Watoto wa vigogo na upendeleo wa ajira nyeti serikalini

kuna wataalam wanaiondoa hoja taaratib kuipeleka kusiko,
hapa tunajadili watoto wa wakubwa na wengine wanajadili upedeshee ktk JF hahahaha. enewei ntashangaa kama hatutamjadili pia ridhwani ambaye anafukuzia mwaka 2025 kumrithi baba yake. kwa hiyo mie nitakosa nafasi ya ukuu wa kaya kwa kuwa mdingi wangu siyo kizito???
 
kuna wataalam wanaiondoa hoja taaratib kuipeleka kusiko,
hapa tunajadili watoto wa wakubwa na wengine wanajadili upedeshee ktk JF hahahaha. enewei ntashangaa kama hatutamjadili pia ridhwani ambaye anafukuzia mwaka 2025 kumrithi baba yake. kwa hiyo mie nitakosa nafasi ya ukuu wa kaya kwa kuwa mdingi wangu siyo kizito???

kwani huyo mtoto sio raia wa tanzani ? kama atakuwa ametimiza vigezo vyote vya kugombea urais, kuna tatizo gani ? au ndo mnamuandalia skendo mapema ?mhm, ntoke mie !

hii thread inaongozwa na maneno ya uswahilini, vijiweni! FACTS HAMNA ! hehehee, natoka zangu mie !
 
kwani huyo mtoto sio raia wa tanzani ? kama atakuwa ametimiza vigezo vyote vya kugombea urais, kuna tatizo gani ? au ndo mnamuandalia skendo mapema ?mhm, ntoke mie !

hii thread inaongozwa na maneno ya uswahilini, vijiweni! FACTS HAMNA ! hehehee, natoka zangu mie !

...ukweli huuuma always
 
Ina nikumbusha kipindi cha "mikingamo" ktk radio Tanzania enzi zileeeeeeeee nikiwa katoto wakti wa ulanguzi!!!. Tuhuma za kweli, uongo, majungu, chuki, uzandiki, ufitinishi, kupakaziana, na kadhalika, ili mradi ilikuwa tafrani!!. Tena hiyo na kadhalika ndio mbaya zaidi, halafu kizunguzungu ni pale tuhuma zote zinapo onekana kweli.......hivi kipindi cha mikingamo kilifanikiwa kweli???. Ufumbuzi wa kweli na wakudumu ktk matatizo haya ndio dili na sio kuleta janja ya kwapa kunuka bila kidonda!!.
 
...ukweli huuuma always

kwani uongo ? huyo dogo kugombea kwake hakunihusu, lakini saa nyignine tuondoeni chuki na upuuzi usiokuwa na maana yoyote, KAMA DOGO ANA VIGEZO VYOTE KWA NINI ASIGOMBEE KAMA MTU MWINGINE TU ? hata wewe unaweza kugombea urais achilia 2025 huko mbali kabisa, yaani 2010 mzee ! panga nyundo zako uende ukagombee, nitakupigia wewe msanii kura !
 
Nadhani hapa ishu kubwa siyo kuwa ni kwa nini hao wanaoitwa watoto wa wakubwa wanapata hizo advantages katika mazingira ya nchi tunayojenga usawa na haki. Kwa mfano kama kuna ushindani wa uwazi na halafu wao wakaonekana videdea, nadhani mjadala wa namna hiyo utakuwa ni udaku na awanachi wengi hawatauelewa. Ila kuna haja ya kuuliza endapo watu hawa wanapata unfair advantage hizo bile ushindani au wakati mwingine kwa kuondolewa ushindani halali kwa misingi isiyokuwa ya haki.

Mambo madogo madogo kama haya ndiyo yanayolipua moto katika jamii inapoonekana kuwa wanaoohoji uhalali wa baadhi ya raia kupendelewa kutokana na koo zao halafu walalamikaji wakawa-igbored. Nchi nyingi za kiafrika zenye magomvi ya wenyewe kwa wenyewa hutokana na koo chache kupendelewa katika nafasi mbalimbali za umma: anzia na jirani zetu Rwanda, Burundi, Liberia n.k.

