Watoto wa vigogo wasio na sifa Mizani kukiona

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
Watoto wa vigogo wasio na sifa Mizani kukiona Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) imekiri kuajiriwa baadhi ya watoto wa vigogo wasio na sifa katika vituo vya mizani na kuahidi kulishughulikia suala hilo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango, wakati akijibu hoja iliyotolewa na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Vicent Nyerere ambapo walikutana na Tanroads kwa ajili ya kukagua matumizi ya fedha zao pamoja na ufanisi. Nyerere alidai kuwa hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alieleza kuna baadhi ya watoto wa vigogo wasio na sifa wameajiriwa katika vituo vya mizani ambapo alitaka kupatiwa ufafanuzi juu ya suala hilo. Akijibu hoja hiyo, Balozi Mrango alisema waziri akizungumza jambo linakuwepo na ni kauli ya serikali na kueleza kuwa wanafanya utaratibu wa kuajiri upya na kila mmoja ataajiriwa kwa sifa zinazotakiwa. Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale, alisema tayari amepeleka muongozo kwa mameneja wa mkoa kuajiri kwa kufuata vigezo vinavyotakiwa. Alisema utaratibu huo utafuatwa kwa vigezo vinavyotakiwa bila ya kuangalia watoto wa vigogo na kwamba suala hilo tayari limeshaanza kufanyiwa kazi ili kuwaondoa wasio na sifa. Mhandisi Mfugale alisema ishu sio kuwaondoa watoto wa vigogo ni kuboresha hali ya utendaji katika vituo vya mizani na kutokomeza suala la rushwa. Hata hivyo alisema nafasi za kazi zimeshatangazwa na kwamba wataangalia vigezo na watakaomba wametakiwa kuwa na ushindani ili kuwepo na utendaji mzuri wa kazi. Alisema mpaka sasa haelewi idadi wa hao watoto wa vigogo walioajiriwa katika vituo vya mizani. Mhandisi Mfugale alisema mara nyingi watoto wa vigogo wamekuwa wakipatiwa vimemo na kuviwasilisha kwa mameneja wa mkoa, hivyo kwa sasa suala hilo halitaangaliwa ajira itatolewa kwa yule mwenye vigezo
 
Maneno 2 hayo ushayazoea,wala vilaza wa BOT wamefanywa nn mpaka leo?
 
Tulikataa ukoloni wa kizungu sasa nimeambulia ukoloni mambo leo na ufalme wakudumu!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom