Watoto wa Vigogo/Mafisadi wakianza kutekwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Kutoka "Uwazi"

Habari hii niliisikia siku chache zilizopita. Naona bado iko hewani:

Mtandao mkubwa wa majambazi wanaotumia mbinu mpya za utekaji nyara uliopachikwa jina la Black Mafia umeibuka katika Jiji la Dar es Salaam na kuzusha hofu kubwa ya usalama wa raia na watoto wao.

Kujulikana kwa mtandao huo kumetokana na tukio la hivi karibuni la utekaji nyara wa mtoto mwenye umri wa miaka miwili, Fardosa Mohamed Othumani mkazi wa Mtoni Sabasaba lililofanywa na kikundi hicho cha utekaji nyara.
Akielezea kwa masharti ya kutotajwa jina lake, mmoja wa viongozi wa serikali ya Mtaa uliotokea tukio hilo, Kata ya Wailes, Chang’ombe alisema kuwa majambazi hao wana kikundi kikubwa kinachosaidia kufanikisha kazi zao.

‘Watekaji hao wana mtandao mkubwa kwani mzee Mohamed Shariff, baba wa mtoto aliyetekwa, kila alilokuwa akilifanya ili kumnasua mtoto wake lilikuwa likiwafikia majambazi na kisha baba huyo kutaarifiwa kwa njia ya simu, alishangaa kuulizwa kwa nini anakwenda na polisi wakati ambapo polisi hao walitumia gari binafsi ambalo ni vigumu kwa wao kubaini,’ kiongozi huyo alibainisha.

Katika hali nyingine iliyothibitisha ukubwa wa mtandao huo ni tukio la kutatanisha la kuibiwa kwa kunyakuliwa kwa simu ya mzee Sharif aliyokuwa akiitumia kwa mawasiliano na majambazi kabla ya kufika nyumbani kwake baada ya kumkomboa mwanaye kwa malipo ya mamilioni ya pesa.

Hata hivyo, mwandishi wetu alipowasiliana na wazazi wa mtoto Fardosa Mohamed Othumani ili waeleze kwa undani tukio hilo walisema hawako tayari kufanya hivyo kwa usalama wao na pia kesi hiyo tayari iko katika uchunguzi wa polisi
Aidha, baadhi ya wakazi wa Kata ya Wailes ambako tukio hilo limetokea walieleza wasiwasi wao baada ya kuibuka kundi hilo la utekaji watoto la Mafia na kisha kudai mamilioni ya shilingi na wengi walikuwa na maoni tofauti kuhusiana na sakata hilo.

“ Nahisi hii ni aina mpya ya ujambazi ambao ni hatari sana kwani watoto wetu watakuwa wanatekwa ili wazazi tuwakomboe kwa kutoa mamilioni ya pesa, huu ni mtihani mwingine kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye jukumu la usalama liko mikononi mwake kwa kutumia vyombo vya dola,” alieleza Mama Kibibi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi ameelezea kuwa jeshi lake limepokea taarifa ya kuwepo kwa aina hiyo ya ujambazi na tayari wameanzisha msako mkali wa kuwabaini wote wanaojihusisha na masuala hayo ya utekaji nyara.

Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipofuatwa na waandishi wetu ofisini kwake, aliwakabidhi kwa msaidizi wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Evarist Mangara ambaye alielezea mikakati ya kupambana na ujambazi jijini.

Bw. Mangara alisema jeshi la polisi tayari limeweka mikakati ya kuwanasa majambazi wote katika mpango aliouita Inter district operation ambapo polisi wengi wanafanya msako katika wilaya moja baada ya nyingine kwa pamoja.

“Kwa tukio hili tunafanya Intensive investigation (Upelelezi wa kina) ili kuwabaini, ni tukio geni na limetushitua sana. Tutafanya ukaguzi nyumba hadi nyumba ambazo zinatuhumiwa kuhifadhi majambazi na ninawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwa majambazi wanaishi katika jamii yetu,” alisema Mangara.

