Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,763
- 40,988
Kutoka "Uwazi"
Habari hii niliisikia siku chache zilizopita. Naona bado iko hewani:
Mtandao mkubwa wa majambazi wanaotumia mbinu mpya za utekaji nyara uliopachikwa jina la Black Mafia umeibuka katika Jiji la Dar es Salaam na kuzusha hofu kubwa ya usalama wa raia na watoto wao.
Kujulikana kwa mtandao huo kumetokana na tukio la hivi karibuni la utekaji nyara wa mtoto mwenye umri wa miaka miwili, Fardosa Mohamed Othumani mkazi wa Mtoni Sabasaba lililofanywa na kikundi hicho cha utekaji nyara.
Akielezea kwa masharti ya kutotajwa jina lake, mmoja wa viongozi wa serikali ya Mtaa uliotokea tukio hilo, Kata ya Wailes, Changombe alisema kuwa majambazi hao wana kikundi kikubwa kinachosaidia kufanikisha kazi zao.
Watekaji hao wana mtandao mkubwa kwani mzee Mohamed Shariff, baba wa mtoto aliyetekwa, kila alilokuwa akilifanya ili kumnasua mtoto wake lilikuwa likiwafikia majambazi na kisha baba huyo kutaarifiwa kwa njia ya simu, alishangaa kuulizwa kwa nini anakwenda na polisi wakati ambapo polisi hao walitumia gari binafsi ambalo ni vigumu kwa wao kubaini, kiongozi huyo alibainisha.
Katika hali nyingine iliyothibitisha ukubwa wa mtandao huo ni tukio la kutatanisha la kuibiwa kwa kunyakuliwa kwa simu ya mzee Sharif aliyokuwa akiitumia kwa mawasiliano na majambazi kabla ya kufika nyumbani kwake baada ya kumkomboa mwanaye kwa malipo ya mamilioni ya pesa.
Hata hivyo, mwandishi wetu alipowasiliana na wazazi wa mtoto Fardosa Mohamed Othumani ili waeleze kwa undani tukio hilo walisema hawako tayari kufanya hivyo kwa usalama wao na pia kesi hiyo tayari iko katika uchunguzi wa polisi
Aidha, baadhi ya wakazi wa Kata ya Wailes ambako tukio hilo limetokea walieleza wasiwasi wao baada ya kuibuka kundi hilo la utekaji watoto la Mafia na kisha kudai mamilioni ya shilingi na wengi walikuwa na maoni tofauti kuhusiana na sakata hilo.
Nahisi hii ni aina mpya ya ujambazi ambao ni hatari sana kwani watoto wetu watakuwa wanatekwa ili wazazi tuwakomboe kwa kutoa mamilioni ya pesa, huu ni mtihani mwingine kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye jukumu la usalama liko mikononi mwake kwa kutumia vyombo vya dola, alieleza Mama Kibibi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi ameelezea kuwa jeshi lake limepokea taarifa ya kuwepo kwa aina hiyo ya ujambazi na tayari wameanzisha msako mkali wa kuwabaini wote wanaojihusisha na masuala hayo ya utekaji nyara.
Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipofuatwa na waandishi wetu ofisini kwake, aliwakabidhi kwa msaidizi wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Evarist Mangara ambaye alielezea mikakati ya kupambana na ujambazi jijini.
Bw. Mangara alisema jeshi la polisi tayari limeweka mikakati ya kuwanasa majambazi wote katika mpango aliouita Inter district operation ambapo polisi wengi wanafanya msako katika wilaya moja baada ya nyingine kwa pamoja.
Kwa tukio hili tunafanya Intensive investigation (Upelelezi wa kina) ili kuwabaini, ni tukio geni na limetushitua sana. Tutafanya ukaguzi nyumba hadi nyumba ambazo zinatuhumiwa kuhifadhi majambazi na ninawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwa majambazi wanaishi katika jamii yetu, alisema Mangara.
Aidha, Mangara aliwataka wazazi kuchunga watoto wao kwa kuwaelekeza watu wanaobaki majumbani mwao wakiwa hawapo kuwa makini. Kuhusu kutokamatwa kwa watekaji kamanda huyo alisema watekaji hao walinasua mtego wa polisi baada ya kumuamuru mzee Shariff ambaye alikuwa katika gari lake kushuka na kutembea kwa miguu, kitu ambacho polisi hawakukijua, hivyo kupoteana na vijana wake ambao walikuwa katika gari lingine wakimfuatilia.
My Take:
Endapo jambo hili linaanza kufanyika kwa watu wa mbali na kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kama phones etc na internet (which is possible). Huko tunakokwenda tujiandae kusikia watoto wa vigogo na watu wanaotuhumiwa ufisadi watakapoanza kutekwa na familia zao kudaiwa fedha za kuwagomboa. Sijui ni kwa kiasi gani Jeshi letu lina uwezo wa kutrack na kufuatilia mawasiliano ya namna hii ikiwemo live GPS positioning.
Vinginevyo, miezi michache inayokuja especially towards 2010 na kwa kadiri watu wanavyozidi kukata tamaa tujiandae kusikia matukio makubwa namna hii.