Kwa mfano endapo tenda ya kujenga benki kuu ya zanzibar ilitolewa hadharani ikashindaniwa kihalali ikaonekana kwamba Bwana Apson ni mshindi halai basi hakuna neno. Ila kama tenda hiyo ilitolewa kimya kimya na kupewa kijana kuwa hiyo ndiyo kula yake, basi hapo kuna haja ya kuhoji na sidhnai kama ni "wivu." Jengo kama la benki kuu linatakiwa lijengwa kwa viwango funali ambavyo hatuwezi kutumia pesa ya watu wetu bila ya uhakika kama viwango hivyo tutavipata.
 
kuna wataalam wanaiondoa hoja taaratib kuipeleka kusiko,
hapa tunajadili watoto wa wakubwa na wengine wanajadili upedeshee ktk JF hahahaha. enewei ntashangaa kama hatutamjadili pia ridhwani ambaye anafukuzia mwaka 2025 kumrithi baba yake. kwa hiyo mie nitakosa nafasi ya ukuu wa kaya kwa kuwa mdingi wangu siyo kizito???

Sasa hivi Baba ameshika tunaona mambo yanavyokwenda, akishika mtoto huenda nchi ikazama kabisa, naona kweli trend sasa hivi inaonesha kama Tanzania ni Kingdom, kurithishana uongozi, na kueana kazi kutokana na majina. Why Don't we call ourselves United Kingdom of Tanzania?
 
wewe utamweza kada; wakati mwingine huwa anaandika ili watu wajue yupo!


Nilishasema huyu jamaaa na midevu yake ni mtu mwenye sifa za kitoto sana.Sijui ndio kudumaa akili huko.Utoto wake na kutokuwa kwake mstaarabu apeleke hizo tabia Darhotwire.


Nilishamwabia hapa hatulei watoto
 
jamani naona kule kwenye thread ya Mama Mongella kula rushwa kule AU imeingiliwa na habari ya tuhuma za namna watoto wa MALECELA walivyojazana katika idara mbali mbali za serikali na hasa wizara ya Mambo ya Nje

Na kusema kweli ES amekuwa very effective katika rebuttal zake na inaonekana kuwa hakuna mwenye enough counterargument kwenye hili. In short ES amekuwa kama unguided missile huku akisaidiwa na cyber bullying tactics

Nashauri bora tuiache ile thread iendelee na namna serikali itakavyo-deal vilivyo na huyo Mama MLA RUSHWA aka MAMA MONGELLA halafu ile ya allegations za watoto wa MALECELA "ku-colonise" FOREIGN tujadili hapa
 
habari ya tuhuma za namna watoto wa MALECELA walivyojazana katika idara mbali mbali za serikali na hasa wizara ya Mambo ya Nje

Mkuu Theory,

Heshima mbele mkuu, mbona unajaribu kuzusha yasiyozushika? Haya maneno umeyatoa wapi mkuu? Thread ipi unayoiongelea hapa inayosema Malecela ana watoto wengi Foreign?

Foreign kuna mtoto mmoja wa Malecela, ambaye ni mwanasheria aliyeko UN (Diplomat), na kuna mtoto wa marehemu makamu wa mwenyekiti wa Chadema (Local Staff), ambaye ni mke wa mtoto wa Malecela, sasa hao watoto wengi wa Malecela kuwa Foreign umeyatoa wapi?

Vipi mkuu una tatizo lipi maana ninakuona unanitafuta for a while sasa na hii ishu vipi mkuu, mbona unaheshimika sana humu kuzusha hizi nyepesi nyepesi? Yaaani mnamchukia Malecela hata mtoto wake akiwa mmoja mnasema ni wengi?

Ningekuelewa ukisema Malecela, ana watoto wengi serikalini, ambao so far ni watatu tu ningeeelewa, lakini foreign kuna mtoto wake mmoja tu sasa kuna sheria inayosema mtoto wa kiongozi asifanye kazi serikalini? Mkuu jina lako hapa forum halifanani na huu uzushi vipi kuna nini mkuu?

Mke wa mtoto wa Malecela, ambaye ni Local Staff aliajiriwa kazi ubalozi wetu Brussells mwaka 1990 baada ya kumaliza shule ya lugha mbali mbali ki-Belgiji kikiwemo, wakati baba yake akiwa makamu mwenyekiti wa Chadema, na baba yake mdogo Mwasakafyuka akiwa balozi Lagos, akaolewa na mtoto wa Malecela mwaka 1995 na kuhamia kuishi kikazi NY sasa does that makes her mtoto wa Malecela?

Jamani I am lost au kuna something sielewi hapa?

