI WAO NA FAMILIA ZAO KWA AJILI YA CHAGUZI ZIJAZO.

  Mtu kama hakukaribishi ni bora kuachana naye, kujibaraguza na kujipendekeza kutazaa matunda mabovu, tena miye naona wanabahati kinamna fulani, maana walau wanafahamu kuwa kiongozi fulani au viongozi fulani hivi wanatuchukia sisi na mama/baba yetu... hivyo they can really prove the other part wrong and do things to their advantage if they do so wish, since they'll fully be equipped with the awareness of their surroundings. You know the adage - knowledge is power! Knowing that somebody despises you is power against the same person in my opinion.

  SteveD.
   
 7. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ningeshauri tujaribu kudiscuss mambo muhimu ya kulisogeza taifa mbele, na sio mambo ya ccm vs wapinzani ! nimerudi !
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Vizuri sana umerudi!

  Kuna thread hii HAPA , labda uicheck na unaweza ukajibu waliokuwa wanakutafuta hapo awali.

  SteveD.
   
 9. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ok, lakini waliniban !
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mkuu tunakupongeza kwa kurudi, na walaaniwe waliokuban, ati umetumia haki yako ya kidemokrasia kueleza hisia zako.
   
 11. l

  leedar New Member

  #11
  Oct 6, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Me naona hakuna umuhimu wowote wa kumuona Rais kama kuna jambo muhimu utapita ngazi na utaratibu uloowekwa vinginevyo wasaidi wake wapo utawaona ama kwa suala la kumsalimia tu ah sioni kuna big issue, hata hivyo mbona kuna waliogombea na wamo ktk uwaziri? tuwache chuki binafsi, au mlikua family friend?
   
 12. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hao watoto nao si watanzania kama sisi?kwa nini wao wawe na nafasi ya kumwona rais zaidi ya wengine?

  Kama wamezoea kupendelewa naona bora waachane na hizo tabia ila watumie nguvu zao na akili zao kama wanazo kwa ajili ya kujitegemea na sio kulialia kila siku.
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  What?! :(

  Mtu wa Pwani vipi tena, unataka JF management ilaaniwe na hivyo kutoweka hewani kutokana na Kada tu kufungiwa kwa siku moja?! Naomba ueleze tafadhali, je unataka walio m-ban Kada walaaniwe na kuwa vipi?! Maana wanao mban mtu hapa ni management ya JF, Mbona itasikitisha sana kuona kuwa JF inaanza kulaaniwa kutokana na member kukiuka sheria mojawapo na hivyo kuwa banned.

  SteveD.
   
Loading...