Aidha, Mangara aliwataka wazazi kuchunga watoto wao kwa kuwaelekeza watu wanaobaki majumbani mwao wakiwa hawapo kuwa makini. Kuhusu kutokamatwa kwa watekaji kamanda huyo alisema watekaji hao walinasua mtego wa polisi baada ya kumuamuru mzee Shariff ambaye alikuwa katika gari lake kushuka na kutembea kwa miguu, kitu ambacho polisi hawakukijua, hivyo kupoteana na vijana wake ambao walikuwa katika gari lingine wakimfuatilia.

My Take:
Endapo jambo hili linaanza kufanyika kwa watu wa mbali na kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kama phones etc na internet (which is possible). Huko tunakokwenda tujiandae kusikia watoto wa vigogo na watu wanaotuhumiwa ufisadi watakapoanza kutekwa na familia zao kudaiwa fedha za kuwagomboa. Sijui ni kwa kiasi gani Jeshi letu lina uwezo wa kutrack na kufuatilia mawasiliano ya namna hii ikiwemo live GPS positioning.

Vinginevyo, miezi michache inayokuja especially towards 2010 na kwa kadiri watu wanavyozidi kukata tamaa tujiandae kusikia matukio makubwa namna hii.
 
Vinginevyo, miezi michache inayokuja especially towards 2010 na kwa kadiri watu wanavyozidi kukata tamaa tujiandae kusikia matukio makubwa namna hii
.

Hao majambazi/Black Mafia na wenyewe wajiandae kutandikwa risasi maana watoto wa vigogo aka mafisadi (at least wengi wao) wana pack heat vile vile.
 
Mimi naona wawateke wale mafisadi wenyewe na waseme bila kesi kufunguliwa wasiachiwe.

Nchi haina uongozi hiyo na inaonyesha huo ndio mwanzo wa Guerilla war tactics kama hakuna mabadiliko.

Na hiyo ni wazi inaanzia from within...Mtandao wameundiwa mtandao.
Unaambiwa ugaidi unamalizwa kwa kutumia ugaidi.

Watoto wa vigogo wana madharau sana!
Halafu eti wanataka kurithi nchi!
Nani kasema?
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu wahalifu au maghaidi kitu kimoja wanachofanya kwanza ni 'trial runs" ambapo wanajaribisha ni rahisi kwa kiasi gani kufanya utekaji au uhalifu wao. Siwezi kushangaa hao jamaa wamejaribu kubeep tu na kuona how long it'll take the Police kuwakamata. Sasa ni karibu wiki mbili tangu tukio hili litokee na wapelelezi wetu walikuwa na haraka ya kwenda kwa Kubenea badala ya kuweka nguvu zao kuwatia mbaroni hawa jamaa.

Vinginevyo tujiandae kwa uhalifu wa aina nyingine kabisa ambao bado hatujauona Tanzania.
 
Hivi na huyo Gogo ni nani?
Ni usalama wa Taifa ama mtoto wa Kigogo?

Hayo mambo ya ajabu aliyofanyiwa mama yetu Killango kama ni kubakwa...Basi NCHI ITAMWAGA DAMU!
KAMA MAMA KILLANGO ALIBAKWA SERIKALI IJIUZULU MARA MOJA LA SIVYO VITA NA IANZE!
Huu NI UHUNI ULIOKUBUHU NA UMAFIOSO!
Watanfanyiaje mama wa atu matendo maovu jamani!
Hivi kweli Mungu yupo?

JMUSHI
HIVI HILE POST ILITUMWA NA NANI VILE?mie nataka jamaa hayamwage hapa hayo mabaya kama akishindwa basi ani pm mimi
 
MKJJ kwenye maswala ya GPS itakuwa ngumu kidogo maana mitaa yetu haiko kwenye system...the best it can do ni kukuambia distance na direction...

NN, hii(Black Mafia) inanikumbusha BMF(Black Mafia Family)..
Anyways inategemea na wanaofanya hivyo vitendo ni mtandao ulioko chini ya mafisadi au kikundi cha vijana wasio na ajira wamekuwa inspired na movies wakaamua kuform kundi lao la ulaji?
 
kumekucha,ama kweli lisemwalo lipo kama halipo laja

Cha muhimu ni kwamba maelezo yote yana connect the dots kuanzia pesa za Kabila ambazo zilitokana na URANIUM ya IRAN.