In short ES amekuwa kama unguided missile huku akisaidiwa na cyber bullying tactics

Mkuu Theory ni kweli wewe ndio umeandika hii quote? Vipi ukinifafanulia nikuelewe exactly unasema nini mkuu maana so far sikuelewi? Bullying tactics? Zipi hizo na mimi ninaweka facts tupu hakuna mikwaruzo mkuu, ila kuniiita unguided missle ni matusi sikutegemea hata siku moja kutoka kwako, ninaaamini kuna sababu mkuu maaana this is not you mkuu nifahamishe kuna nini, maana lazima hapa kuna bigger ishu than mtoto mmoja wa Malecela kuwa wengi na ku-Colonize foreign, ila mkuu sikutegemea hata siku moja wewe kuandika this low , lakini mimi kama kawaida huwa sio mchokozi na wala siogopi hoja wala vitisho kwa hiyo mkuu karibu sasa utimize nia yako mkuu maana najua kuna kitu unahitaji kukitoa hiii imechukuliwa kama chambo, bring it on mkuu!
 
FMES

Mkome nyani giladi kweupe kabla ya kuingia giza maana huko Tanzania nimeambiwa miti yote inateleza tu. Teh Teh teh ...........
 
January na Mwamvita wote wameajiriwa ikulu kama wasaidizi wa rais? Alafu hii NPS sc ni ya mama yake Kinje aliipata vipi kutoka kwa yule mkury sijui. Kuna baadhi ya watoto wa wakubwa wamehustle na wanaqualifications sasa wasiombe kazi kisa jina la ukoo?inabidi tuangalie asilimia ngapi imequalify na ngapi wamepewa kwa deal.
 
Quote;-

Kuna baadhi ya watoto wa wakubwa wamehustle na wanaqualifications sasa wasiombe kazi kisa jina la ukoo?


Simple and very clear!
 
Mambo mawili yametokea mwezi huu:

Kwanza JF iliwaexpose watoto wawakubwa ambao kuna habari kuwa wamepewa kazi pale BOT kwa upendeleo au kutokana na nafasi za kisiasa za wazazi wao

Pili huu mjadala unaoendelea kuhusu mtoto wa karume wakili FATMA humu ndani

Mfano Kinje ambaye ni mtoto wa Kingunge tunaambiwa kuwa procurement yote ya JWTZ kakamata yeye japo si mwajiriwa wa JWTZ

Mtoto wa kanali APSON ambaye alikuwa ni mkuu wa usalama wa Taifa ndiye aliyepewa tenda ya kuweka security systems Ikulu Dar, na sasa hivi amepewa tenda ya kujenga BENKU KUU ZANZIBAR

Watoto wa MKAPA nao nikianza kuandika mambo yao basi itachukua si chini ya ma saa 8

Mtoto wa kigogo mwingine ndiye amepewa tenda ya PARKING SYSTEMS DAR ES SALAAM

Mwingine alipewa tenda ya mkusanyo Saba saba

the list is endless....
Sasa kuna mengi yanasemwa na mengine watu wanaongeza chumvi lakini ukweli ni kuwa kuna RESENTMENT kubwa tuu dhidi ya wakubwa na watoto wao

Swali je tunaruhusiwa kuanzisha mjadala JAMBOFORUMS wa kuwajadili hawa watoto wakubwa humu kwenye siasa bila malalamiko kuwa hapa si mahala pake?

Nauliza kwa sababu hakuna haja ya kuanzisha mjadala ambao mtu unajua fika kuwa utaondolewa ili kuwa protect hawa watoto

Je wana bodi mnasemaje?

Mwenye tenda ya Parking hapa Dar ni mke wa Kingunge,na mwanawe(Kinje) yumo kwenye kampuni kama director.Pia sina uhakika kama Kinje kuna wakati alikuwa na kazi ya kusupply maduka ya jeshi na bidhaa.Lakini hili nakumbuka ilikuwa ni dili ya marehemu Ipi Malecela akiwa na jamaa mmoja anaitwa Albert Marwa,hii ilikuwa ni zamani.Watoto wa Mkapa wa kumuongelea labda ni mmoja tu,Nicholas,na sidhani kama kuna mengi kiasi hicho ya kuandika juu yake zaidi ya Kiwira ambayo kwa kweli ni well documented.
 
