Watoto wa vigogo Tanroads wafukuzwa kwa kughushi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa vigogo Tanroads wafukuzwa kwa kughushi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 21, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  SERIKALI imewafukuza kazi watoto wa vigogo waliopata ajira bila ya kufuata taratibu za kisheria katika mizani inayosimamiwa na Wakala wa Ujenzi wa Barabara(Tanroads).

  Hata hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kudai kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo wamepata ajira kinyume na taratibu.

  Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuu (PAC), Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale alisema watoto hao waliajiriwa kimakosa.
  Alisema watoto hao wametambuliwa na kwamba baadhi yao tayari wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi huku wengine vyeti vyao vikiendelea kukaguliwa.

  “Kuna baadhi ya wafanyakazi walikuwa wamepata ajira kinyume na taratibu, hii inatokana na kupata ajira kwa kujuana lakini suala hili tayari tumelifanyia kazi na baadhi yao tumewafukuza,” alisema Mhandisi Mfugale.

  Alisema kutokana na hali hiyo, wataendelea kuhakiki vyeti vya wafanyakazi wote na kuhakikisha kuwa, wanatangaza ajira upya ili wenye vigezo waweze kupitishwa na wasiokuwa navyo waondolewe.

  Alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, ajira zinazotolewa katika idara hiyo ni za muda mfupi, ili kuondoa mianya ya ajira za kujuana.

  Aliwataka mameneja wote wa mikoa kufuata taratibu za kisheria katika kutoa ajira kwa wafanyakazi wapya.
   
 2. t

  tz03 Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha kushangaza,wenye vyeti na elimu iliyobobea wanaambiwa "over qualified" halafu mnachukua watu wa barabarani then mnalalamika ooh wamegushi,so what do u want?????
   
 3. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Safi sana,

  Yale mambo ya zamani mtoto wa mkubwa kupewa kazi na tenda hakuna tena, ukifanya hivyo wewe ulietoa ajira na muajiriwa wote mnafukuzwa kazi, safi sana serikali naomba muwapekue na wengine wengi
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,027
  Likes Received: 37,780
  Trophy Points: 280
  Baadae utasikia kimya kama hakuna kosa lililotokea.
   
 5. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Wekeni majina yao
   
 6. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Waweke majina hadharani kuthibitisha hilo isijekuwa changa la macho!
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Bila hili suala kuvuja Mfugale angefungua kinywa?
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kuwafukuza tu baada ya makosa haya makubwa kunatosha au kwa kuwa ni watoto wa wakubwa ? Hakuna jinai hapo jamani ?
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  huyu mkurugenzi naona anaongea siasa ataje majina huu si wakati wa kuficha kitu bali ni kutoa mpaka hata na uhuni walioutumia kupata nafasi zao
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  Hawa watoto wa Vigogo majina yao ni marufuku kuyataja hadharani!? Au ndio mwendo ule ule wa kulindana? SMH!
   
 11. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Tunaomba majina yao (bila kusahau ubin)
  pamoja na picha ikiwezekana
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Kugushi doccument yoyote ile ni kosa la jinai, hayo majina yangetajwa halafu ili kulinda heshima ya taaluma wafikishwe mahakamani kwa kosa la kughushi!
   
 13. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wamewaonea tu. katika baraza la mawaziri kuna watu kibao kama Nchimbi, Lukuvi wameghushi elimu zao. Kwa nini wasianze na hawa wakubwa ili iwe funzo kwa wadogo?
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hapa kuna sanaa tu
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  Nami naona hivyo hivyo BT, yaani badala ya kuwataja kwa majina wanaamua kuficha majina yao na kutumia "Watoto wa Vigogo" bado wanakingiana vifua kwa kiwango cha kutisha. Huyu Mfugale akishinikizwa kuyaanika majina hayo hadharani kamwe hataweza kufanya hivyo.

   
 16. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mkuu unoge!! unadhani wanamaanisha? naamini kabisa ni maneno yalitolewwa tu mbele ya hiyo kamati but in actual practice tusitegeme lolote
   
 17. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndimnofu mkuu, najua hawa wezi kuwafukuza wote lakini nadhani wataondoa baadhi ya madudu, siku hizi yale mambo ya kubebana yanapigwa vita sana kwa sababu kuna vyama vingi kwa sababu usipomtaja mimi nitamtaja kwa hiyo serikali inakuwa under presure na isingependa kuchafuliwa jina kwa sababu ya manufaa ya watu wachache
   
 18. P

  Pampuka Senior Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kosa kubwa walilofanya hawa ni kughushi ambalo ni kosa la jinai, tulitaraji kuambiwa wanapelekwa kwenye vyombo vya sheria pamoja na walioshirikiana nao kula njama hii, na huenda kukawa hata na kosa rushwa hapa. lakini nafiri hii CCM ya sasa ni makaburu, majitu yalityojaa ubaguzi, Mwal. aliwahi kusema kuwa hatuwachukia wazungu kwa sababu ya rangi zao bali kwa sababu ya ubaguzi wao ndio maana tukawaita makaburu. Hivyo CCM in Chama Cha Makaburu kwa kuwa wanabagua watu kwenye siasa na kuingiza wanafamilia peke yao kama wafalme, wanatubagua kwenye ajira, huduma za Afya, makazi, maji, na rasilimali zingine za Taifa. Ni makaburu tu................!!
   
 19. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  sakata la watoto wa vigogo bot waliofikishwa mahakamani kwa kughushi liliishaje?
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Changa la macho hilo!

   
Loading...