Sasa Mwinyi na Salmin na Hata Mkapa waliowa na kuuza nchi..Na sasa tunaendelea kuwarithisha mali zetu hawa watoto wa Vigogo kina Mwinyi na wengineo kama vile kile walichopora hakiwatoshi.

Sasa huyu mke mwarabu si ndiye yule MKJJ aliyekuwa akisema ni dada wa Rostam pale aliposema RA ana ushemeji na JK?

Ama ana mwarabu mwingine tena?
Na kauziwa Serengeti sasa kama hii nchi si ya JK NA RA basi endeleeni kuniita kichaa na ukweli mtauona!

Sasa huko si ndio Wangwe alienda kukutana na RA?

Ee Mungu OKOA TAIFA LETU!

7.Ubadhirifu.
Aliweza kujichukulia eneo ndani ya mbuga za wanyama kule Serengeti na sasa anajenga hotel ya kisasa nah ii anaijenga yeye kwa ubia na mke wake huyo wa uarabuni akishirikiana na mashemeji zake hao , swali la kujiuliza ni je?huu mkataba hautaishia kwenye kuliuza taifa hili?
Mke anaenda kupewa mahari ya rasilimali zetu? Kama kila rais akioa ni sharti atoe sehemu ya mbuga zetu je? Mpaka lini tutakuwa tunachezea taifa kwa faida za kuoa ama kupata ngono!
 
Huu mtandao wote ni mtandao wa POLISI, Polisi wanahusika kwa 100% na ndio wanaotoa taarifa kwa majambazi kwani nao wanamgao wao. Mimi Jeshi la Polisi la Tanzania siliamini hata kidogo kwani ni Jeshi la majambazi. Kweli wengi wao ni majambazi Ule mfano wa ZOMBE na wenzake sio particular case ni General Case ya Jeshi la POLISI Tanzania karibia 95% wote wanamawazo ya kujitarisha na katika jeshi la polisi kujitarisha maana yake ni kula dili na wahalifu ili wakupe Commission.

Mnakaa kwenye vikao mnapanga mikakati halafu mkitoka jamaa wanawataarifu majambazi hameni leo tunakuja kufanya Ambush. JESHI LA POLISI LIANZE KUJISAFISHA KWA KUAJIRI WATU WAADILIFU NA WALIoPATA MAFUNZO MAZURI YA KISASA SIO KUWAWEKA WATU CCP PALE MOSHI WANAJIFUNZA SHABAHA NA MCHAKAMCHAKA, UNASEMA WAMEFUZU. NI WAKATI WA JESHI LETU SASA KUWA LA KISOMI, KUNA DEGREE NA MASTERS ZA SECURITY HUKU KWA WENZETU ZINATOLEWA SISI WETU WANASOMA LLB BASI ILI WAPANDE VYEO NA KUSHIRIKIANA VIZURI NA MAJAMBAZI.
 
MKJJ kwenye maswala ya GPS itakuwa ngumu kidogo maana mitaa yetu haiko kwenye system...the best it can do ni kukuambia distance na direction...

NN, hii(Black Mafia) inanikumbusha BMF(Black Mafia Family)..
Anyways inategemea na wanaofanya hivyo vitendo ni mtandao ulioko chini ya mafisadi au kikundi cha vijana wasio na ajira wamekuwa inspired na movies wakaamua kuform kundi lao la ulaji?

Free Big Meech....

BMF walikuwa wako sophisticated sana kushinda hawa wenye njaa wa bongo....
 
Hii mada haihusu watoto wa viongozi kwa maana inakoelekea. Lengo la mada ni kuonesha kuwa as long as ni watoto wa "uraiani" au wafanyabiashara wanatekwa, viongozi wetu hawatashtuka sana na kulipa umuhimu. Na kwa kadiri hawa jamaa wa Black Mafia au (wenzao) watafanikiwa kutumia teknolojia ya kisasa kuteka watoto/watu na kudai malipo na wakalipwa utaona ni jambo ambalo litawafanya wathubutu zaidi.