Nauliza kwa sababu hakuna haja ya kuanzisha mjadala ambao mtu unajua fika kuwa utaondolewa ili kuwa protect hawa watoto

Sasa hoja hii ina zaidi ya mwezi, mwanzishaji kimyaa. Anasubiri ijifie? Anasubiri iingie kwenye archive kisha aseme "Imefutwa kabisa"? Ni bora uendelee, none is moving this thread to anywhere. Be fair, kuandika kuwa utaamishwa kuwa-protect watoto wa wakubwa ni kutukosea tu moderators. Ni vema uendeleze mjadala. Mchangiaji akitukana basi ndipo hoja yake hufutwa, ama mwanzishaji akibadili mtizamo na kushauri hoja ifungwe itafungwa. Ama vinginevyo hoja ikijaa udaku bila data zaidi na kuwa mada ya salaam n.k basi hakika itahamishiwa kuleee...

Lete data, hakuna asiyeongeleka. Ila tuwe fair katika hoja. Kila mtanzania ana haki ya kuheshimiwa utu wake. Haijalishi kazaliwa na Mkapa, Nyerere, Malecela, Mbowe n.k. Ili mradi tusiwatukane na kuwachafulia majina kwa makusudi. Ukitoa hoja tarajia kupingwa ama kuungwa mkono, ni two way traffic.

Karibu GT :)
 
Ndugu zanguni wana jf katika pita pita yangu ya hapa na pale nimefanikiwa kupata majina ya baadhi ya watoto wa wakubwa manaoitafuna bot yetu kwa maslahi ya watoto wao.

PAMELLA LOWASSA
FILBERT SUMAYE
ZALIA KAWAWA
HARIETH LUMBANGA
SALAMA ALI MWINYI
RACHEL MUGANDA
SLVIA OMAR MAHITA
JUSTINA MUNGAI
KENNETH JOHN NCHIMBI
LIKU IRENE KATTE KAMBA
THOMAS MONGELLA
JABIR ABDALLAH KIGODA
VIOLETH PHILLEMON LUHANJO
KENNEDH JOHN NCHIMBI
BLASSIUS WILLIAM MKAPA

Hawa ni ambao nimefanikiwa kuwapata, sasa siwalaumu wao kuwepo katika nafasi hizo ,japokuwa nafasi za wazazi wao zimetumika kwa asilimia 100,cha kujiuliza wahusika hawa wana ujuzi gani ama uzoefu gani kuwepo katika idara za taasisi nyeti ya nchi.Ambae ninamjua ni mbabaishaji ni huyo jabir kigoda

Na kilichoniuma mimi ni baada ya kuona mshikaji wangu wa karibu ambaye yeye kamaliza masters yake ya uchumi hapa international university of australia kakataliwa bot,sababu hana uzoefu wa muda mrefu,JE HAWA WATOTO WA WAKUBWA WANA ELIMU GANI NAUZOEFU GANI WA KUTOSHA ILI KUWA WATENDAJI KATIKA TAASISI HIYO NYETI?
 
Thanks bro, lakini hii ilishaletwa hapa zamani sana na ikawa discussed, tafuta unaweza kuipata.
 
4GSpEk860844-02.jpg

c6NRi.537538-02.jpg


430710154.img.jpg

Nimefanikiwa kupata picha za huyo mtoto wa kigoda, kiufupi huyu bwana ameishia o level tu,na kwa wale wanaomfahamu vizuri mtihani wake wa form 4 alifanyia hospitalini bada ya kuvunjika mkono,alifanyia akiwa MOI, bada ya hapo akawepo tu home akipata goodtime gafla tukashangaa keshaingizwa BOT
displayPhotoUser.do
.Mwenye data za wengine atumwagie ili tuwachambue hasa hasa uwezo wao wa kiutendaji

ANGALIENI WATOTO HAO WA KUBWA WANAVYOKULA BATA MJINI HAPA KWA KODI ZETU.
 
Jamani samahanini nimejaribu kuzitaweka ila nimeshindwa ila zinapatikana katika link zifuatazo chini,

http://hi5.com/friend/photos/displayPhotoUser.do?photoId=542085005&ownerId=102274855

ila kama unataka kupata picha nyingine copy hiyo link yote kama ilivyo ila kwenye hiyo no 542085005 ibadilishe weka 480710154 nyingine 671396184 na ya mwisho ni 1003335265, ila maneno mengine yote yacopy kama yalivyo ila kwenye izo no ndo badilisha
 
Back
Top Bottom