Watoto wa vigogo waongoza kuchakachua ripoti vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa vigogo waongoza kuchakachua ripoti vyuo vikuu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kilimasera, Apr 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SUALA la uchakachuaji mitihani limeingia katika sura mpya baada ya kuibuka kampuni zinazoendesha biashara ya kuwaandikia ripoti za utafiti, wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu katika vyuo vikuu.

  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa kampuni hizo hutengeneza kazi hizo, ambazo baadaye huziandika ili zionekane zimefanywa na mwanafunzi husika baada ya kukamilisha malipo.

  Wanafunzi hao ni wale wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini katika ngazi ya shahada, shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu (PhD).

  Wanafunzi wengi kabla ya kukamilisha mafunzo katika ngazi husika kwa kawaida hutakiwa kufanya utafiti na baadaye kuandika ripoti kuhusu taaluma aliyosomea, lakini kwa kuona ugumu wa kazi hiyo, wenye uwezo hutumia kampuni hizo ili kufanyiwa kazi hiyo tena kwa ustadi wa hali ya juu.

  Uchunguzi unaonyesha kuwa wanafunzi wenye tabia hiyo wengi wao ni watoto wa vigogo ambao hutumia ipasavyo uwezo wa kifedha wa wazazi au baadhi ya wale wanaosoma huku wakiwa kazini.

  Wanafunzi hao inaelezwa hutoa kati ya Sh2 milioni hadi saba ili kupata taarifa za tafiti wanazozihitaji zikiwa tayari zimetengenezwa katika mfumo wa kitabu.

  Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wamekiri kuwapo kwa vitendo hivyo wakieleza kuwa walivibaini baada ya kuwauliza maswali wanafunzi kuhusu tafiti walizoziwasilisha, lakini wakashindwa kujitetea.

  "Mmoja aliandika tafiti nzuri. Nikawa na wasiwasi.
   
 2. matwi

  matwi JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili ni tatizo kubwa na sio tu kwa watoto wa vigogo hata wengine wanatumia miili yao kama rushwa kuandikiwa riport tabu inakuja pale wanapoambiwa wafanye presentation.unakuta hata mtu hajui eneo alilifanyia hiyop research.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaa kweli nchi sasa inaandaa vilaza kwanini watu wasijitume tu hv kwa mtindo huu tutaendelea kweli
   
 4. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33
  nakubaliana na wewe tena maswali katika presentation mengi yanataka ku prove kama hiyo research umeifanya wewe mwenyewe au vinginevyo (HASA RESEARCH ZA UNDERGRADUATE), ila wanavyochemka aibu... ukitaka kuwagundua mapema fanya uchunguzi karibu na siku ya presentatation utakuta mtu anakomaa kuisoma repoti utafikiri ni desa!!! kumbe hajui kilichomo kwenye hiyo repoti

  SHAME ON THEM...
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Tuanze kwa kuwataja kwanza watoto wa vigogo alafu tuenddlee kuchangia.....................hivi wale wa bot waliishia wapi?
   
 6. L

  Leliro Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hali ndo hii basi tumekwisha! unategemea mtu kama huyu anaweza kuwa critical kwa jambo linalohusu maendeleo ya nchi yake? sidhani kwani huyu atakuwa mstari wa mbele kujilimbikizia mali na kuiacha Tanzania ikiwayawaya. kweli tumekwisha, ukombozi haupo hata kidogo!
   
 7. N

  Newvision JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani Si lazima wawe watoto wa vigogo tu wote wanaofanya hivyo ni sawa tu-VIHIYO++++++
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Bongo bongo bongooooooo!!
   
 9. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ...for a great thinker THIS IS AN OPPORTUNITY! if we have too many fools at mid-levels, then the smart few will ultimately PROSPER. Just a matter of staying awake. Usijali sana ukimwona kobe juu ya mti, jipange.
   
 10. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nasikia IFM wanaongoza
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yalimalizwa kimyakimya ila mpaka sasa bado wanabebana pale nadhani hali hii itakwisha labda mpaka chama cha upinzani kichukue madaraka!wewe huoni tu hali ilivyo sasa hv kila sehemu CCM wanachakachua kisa watoto wao ndio warithi nafasi hizo!wakati utafika tu hata kama itachukua muda mbona kenya waliweza na maka sasa haoo wanapiga bao!
   
 12. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #12
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni kubwa kuliko linavyosemwa
   
 13. B

  BARRY JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Kazi ipo, kama ni uzembe hiyo hatari.
   
 14. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama mtu kuanzia anaanza 1st yr amezoea kumeza unategemea mwisho afanye nini ili apete gamba? ARDHI kidogo wanjitahidi maana wao kuanzia semister ya kwanza hadi ya mwisho wana project hii inawasaidia wakati wa dissertation
   
 15. i411

  i411 JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  I will do anything for Grade 'A'
   
 16. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  ril??...?..?
   
Loading...