Huko nyuma watu walikuwa wanaiba na kuvamia kwenye nyumba za watu waliowadhania ni matajiri. Baada ya kukua kama uyoga kwa taasisi za benki na mabaa kila kona majambazi wakaanza kuachana sana na kuvamia nyumba za watu na kuamua kwenda kwenye fedha nyingi.

Endapo mtindo huu wa kuteka, kudai malipo na baadaye kupatiwa fedha hizo kiulaini kutaendelea, nina uhakika wataachana na soft targets na wataanza kufuata wanaodhaniwa kuwa na fedha zaidi, ni nani hao katika jamii yetu? Wafanyabiashara wakubwa, Wanasiasa wakubwa, na viongozi wakubwa ambao wanaonekana kuwa na fedha. Badala ya kuwashambulia au kuvamia nyumba zao watawania watoto wakiwa shule, sokoni barabarani n.k na kwa vile kama alivyosema Icadon hatuna uwezo wa GPS basi watatumia teknolojia hii hii kufanya uhalifu huo.

Hivyo siyo lengo langu kutarget watoto wa viongozi, watawala, au wafanyabiashara wakubwa nimejaribu kufikiria tu for few seconds like a criminal would.
 
Aliyeharibu hapa ni wewe, kama una ushahidi zaidi ya nilioutoa uweke hapa au niwekee kwenye PM, kama huna basi ni bora unyamaze tu!

Kwa sababu kama kweli una uwezo mkubwa wa kufikiri na kusoma, basi ungeelwa kuwa mimi sio niliyeanza kutoa hizi sumu, wewe ndiye uliyeanza na kusema kuwa utatoa ushidi zaidi kwenye PM,

Sasa ninarudia tena kuwa ninakupa nafasi tena sema hapa kama una mengine zaidi ya ushahidi au utume kwenye PM kama ulivyoahidi, mkuu hapa ni suala la ukweli au uongo wa sumu zilizotemwa, sio PM wala hizo nonesense zako, kama una ukweli zaidi uweke hapa usipoteze muda wa wananchi hapa na maneno matupu, na mijadala isiyokuwa na kichwa wakati kichwa kimewekwa tayari,

Aliyeharibu hapa ni wewe ambaye huna hoja, ila kazi kurukia tu as soon unapoona jina la Mama Kilango limetajwa, sasa weka ukweli mkuu wa hizi sumu!

Are you sure ni mimi Kana-Ka-Nsungu?
 
...Chuki za kidini na Kikabila dhidi ya wachagga ambao wamekuwa mwiba kwa kila aina ya mkoloni zinaelekea kuzaa matunda kwani kuna mamluki kama kina Wangwe ambao walikutana kwenye hoteli hiyo ya waarabu huko Serengeti!
Watanzania tukatae.

Mushi unajua Wachaga siku wakija kuwa kweli discriminated halafu uka sound alarm hautasikilizwa kwa sababu umesha sound false alarms nyingi.

Wachaga hawachukiwi kiasi cha kuichomeka chomeka hiyo ishu kila pasipohusika .

Unapiga mayowe "simba, simba," ngoja siku atokee simba kweli!
 
Hivyo siyo lengo langu kutarget watoto wa viongozi, watawala, au wafanyabiashara wakubwa nimejaribu kufikiria tu for few seconds like a criminal would.

Nina uhakika kuna baadhi ya watu hawajaelewa MKJJ anazungumzia nini mpaka sasa...Kwenye hili swala wasi wasi wangu ni lisije kuwa ni kambi moja ya wenye hela(the so called untouchables wa Tanzania) wameamua kuanzisha kikundi chao cha kulipa kisasi dhidi ya kambi nyingine mainly politicians our business rivals.
 
Kwa kuwa aina hii ya wizi ni mpya kwa Tanzania, polisi wana wajibu wa kujifunza kila mbinu katika karne hii ya 21.

Kwa suala la hao wanaojifanya ma-gangsters wa kutaka fedha za mchekea ni lazima wadhibitiwe kwa mbinu mpya na kisasa.

Na kwa kuwa ujambazi wa aina hii unatokea kila siku katika nchi za Colombia, Brazil, Argentina, Venezuela na kule Niger Delta basi ni budi polisi wetu nao wakenda kupata vikozi vifupi kuhusu namna ya kudhibiti hali hii na ikiwezekana kuwepo na special force kwa ajili hio.

Kuhusu simu za mobile nafikiri mitambo ya zimu (mast) inawasadia sana polisi kuwapata "victims" kutegemea na simu kuwa "on" mpaka pale inapozimika.

Kwa wale wataalam wa mawasiliano wanafahamu kwamba simu inapokuwa "on" inakuwa akiwasiliana na "mast" yoyote iliopo karibu na simu hio na endapo itazimikia eneo hilo bado registration ya "IMEI number" (International Mobile Equipment ID) yake itakuwa imefanyika na kuweka details kwamba ni muda gani, hivyo kuwapa polisi nafasi ya kujua last location ya victim.

Kuhusu GPS nafikiri hakuhusiani na uwezo wa polisi kujua location ya simu hio isipokuwa kama chombo hicho kina hio software ya kutumia GPS ambayo nafikiri kwa Tanzania ni lazima gharama za kulipia zitakuwa kubwa.

Ila yote inategemea na kukua kwa teknology kwa kiasi kikubwa.
 
My Take:
Endapo jambo hili linaanza kufanyika kwa watu wa mbali na kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kama phones etc na internet (which is possible). Huko tunakokwenda tujiandae kusikia watoto wa vigogo na watu wanaotuhumiwa ufisadi watakapoanza kutekwa na familia zao kudaiwa fedha za kuwagomboa. Sijui ni kwa kiasi gani Jeshi letu lina uwezo wa kutrack na kufuatilia mawasiliano ya namna hii ikiwemo live GPS positioning.

Vinginevyo, miezi michache inayokuja especially towards 2010 na kwa kadiri watu wanavyozidi kukata tamaa tujiandae kusikia matukio makubwa namna hii.

Hii nafikiri bado kwani inabidi wawe wanawasubiri pale uwanja wa ndege kila likizo zinapowadia kwani wengi wapo nje ya nchi.

Sasa itabidi polisi wawe wanajazana uwanja wa JK Nyerere!

Au wote tu wapige kambi pale uwanja wa JK Nyerere International Airport ingawa ni wazo "suicidal" kuliko yote.
 
Kwa kuwa aina hii ya wizi ni mpya kwa Tanzania, polisi wana wajibu wa kujifunza kila mbinu katika karne hii ya 21.

Kwa suala la hao wanaojifanya ma-gangsters wa kutaka fedha za mchekea ni lazima wadhibitiwe kwa mbinu mpya na kisasa.

Na kwa kuwa ujambazi wa aina hii unatokea kila siku katika nchi za Colombia, Brazil, Argentina, Venezuela na kule Niger Delta basi ni budi polisi wetu nao wakenda kupata vikozi vifupi kuhusu namna ya kudhibiti hali hii na ikiwezekana kuwepo na special force kwa ajili hio.

Kuhusu simu za mobile nafikiri mitambo ya zimu (mast) inawasadia sana polisi kuwapata "victims" kutegemea na simu kuwa "on" mpaka pale inapozimika.

Kwa wale wataalam wa mawasiliano wanafahamu kwamba simu inapokuwa "on" inakuwa akiwasiliana na "mast" yoyote iliopo karibu na simu hio na endapo itazimikia eneo hilo bado registration ya "IMEI number" (International Mobile Equipment ID) yake itakuwa imefanyika na kuweka details kwamba ni muda gani, hivyo kuwapa polisi nafasi ya kujua last location ya victim.

Kuhusu GPS nafikiri hakuhusiani na uwezo wa polisi kujua location ya simu hio isipokuwa kama chombo hicho kina hio software ya kutumia GPS ambayo nafikiri kwa Tanzania ni lazima gharama za kulipia zitakuwa kubwa.

Ila yote inategemea na kukua kwa teknology kwa kiasi kikubwa.

Hii ya kutrack simu ni very easy inaitwa Triangulation, inawapa exact locations up to within metres as long as simu iko on...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom